Akilitime
JF-Expert Member
- Dec 27, 2017
- 581
- 757
Wasalaam
Ndugu Waziri hongera kwa jitihada zako za kukabiliana na janga la Corona nchini.
Ushauri wangu kwako hawa wanafunzi wa secondary wenye mitihani yao ya mwisho pamoja na wanafunzi wa vyuo ni bora tu waendelee na masomo yao huko huko walipokuwa.
Nchi za wenzetu wamefunga shule lakini bado wanafunzi wao wanaendelea kupata masomo yao kupitia online learning! (Kurudi nyumbani hakuwaathiri)
Pia kulikuwa hakuna ulazima sana wanafunzi wa vyuo kurudishwa nyumbani kwao, kitu pekee kingefanyika vyuoni kwao ni pamoja na kudhibiti mihadhara mikubwa wakati wa ufundishaji, na hili wangeratibu manaopanga ratiba za ufundishaji huko vyuoni.
Shule za secondary za boarding zisizo na michanganyo ya watu kutoka nje, basi hawa wanafunzi wangebakizwa tu huko Shuleni wakiwa chini ya uangalizi wa walimu wao.
Swali je kama kukiendelea kuwepo viashiria vya virusi, inamaana masomo yatasitishwa nchini? Au serikali mmejipangaje juu ya hili?
Jana wataalamu wa afya nchini Marekani wanasema chanjo ya Corona yaweza patikana baada ya miezi 18, you see hili sio tatzo la kuisha saivi (Though God can intervine the spread)
Kuruhusu wanavyuo kurejea kwao na kuanza kuzurura mitaani pasipo kuweka Lockdown, Ni sawa na kuchochochea maambukizi tu.
Serikali liangalie upya watoto warudishwe waendelee na masomo, na Elimu ya kujikinga wapatiwe huko huko.
Pia suala la kusogeza mitihani mbele halitaathiri wanafunzi tu, bali hata Wizara itaathiriwa mno.
Ni ushauri tu, unaruhusiwa kuupinga kwa hoja zako, ili kwa pamoja tuendelee kudhibiti maambukizi ya virusi.
Hapa sio mahali pa kuonesha ujuaji bali Ni sehemu ya kujifunza, hivo toa maoni yako kwa lengo la kutuelimisha , na sio kucrash maoni ya mtu.
Mwisho: Sijapinga maamuzi ya serikali kufunga secondary na vyuo. Ninaunga mkono jitihada za serikali kwa kutoa maoni yangu.
Nawasilisha.