Toosweet
JF-Expert Member
- May 27, 2012
- 2,141
- 1,982
Heshima Kwenu,
Nimefuatilia Bunge kwa siku za karibuni na hasa Bunge la Bajeti na kugundua kuwa Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai anafanya bidii sana kuhakikisha ana-undermine hoja zonazotolewa na Opposition hasa na wabunge wa CHADEMA.
Wakati akichangia mjadala leo mbunge wa Kilombero Mh. Peter Lijualikali alisisitiza kuwa wote waliohusika na mikataba mibovu wasionewe haya iwe ni Mh. Chenge mbunge wa Bariadi na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa kuingia mikataba na marais waliokuwepo wakati huo(wa awamu ya tatu na nne). Baada ya kauli hiyo Mh. spika alitoa kauli za kejeli akionekana kupinga kwa kudai Mh. Lijualikali awe mwangalifu kwa kutaja marais wastaafu kwani hata upande wa pili kuna mawaziri wakuu wastaafu. Aliendelea kudai kuwa Mh. Lijualikali hana uzoefu ndio maana anaongea alivyoongea.
Kwa mtu mwenye dhamana ya spika, maneno ya Mh. Ndugai ni
maneno ya kibaguzi tena ya kejeli. Hayafai kutamkwa na Spika wa Bunge. Kabla ya hapo alikejeli pia kauli za wabunge waliosimamishwa kuhudhuria vikao kadhaa vya bunge Mh. Halima Mdee na mwenzake Mh. Ester Bulaya kuwa watakwenda mahakamani.
Ni kawaida kwa Mh. Spika na Naibu wake pamoja na wabunge wa CCM kutenda kama mawakala wa serikali kwa kujibu au kukosoa michango ya wabunge wa upinzani. Kuendelea kuwa na spika wa aina ya Mh. Ndlugai ni hatari kwa afya ya Bunge.Ikumbukwe pia kuwa Spika aliamuru Mbunge wa Kibamba Mh. Mnyika atolewe nje kama kibaka kisa kuomba mwongozo wa Spika kuhusu yeye kuitwa mwizi na Mh. Kibajaji. Inasikitisha sana kuwa spika anabagua wabunge anaowaongoza, kupendelea wa CCM na kupuuza wa upinzani hata kama wana hoja. Mwaka 2007 Mh. Zito Kabwe wakati huo akiwa CHADEMA alifukuzwa bungeni ikisemekana amelidanganya bunge alipodai kuwa Mh. Karamagi, Waziri wa Nishati na Madini wakati huo amesaini mkataba akiwa hotelini London, Uingereza. Ilikuja kubainika kuwa Mh. Zito alisema ukweli. Mambo waliyoyatetea wabunge wa CCM wakati huo pamoja na spika wao, ndiyo anayohangaika nayo Mh. Magufuli wakati huu, mikataba ya kijinga kwa sababu ya ushabiki wa kijinga wenye maumivu kwa nchi.