Mh. Zitto: Tunasukumwa na Uzalendo wako

Said Bagaile

JF-Expert Member
Jun 23, 2011
686
256
Imekuwa ikishuhudiwa misururu ya watu wa kada mbalimbali ikienda kumtembelea Zitto kabwe hospitalini na wengi wetu tukiumia na kumwombea ili apone haraka kutokana na maradhi yanayomsumbua. Na laiti kama kungekuwa na uwezo wa kubadilishana afya, basi mimi binafsi ningeshauri hii afya ya Zitto kwa sasa wangebadilishiwa wale wote walioiingiza nchi yetu kwenye migogoro mikubwa ya kiuchumi lakini majitu haya hayataki hata kuugua japo mafua ili tufurahi.
Si Mh. Zitto pekee ambaye yupo kwenye sick bed mpaka sasa tuna Mawaziri karibu Watatu nao wapo huko huko India lakini wanaofuatilia afya zao kwa karibi pengine ni serikali na familia zao tu. Hii ni tofauti na Mh. Zitto ambae hali ya afya yake inakuwa kama inamgusa kila mtu hata nje ya Serikali, Chama chake na familia yake. Na hili halina tafsiri nyingine zaidi ya Uzalendo wake kwa nchi na Wananchi wake.
Zitto ni mtu wa Watu, japo si Waziri lakini kuugua kwake kumefunika maradhi ya Mawaziri ambao walikuwa wakijidhani ni maarufu sana.

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom