Mh. Waziri mkuu, angalia Halmashauri mpya zilizoanzishwa kwa karibu na umakini

DiwaniMteule

New Member
Nov 23, 2015
2
0
Hongera sana Mh.Majaliwa Kassim Majaliwa kwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu wa serikali yetu tulivu ya Tanzania.Tunakuomba angalia kwa makini hizi halmashauri mpya katika utendaji na ufanisi wake na hasa halmashauri za mikoa ya pembezoni ya nchi kama vile Kigoma,Ruvuma, Katavi na mingine iliyoko pembezon ikama hiyo.Kwa kuwa waifahamu sana wizara hii ya serikali za mitaa.

Tunategemea msemo wa HAPA KAZI TU upitie mpaka katika halmashauri za nchi yetu ili tuweze kuwa na Imani Zaidi na seikali yetu makini.Vilevile utumikaji wa raslimali za umma umekuwa sii wa kikazi za serikali,Rais amepunguza safari za maofisa waserikali kwenda nje ya Nchi ili kubana matumizi lakini katika hatua ya kushangaza utakuta kuwa magari ya serikali yanatumika kwa shughuli binafsi tofauti na za kiofisi hata siku za mwisho wa wiki kama jumapili.

Naomba tuangalie kwa makini pia.

ASANTE.
 
Nilidhani unashauri zifutwe. Binafsi, naona baadhi ya wilaya na halmashauri mpya nyingi zimeanzishwa along political lines bila kujali uwezo wa serikali kuhimili gharama kubwa kwa ajili ya uanzishwaji huo. Binafsi sio muumini wa hoja kuwa uanzishwaji wa wilaya mpya ndio suluhu ya kusogeza huduma karibu na wananchi.

Nianze kwa kusema hivi, ukizingatia gharama ya kuanzisha wilaya mpya dhidi ya huduma za kijamii utabaini kuwa ni gharama ndogo kupeleka huduma za kijamii ktk maeneo husika kuliko njia ndefu ya kuanzisha wilaya kwanza ndipo huduma ziwafikie wananchi.

Mfano, ili uanzishe wilaya kuna taasisi za lazima ambazo zinaambatana na hatua hii kama vile

1) taasisi ya Mkuu wa Wilaya (yeye na watumishi wengine ndani ya ofisi yake)
-Yatahitajika majengo kwa ajili ya ofisi na makazi ya mkuu wa wilaya
-Magari (V8) + mengine kwa ajili ya DAS na wengine
-Gharama ya kuajiri watumishi wapya - watalipwa mishahara na gharama za ajira mpya
-Vitendea kazi vingine kama computer, nk

2) Halmashuri ya wilaya na mji/miji
-Watahitajika wakurugenzi wa wilaya na mji/miji
-Majengo kwa ajili ya ofisi (hugharimu mabilioni ya fedha)
-Magari (V8 za wakurugenzi pamoja na magari ya wakuu wa idara na vitengo)
-Kuajiri watumishi wapya kwa ajira za kudumu

3. Jeshi la Polisi
- Kila wilaya inakuwa na jeshi la polisi kuanzia Kamanda wa Polisi wa Wilaya na askari wa chini yake
-Wanatakiwa kuwa na jengo kwa ajili ya ofisi
-Where necessary, wanalazimika kuajiri askari wapya


Nimeainisha haya maeneo kwa ufupi sana. Sasa ukikokotoa gharama inayohitajika kuanzisha wilaya mpya dhidi ya gharama halisi za huduma za kijamii zinazohitajika eneo husika utakubaliana nami kuwa kunatofauti kubwa.
Mabilioni yanayotumika katika majengo, kununua magari, kuajiri watumishi kuanzia mkuu wa wilaya, wakurugenzi, wakuu wa idara na vitengo, maafisa pamoja na jeshi la polisi yangeweza kupeleka huduma za afya, elimu. barabara, umeme, maji, na mambo mengine ya msingi kwa gharama ndogo.

Binafsi naona tumeamua kutumia njia ndefu ambayo haina tija ya haraka kwa walengwa tena ya ghali. Tungeweza kutatua kero za wananchi bila kupoteza gharama kubwa ya kuanzisha taasisi za wilaya mpya. Hii ndio sababu ya mapato mengi, karibu 60%, ya kila mwezi yanatumika kama mishahara. Kinachobaki ndicho kinagawanywa kwenye competing wants kama maji, afya, miundombinu, nk.

Ni mtazamo wangu huru. Ahsanteni


Hongera sana Mh.Majaliwa Kassim Majaliwa kwa kuteuliwa kuwa waziri mkuu wa serikali yetu tulivu ya Tanzania.Tunakuomba angalia kwa makini hizi halmashauri mpya katika utendaji na ufanisi wake na hasa halmashauri za mikoa ya pembezoni ya nchi kama vile Kigoma,Ruvuma, Katavi na mingine iliyoko pembezon ikama hiyo.Kwa kuwa waifahamu sana wizara hii ya serikali za mitaa.Tunategemea msemo wa HAPA KAZI TU upitie mpaka katika halmashauri za nchi yetu ili tuweze kuwa na Imani Zaidi na seikali yetu makini.Vilevile utumikaji wa raslimali za umma umekuwa sii wa kikazi za serikali,Raisi amepunguza safari za maofisa waserikali kwenda nje ya Nchi ili kubana matumizi lakini katika hatua ya kushangaza utakuta kuwa magari ya serikali yanatumika kwa shughuli binafsi tofauti na za kiofisi hata siku za mwisho wa wiki kama jumapili. Naomba tuangalie kwa makini pia. ASANTE.
 
Back
Top Bottom