Mhadhara wa Donge washindwa kufanyika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mhadhara wa Donge washindwa kufanyika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by abdulahsaf, Jun 17, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=1][/h]Posted on June 17, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Waislamu waliofika katika viwanja vya Malindi baada ya kutawanywa na jeshi la polisi huko Mahonda ambapo walikuwa wakienda Donge. baadhi ya watu wameumizwa baada ya kupata kipigo kutoka kwa polisi wakiwemo wanawake ambao walikimbilia msikitini na kupata kichapo huko huko ndani ya msikiti
   
 2. J

  John W. Mlacha Verified User

  #2
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  udhalimu wa serikali ya ccm na kikwete utaisha lini??
   
 3. J

  John W. Mlacha Verified User

  #3
  Jun 17, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  msishangae wakija watu hapa na kusema kuwa askari wanatimiza matakwa ya kanisa ama ya pinda.
   
 4. B

  Bob G JF Bronze Member

  #4
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  May be ya weza kuwa mwarobaini wa kuzuia kuchanganya Dini na siasa na kuzaliwa kwa makundi ya kihuni na magenge ya KIGAIDI kama UAMSHO, polisi tembezeni kipiko kwa saana ili liwefundisho na kwa wabara wanaopenda kuiga mambo ya kigaidi kwa kutumia mgongo wa Dini
   
 5. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,315
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  UCHANGANYAJI WA DINI NA SIASA WAULIZE MAPADRI WAKO, HII NI KITU GANI ??? KUTOKA GAZETI LA KIONGOZI

  ‘Siasa bila dini ni uendawazimu’

  Na Lilian Nyenza


  Kanisa halitaacha kutoa mwongozo kwa watu wake hata kwa mambo ya kisiasa ukiwamo uchaguzi kwa kuwa, siasa bila dini ni sawa na uendawazimu.

  Aidha, imedaiwa kuwa tabia ya kuwalaghai vijana kuwa ni taifa la kesho, ndiyo inayowadumaza kiakili na kuwafanya watumiwe na wanasiasa kufanya fujo, badala ya kujitokeza kuongoza kwa kufuata taratibu za nchi.

  Mkurugenzi wa chama cha kifamilia cha Undugu Association Tanzania, Padri Baptiste Mapunda, alitoa kauli hiyo katika sherehe za kuuaga mwaka 2004 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2005, zilizofanyika katika ukumbi wa Parokia ya Mt. Yosefu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
  Mkurugenzi huyo wa UNDUGU ASSOCIATION TANZANIA alisema kuwa, Tanzania imeanza kuonesha dalili mbaya za machafuko kutokana na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa kuweka mbele ubinafsi.
  "Tukikaa kimya huku mambo yanaharibika katika jamii; eti tuwaachie wanasiasa wafanye watakavyo, tutakuwa hatutendi wajibu wetu na hivyo, Kanisa halitaacha kusema ukweli kwa maslahi ya umma hata kama unamkera mtu. Hii ni kwa kuwa tunajua wazi kuwa siasa bila dini, ni uendawazimu ambao mtu hajui akifanyacho kwa kuwa akili yake haijatimia kiroho." alisema.
  Aliitaka jamiii ya Kitanzania ijifunze thamani ya amani na siasa safi kutokana na hali ya amani na usalama katika nchi jirani za Rwanda na Burundi ambayo ni hatari na inasikitisha.
  Alisema vita na mauaji yanayoendelea katika nchi hizo, yanasababishwa na uroho wa madaraka wa watu wachache ambao hawajali utu wa wengine.
  Aliongeza kuwa, "Siku zote tunapaswa kukumbuka kuwa, amani na mapendo ambayo Mungu ametujalia, tunapaswa kuyaenzi sisi sote kwa kuwa siasa bila dini, ni sawa na uendawazimu."
  Padri Mapunda aliiasa jamii kuendelea kumuomba Mungu ili azidi kuwajalia amani,upendo na utulivu uliopo sasa, kuwa uwepo hata baada ya Uchaguzi Mkuu kupita.
  Amewataka Waamini kuwaombea viongozi wanyanyasaji kama Herode, wabadilike na hivyo, kuongoza nchi kwa haki na akawasihi Watanzania kuyashinda maovu kwa kutenda yaliyo mema.
  Hata hivyo, Padri Mapunda amewatahadharisha vijana kujiepusha kutumiwa na baadhi ya viongozi wa siasa, kwa nia ya kufanya fujo katika uchaguzi.

  "Vijana mara nyingi wamekuwa wepesi wa kurubuniwa na vijizawadi vidogo vidogo, ili wafanye kile wanachokitaka wanasiasa wabinafsi. Sasa mimi nasema mkae chini na mlitafakari hilo kwa makini. Mtakao angamia ni ninyi na si wao," alitahadharisha.


  Alisema vijana ni Taifa la leo na Taifa bila vijana limekufa, hivyo aliwasihi kuwaheshimu wazazi na walezi ili wapate kuishi maisha marefu na yenye heri duniani, kama walivyojaliwa kuuona mwaka huu mpya.
   
 6. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  kwa nini tufike hapa ili hali viongozi wetu wapo, je, tuamini kuwa kweli kabisa wameshindwa kukaa meza moja na kujadiliana ya kufanya. kama issue ni muungano mbona unajadilika vizuri
   
 7. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Tuna watawala wanaopenda kuburuza watu,hatuna viongozi
   
 8. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #8
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kwa nini usianze kujishangaa wewe mwenye kwa kushabikia vikundi kwa kigaidi!Vipi pinda ameshakuwa rais sasa?makanisa yataendelea kuwepo mbaka mwisho wa dahari,na kwa sasa tunafatilia mwenendo wa vikundi vya kigaidi kwa karibu zaidi!
   
 9. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hakuna udharimu wowote,kilichpo ni kuwa taifa linakabiliwa na tatizo la ugaidi,yatupasa tuungane sote ili tupambane na vikundi vya kigaidi!
   
 10. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  This time hawajachoma moto makanisa na mabaa? JUST FOR CURIOSITY!
   
 11. R

  RMA JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao ni vibaka tu hawana lolote la maana, wanastahili mkong'oto!!!
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hivi ndivyo alivyoandika Mervlyn Hiskett:

   
Loading...