Mh Slaa ateta: Nafasi ya 30 Afrika haitoshi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Slaa ateta: Nafasi ya 30 Afrika haitoshi.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Zawadi Ngoda, Oct 15, 2010.

 1. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Mheshimiwa Slaa amezikubali kwa shingo upande takwimu za uchumi za mtandao wa Aneki.com, ambazo zinaiweka Tanzania katika nafasi ya 30 kati ya nchi 52 za Afrika kwa ulinganisho wa income per capita.

  Katika ulinganisho huo nchi ya kwanza ni Equatorial Guinea ($30200), ya pili Botswana ($15 000), ya sita S. Africa ($10500)....... ya 27 Ghana($1500)ya 30 Tz ($1400)........ya 52 Zimbabwe ($200)

  Mh Slaa ameahidi kuwa kama atatinga Ikulu basi ataipandisha Tanzania mpaka nafasi ya 3 baada ya miaka 5. Amesema kuwa Tanzania yenye madini mengi sawa na A. kusini haistahili kuwa nafasi ya 30.

  Tukirudi nyuma, nafasi hiyo ya 30 Tanzania haijawahi kuishika. Hii inaonyesha wazi kuwa kasi iliyoipata TZ ni kubwa sana na inaonekana wazi kuwa hata Mh Slaa anaikubali. Kwani sio sirio kuwa Tanzania tulikuwa tunacheza katika 10 bora katika umasikini duniani.

  Tutakuwa hatuna shukurani kama watanzania ikiwa pamoja na wapinzani hawatakubali kuwapongeza wote walioinyayua hadhi TZ yetu.

  Swali ninalojiuliza ni kama kweli sera za CHADEMA za uichumi zinaweza kutuweka nafasi ya 3? Je mwenzangu unaamini hayo?

  Cheap politics hatuzihitaji.
   
 2. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Uchumi bwana ni very complex. Huwa hakuna jibu rahisi katika hili. Ila halizuii watu kuweka malengo.
  Kiufupi ni kwamba hakuna nchi inayojitegemea, kwahiyo ufanisi katika uchumi hutegemea sera na utekelezaji wake wa ndani lakini pia na hali halisi ya nchi nyingine ambao ndio hasa wahusika. Pamoja na kuwa sera za uchumi za CHADEMA ni vague lakini inawezekana pia likatekelezeka km kuna usimamizi wa maana na hali ya nje ya nchi (kimasoko, madeni nk) inakuwa shwari.
  Pia Zawadi, pamoja na TZ kufika hapo bado inafanya vibaya saana hasa kwenye exchange rates. Wakati currency yetu ikitegemea saana performance ya dollar, wakati huu ambapo dollae inafanya vibaya na Tsh nayo ipo hoi. Hapa ndio ilikuwa pa kutokea.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160

  Inasikitisha sana Kikwete hajui kwanini Tanzania ni maskini!

  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/38756-kwa-nini-tanzania-ni-nchi-maskini-kikwete-hajui.html#post81337


  Hatudanganyiki kabisa ! Imetosha miaka 5 alofanya usanii
   
 4. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ndio maana kipindi hiki cha miaka 5 ya JK amejaribu sana kuitangaza TZ nje ya nchi na kujaribu kutafuta marafiki hata wale ambao siku za nyuma tuliishi nao kama paka na panya. Kitendop ambacho watu wengi Tanzania wamemlaumu.

  Akipewa majina mengi, kama Vasco n.k ni juhudi za kumvunja moyo jitihada zake za kutafuta marafiki kwa udi na uvumba.
  Uhusiano na nchi za nje ni muhimu sana katka kukuza uchumi.

  Sioni sababu kwanini tusimrudishe IKULU JK ili amalize kipande alichokibakiza? Kwanini tuhitaji Rais mpya?
   
 5. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
 6. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Huu ni upuuzi kwani nchi zingine tumezipita nini na Vasco da Gama wetu?
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Ufisadi uliokithiri ukiratibiwa na raisi Kikwete anayemaliza muda wake! Uongozi usiofuta sheria
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu mark my words, Zimbabwe na matatizo yao yoote they are 100 times better than us!
   
 9. m

  mosesk Member

  #9
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 5, 2010
  Messages: 44
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nafikiri Zawadi hajui vitu vingi, urafiki wa nchi siyo kama urafiki wa mtu na mtu, katika ulimwengu huu wa sayansi na technolojia siyo lazima upande ndege ueende marekani eti kisa kutafuta marafiki. Labda kama anatafuta marafiki zake hapo sawa, nchi ni taasisi ina viongozi katika kila ngazi. Tunahitaji mikakati ya maana siyo projo, mtu hupati sifa kwa umaarufu wa kuomba, utapata sifa kwa mikakati ya kujikwamua ili usiwe ombaomba.


  Mme hawezi kujisifia kwa mke wake kuwa yeye ni bingwa wa kuomba, Tanzania hii inaweza kujitegemea badala ya kuomba omba ni akkili kuacha madini yanachukuliwa halafu wewe unaenda kuomba chakula?


  Sasa hizo meli ambazo ameaahidi kila mkoa hata kusiko kuwa na mito au bahari tazipata kwa kutegemea misaada?


  Sisi m wanatakiwa wapumzike, wamechoka kwani wana hofu gani Dr. akachukua nchi hii jamani.
   
 10. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Jamani hivi mnaifahamu hiyo Equatorial Guinea ambayo imekuwa ya kwanza?? Ni ile nchi iliyokuwa na dikteta Nguema. Last month niliona documentary kuhusu hiyo nchi hasira zikanipanda. Ni kisiwa chenye utajiri mkubwa wa mafuta na population yake ni ndogo sana. Utajiri mkubwa uko kwenye mikono ya ukoo mmoja na cronies wa watawala. Wananchi walio wengi wanaishi kama vingunguti machinjioni. HIYO NDIYO NCHI INAYOSIFIWA KUWA NI YA KWANZA!!!!!.

  Kwa vigezo hivyo vya shirika hilo, unakuwa juu kwa kukandamiza watu wako na kuwapa utajiri wageni. Kwa hiyo ili tupande chati, inabidi ule mrahaba wa 3% tuushushe uwe 1%. Uranium tuwape bure watuletee 286 na 386 computers (ambazo kwao wanashindwa pa kuzitupa) shuleni kwetu through a clever NGO!!! Serengeti tuwape waiendeshe wanavyotaka na kuihamishia kwao.

  Kazi iko kwa Dr. Slaa
   
 11. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Lakini zawadi hiyo figure imetengenezwa na wachache. Inwezekana ni zao la matajiri kuzidi kutajirika na masikini kuwa vile vile au kufukarika zaidi. We have to discuss it with precaution.
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nadhani ni kweli Kikwete kajitahidi kuitangaza Tanzania duniani kama nchi maskini anayoiongoza na ina raslimali nyingi lakini hata yeye hajui ni kwa nini! kama hiyo ndio nafasi yake katika diplomasia hatumuhiaji tena ikulu wala kwenye anga za kimataifa.
  NAKUBALI KWAMBA DR SLAA NI CHAGUO SAHIHI KUWA RAIS WETU 2010-2015
   
 13. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Wo wo wo, let me guess who you are. A short and fat guy with an empty head (possibly a pumkin in its place), enjoying trips abroad fortnightly a month pocketing a whooping US$ 420 per day. Tell you what, you are the cause of poverty in this country. Counting down to 31/10, your days are numbered. Thats why you are all scared. You have turned into hyenas waiting for a hand to fall. It will not fall this time around
   
 14. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Takwimu za REDET tulizitilia shaka, za SYNOVATE vile vile, na hizi za aneki nazo tunazitilia shaka. Sasa niambieni msimamo wenu kuhusu Takwimu. Ni shirika lipi mnaliamini kwa Takwimu?

  Fahamuni Takwimu ni muhimu sana kwa kujipanga ki maendeleo, hivyo hatuwezi kuishi bila Takwimu. La msingi niambieni niende wapi kupata Takwimu sahihi za Tanzania?

  Msipoweza kunishauri niende wapi kupata Takwimu sahihi, basi picha ninayoipata ni kwamba Mh Slaa akitinga Ikulu basi atapinga marufuku kuzungumza kwa Takwimu.

  Kama hivyo ndivyo, basi huyu Mh Slaa hatufai kabisa, Tena hatufai haswa.
   
 15. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Zawadi hapa tunajadili professionally, si kisiasa. Yaelekea hukunielewa. Nilivyosema hizo hesabu ni za wachache nilimaanisha katika ukokotoaji wa GDP huo wastani uliopatikana inawezekana ikawa ni zao la matajiri wachache. Yaani wao wamekuwa matajiri zaidi na masikini aidha wamebaki vilevile au wamekuwa masikini zaidi kwahiyo inaggaregate value inaongezeka na mwishoni inaathiri GDP na kuifanya ionekane kubwa. Kiufupi sijabeza TAKWIMU za yoyote, mie nawaangalia tu watafiti saana nasoma walichoandika. Nikibeza basi huwa nina cha kusema ambacho hudhani kina impact. Lakini pia lazima ukubali hakubali research amabyo ipo free from criticism, otherwise watu wasingefanta research.
   
 16. Njilembera

  Njilembera JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2010
  Joined: May 10, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Zawadi, matumaini yangu ni kuwa wewe sio Ngoda ninaowafahamu. Unaelekea kuwa na akili mgando. Yaani tangu nimekujua sijakuona unafikiria tofauti hata mara moja! Unawezaji kuamini kwamba katika dunia ya leo ni lazima Raisi wa Nchi maskini azunguke dunia na kikapu mkononi anaomba omba kama Matonya. Kwa nini Kenya wanatuzidi na baadhi ya mawaziri wao walizuiwa hata kutembelea baadhi ya hizi nchi anazotembelea Kikwete. Kenya wana nini cha kujivunia kwa maana ya utajiri wa halisia (natural wealth). Sisi tuna kila kitu, angalia ramani ya Africa, nchi pekee iliyozungukwa na maji dira zote nne ni Tanzania, tuna dhahabu, almasi, uranium, gas, chuma, mkaa, ulanga, tanzanite, mbuga, milima, ardhi kibao halafu maskini.

  Nadhani pengine kwa lugha hii utanielewa vizuri na namnukuu Perry Sledge (sijui kama unamfahamu) kwamba 'unapokuwa na mke mrembo, kila mtu anampenda, na unakuwa na wageni wengi". Angalia Bush hapendi watanzania for heavens sake anapenda Mbuga vivyo hivyo kina Bill Gates, Clinton, na Carter. They know what they want from this country. Wakati wa JK Nyerere hawakuweza kumwingia, lakini huyu akiitwa anawahi, anapewa red carpet anatoa ruhusa KULENI TU! Huamki Zawadi! Tutakuwaje vi-puppet miaka nenda. HUNA UCHUNGU NA NCHI YAKO WEWE, Umenisikitsha sana
   
 17. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #17
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,999
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  mkuu nafasi ya 30 hailingani na mahandaki yaliyopo sasa, ingetakiwa walau iwe hata ya 6 au 10 kutokana na ukubwa wa mahandaki yaliyopo migoni kwa sasa.
   
 18. O

  Obama08 Senior Member

  #18
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I do wonder every time, when i read ur msgs, u look so arrogant, ignoramus, illerate, or inability to analyse issues, ref, ur words, kuitangaza TZ, kutafuta marafiki kwa udi na uvumba, damn..........!!!!!!!!! go to school, anyway, ur words i can tell ur uneducated, or chicken head ww, au umetumwa....!!? JF is a home of great thinkers, ww umetoka wapi..!? ufisadi, BOT theft, mikataba mibovu, makampuni mengi yamekufa, umaskini uliokidhiri, ujambazi, 1 usd = 1500 Tshs na bado inashuka, bidhaa ghali, wafanyakazi mishahara midogo, wananchi hawana vituo vya afya, afya ghali, maji bado kitendawili 50 yrs now, hizi ndio issues, ww unaongea upuuzi, ukitaka watu wasijue ur most stupid just shut up, hawatajua, don't expose ur ignorance at JF, CCM inakumbatia mafisadi, wauza drugs, wazee wa VX V8, vasities hali mbaya, ww unaongea upupu kama unayempigia debe, give him ur p...y!!!!!!!!! in short ww umezoa vizawadi then kwisha habari yako, kichwani hovyo, i hope ulipata O kama ulifika hata F4, CCM na ahadi, MELI, MEELII, MEEEEEEEEEEELIIIIIIIIII kubwa na za kisasa, uwanja wa kimataifa wa ndege labda VOLTURES ndio watue, Dubai itajengwa, kila mahali sasa Vyuo vikuu, hospitali za rufaa, n.k, these are lies, stop fake promises, stop lying, hatutaki kura za wafanyakazi, hata mkigoma miaka 8 hamtapata nyongeza, na polisi watawashughulikia mkiandamana,
  2010 ndio mwisho wenu
   
 19. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kwa sababu aliyepo ame prove failure!
   
 20. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ukitembelea website yao jamaa utagundua kuwa ina walakini

  Yaani Zimbabwe is poorest kuliko hata Somalia?????

  Kama wameconsider piracy nayo kama chanzo halali cham mapato basi inawezekana kwa tanzania wanahisi pesa za ufisadi wa EPA, RICHMODN NA RADA ni pesa ziliingia mifukoni mwa walalahoi.

  But let assume we trust the statistics. kuwa niza za kweli . Ni ni aibu kubwa sabbau tunazidiwa na RWANDA na KENYA . Yaani nchi iliyokuwa vitani inatuzidi

  Na mwisho kwa mujibu wa takwimu zinazoweka tanzania nafasi ya ya 30 kwafrika ni za UMASIKINI.

  Tembelea uone mwenyewe
  http://www.aneki.com/countries2.php?t=Poorest_Countries_in_the_World&table=fb129&places=*=*&order=asc&orderby=fb129.value&decimals=--&dependency=independent&number=all&cntdn=asc&r=-101-102-103-104-105-106-107-108-109-110-111-112-113-114-115-116-117&c=&measures=Country--GDP%20per%20capita&units=--$&file=poorest

  Kwa hiyo tunaweza kuwa ni wa 30 kwa umasikini lakini tukajikuta vile vile ni wa 40 kwa UTAJIRI. Hakuna cha kufurahisha hapo.
   
Loading...