Ni kazi nyepesi sana kuwa spika wa bunge la Tanzania pengine kuliko nchi nyingine za Africa. Licha ya bunge letu kutokuwa na watu wenye weledi mkubwa (critical minds), pia bunge la Tanzania huendeshwa kibabe na spika hulindwa na chama tawala.
Sasa inapotokea spika wa bunge kama hilo anakuwa spika katika bunge ambapo kanuni, sheria na taratibu hazipindishwi kirahisi basi lazima spika huyo ataona machungu.
Hayo ndiyo yakiyomkuta Tulia Ackson akiongoza kikao cha umoja wa maspika duniani. Tulia alionekana kulalamika kwamba hapati heshima na kwamba anasulubishwa wakati akihojiwa kuhusu taratibu alizopaswa kufuata.
Jambo hili limekuwa kipimo cha ukomavu wa demokrasia yetu na weledi wa mtanzania mbele ya jumuiya ya kimataifa.