MHADHIRI ANAMNYANYASA Mwanafunzi wa kike

MHADHIRI ANAMNYANYASA Mwanafunzi wa kike

INSONSILE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
1,960
Reaction score
2,945
Kuna rafiki yangu anasoma chuo kimoja hapa nchini ambacho kwa kipindi hiki wanafunzi wa Education mwaka wa kwanza na wa pili wako field- Teaching Practice (hapo nadhani mtakuwa mmepata jibu ni chuo gani). Wiki iliyopita amenipigia simu kuwa kuna lecturer amempigia simu kuwa amechagua kuja Dar kufanya assessment kwa ajili yake. Na baada ya hiyo simu akawa anamtumia message za mapenzi. Binti akawa anampotezea na kumkwepa. Hatimaye jamaa akamshsinikiza binti kuwa anataka wakutane private place (hotelini) ili waspend muda pamoja. Binti akakataa. Sasa jamaa amemwambia binti maneno haya, "Unajifanya mjanja eeh!! sawa tutaona..."

Sasa leo asubuhi amenipigia kuniomba ushauri na inaonekana amekuwa frustrated. Nimejaribu kumshauri kuwa atunze message zote anazotumiwa, then amripoti kwa uongozi wa chuo ili ashughulikiwe kisheria maana anaweza kumfelisha makusudi. Pia atunze hizo msg ili ziwe ushahidi. Pia nimemwambia amwambie ukweli kuwa huko tayari kufanya hicho anachotaka, na akimfanya lolote utamshitaki kwa wahusika.

Lakini binti inaonekana mwoga kiasi anasema anaogopa kwani akipeleka litakuzwa na jina lake litakuwa gumzo hapo chuoni. Nimemwambia afanye uamuzi mgumu kwani itakapofikia hatua amefelishwa ndo aanze kulalama it will be too late.
Zaidi ya hapo nimshaurije?
 
Sasa kama unaogopa hata kuitaja DUCE sijui we mwenzetu utashughulikiaje suala hili!
Huyo mchumba wako akuambie vizuri walianzaje mahusiano...kwasababu mwalimu huyo asingechagua tu kuja Dar ikiwa hakuna historia ya nyuma!
Kuna mahala wanashindwana ndiyo maana ameamua kukujulisha!
Mwambie akusimulie na stori ya nyuma!
 
kama anaogopa jambo kukuzwa na jina lake kujulikana mwambie ajiandae kutoa papuchi au kupata supp,halafu hapa jf najua kuna wahadhiri jamani ndo nini baadhi yenu kuwashikisha ukuta watoto wa watu kila kukicha kisingizio eti degree yako iko mikononi mwangu,hivi kweli roho ya utu ishawatoka kabisa.
 
DUCE iko dar halafu mhadhiri kachagua kuja Dar mbona hapa sipati connection,halafu kwa chuo kama DUCE hadi mhadhiri kumfahamu mtu ni vigumu hao watakuwa wanajuana au huwa wanagongana sehemu bhana si bure.
 
Mmmh, PakaJimmy, mbona DUCE wanaenda field mwezi wa saba? Duce, Muce na Mlimani wote ni mwezi wa saba, lets think another college,

Lakini huu ni udhalilishaji mhusika asiufumbie macho. Kama yeye wa chuo kikuu anaona aibu kuripoti, itakuwaje wale wa mtaani wasiosoma?
 
Last edited by a moderator:
Bila shaka ni St. Augustine hiyo, kuna rafiki yangu anasoma ruco nimemwuliza anasema yuko field. Huyo mhadhiri naye ---- tuu na mshamba kupitiliza. Hajui anaihatarisha kazi yake. Alafu vyuoni siku hizi wasichana kibao wanajilengesha wenyewe kwa walimu. Mapepo gani yanampeleka kwa mtu asiyemtaka? Laiti ningemfahamu ningemtafutia waandishi wa habari wamuanike. Mtoa mada plz niinbox basi tuifanyie kazi hii issue, iwe fundisho kwa wahadhiri washenzi kama hawa.
 
Huyo lazima atakua lecturer wa RUCO Iringa, njia nzuri ya kumsaidia huyo dada ni kumtaja wazi wazi huyo lecturer ili tabia yake ikome
 
Tukatae tukubali, Tutorial assistant wa vyuo vyetu vingi ni washamba na wametokea maisha duni kubakizwa chuoni kufundisha wanaona wapo mbali sana...

Sasa kwa mtu mwenye akili yake umfosi mdada kimapenzi halafu umwambie anajifanya mjanja si ujinga huo... Mtoto wa chuo anakuzidi ujanja wakati we upo vizuri,, ni kitendo cha kucheza na saikolojia tu ya mdada mwenyewe anajaa na anafosi hadi harusi...

Hadi kutongoza ni janga la taifa siku hizi...

Shukuruni mnawapata wadada na wanafunzi wanyonge mkikutana na pasua kichwa akaamua kuwanyosha lazima make sawa,,,

Mi mtu anaetumia ubabe kupata kitu ni adui yangu wa kudumu,, kuna mmoja Mzumbe alitaka kukata Course work yangu kisa sikufanya last assigment eti ananikata maksi 10 hilo balaa lake atanisahau ( ulikuwa ni mkwara tu sema aliogopa huyo hata sup hakunipa)
 
Bila shaka ni St. Augustine hiyo, kuna rafiki yangu anasoma ruco nimemwuliza anasema yuko field. Huyo mhadhiri naye ---- tuu na mshamba kupitiliza. Hajui anaihatarisha kazi yake. Alafu vyuoni siku hizi wasichana kibao wanajilengesha wenyewe kwa walimu. Mapepo gani yanampeleka kwa mtu asiyemtaka? Laiti ningemfahamu ningemtafutia waandishi wa habari wamuanike. Mtoa mada plz niinbox basi tuifanyie kazi hii issue, iwe fundisho kwa wahadhiri washenzi kama hawa.

Nadhani kabla hajafanya chochote kuhusu hizo messages...ahakikishe kuwa hiyo namba ya simu iliyotumika kutuma hizo msgs imesajiliwa kwa jina la huyo mhadhiri...la sivyo akienda kushitaki chuoni/polisi halafu jina la mwenye namba ni tofauti itakula kwake! Nachelea kuamini kama huyo mhadhiri anatumia simu aliyosajili kwa jina lake kutongozea wanafunzi na kuwapa vitisho!
 
lecturer huyo atakuwa humu JF
mtaje jina kabisa hapa tuanze kumshughulikia
kama ulivoambiwa tunza kila kitu chake kama msg nk
ole wake akufelishe na hata ujumbe huu wa JF utakuwa ushahidi pia
pls mtaje waziwazi hana adabu huyo na hastahili kuwa mhadhiri
 
Sasa kama unaogopa hata kuitaja DUCE sijui we mwenzetu utashughulikiaje suala hili!
Huyo mchumba wako akuambie vizuri walianzaje mahusiano...kwasababu mwalimu huyo asingechagua tu kuja Dar ikiwa hakuna historia ya nyuma!
Kuna mahala wanashindwana ndiyo maana ameamua kukujulisha!
Mwambie akusimulie na stori ya nyuma!

Jambo usilolijua ni kama usiku wa giza.
Chuo kikuu cha Dar-es-Salaam(DUCE,MUCE&MC)field yao itakuwa
July mwaka huu.
Jipange vzuri kabla ya kuongea!
 
Mpeleke global publisher!!!, cku izi pale kuna maitelenjesia,maninja,makomando, na mapaparazi!, hawatamuchelewesha mbona!
 
na ikibidi kama wakiongea kwa njia ya simu arekodi maongezi kwa siri.huo pia ni ushahidi mzuri tu.huyo jama itakuwa ndio tabia yake hiyo,na inabidi akomeshwe
 
Sasa kama unaogopa hata kuitaja DUCE sijui we mwenzetu utashughulikiaje suala hili!
Huyo mchumba wako akuambie vizuri walianzaje mahusiano...kwasababu mwalimu huyo asingechagua tu kuja Dar ikiwa hakuna historia ya nyuma!
Kuna mahala wanashindwana ndiyo maana ameamua kukujulisha!
Mwambie akusimulie na stori ya nyuma!

Whatever the case PJ, kama binti ameamua hamtaki, basi. Hilo linatosha . Atunze msg kama ushahidi. bahati nzuri electronic evidence inakubalika kisheria sasa.
 
na ikibidi kama wakiongea kwa njia ya simu arekodi maongezi kwa siri.huo pia ni ushahidi mzuri tu.huyo jama itakuwa ndio tabia yake hiyo,na inabidi akomeshwe

Right, tena atafute hata mwanasheria ampe preliminaries za kuuweka ushahidi vizuri.
 
kama anaogopa jambo kukuzwa na jina lake kujulikana mwambie ajiandae kutoa papuchi au kupata supp,halafu hapa jf najua kuna wahadhiri jamani ndo nini baadhi yenu kuwashikisha ukuta watoto wa watu kila kukicha kisingizio eti degree yako iko mikononi mwangu,hivi kweli roho ya utu ishawatoka kabisa.

Papuchi ni nini. We Asnam si umesema unajiandaa na Sabato, sasa maneno ya papuchi yanatoka kwenye kinywa chako. Nakutania anyway!
 
sio mkwawa kweli?

Anyway hizo message ndo ushahidi wake....tena ingekua mie mbona ningemwendea hewani namwambia ahakikishe nina A lasivyo naharibu kibarua chake
 
Back
Top Bottom