Spika Anne Makinda kama anasoma hapa au kama kuna mtu wake wa karibua basi ningependa kumuambia kuwa hakuna mtu aliyeni-dissapoint kama Anne Makinda. Ameharibu kabisa heshma ya bunge, amegeuza bunge kuwa taasisi ya serikali. Bunge ni mdomo wa watanzania, ndio sehemu ya watanzania kupitia wawakilishi wao wanatunga sheria za nchi na pia kuhoji/kushauri wale wanaopewa dhamna ya kuongoza.
Lakini kwa sababu anazozijua yeye Anne Makinda, ameamua kuziba watanzania midomo (kuziba wabunge maana yake ni kuziba midomo watanzania waliowatuma). Mtindo wake wa kuongoza vikao vya wawakilishi wa watanzania kwa hasira, pupa, matumizi/tafsiri potufu ya kanuni za bunge na kujiona yeye ndiye mtu pekee anayezielewa kanuni za bunge imechangia sana kujenga chuki kati wa raia na serikali na kwa maana hiyo CCM. Bunge limekuwa la mabavu na mipasho. Ni afadhali mara 1000 Jenista Muhagama angekuwa Spika.
Wabunge wa CCM wanaweza kufurahia anachokifanya Makinda, lakini gharama za huu uendeshaji mbovu wa bunge watazilipa kwenye sanduku la kura. Ni nadra sana kumpata mtu anayeona kuwa Makinda anaendesha vikao vya bunge vizuri! Lakini pengine tukumbuke jambo moja, Anne Makinda ni mjumbe wa CC ya CCM. Hiki ndio chombo cha juu kabisa cha maamuzi ndani ya CCM. Hivyo ni vigumu huyu mama kwenda kinyume na maazimio ya CC. Hatuna bunge and certainly hatuna spika.