Zikiwa zimasalia Takriban wiki mbili na ushehe mpaka uchaguzi mkuu, Mh Slaa ameweza kujikongoja toka 4% tar 5.9 mpaka 12% tar 7.10. Kwa kupata 12% amefunja rekodi ya wagombea wote wa urais wa CHADEMA katika chaguzi zilizopita. Haya ni maendeleo makubwa sana kwa Chama hicho, yanayostahili pongezi.
Licha ya kuvunja rekodi ya Chama chake, lakini kiwango hicho bado hakitoshi kumuingiza Ikulu. Hata hivyo ninahakika kabisa kuwa safari hii CHADEMA imesikika mbali zaidi, pengine mpaka 50% ya vijiji vya Tanzania. Kwa ushujaa huu wa Mh Slaa utakiwezesha Chama kupata wabunge wengi kati ya 12%-15% ya wabunge wote wa Tanzania. Huu ni ushindi kwa CHADEMA na ni ushindi kwa upinzani.
Tatizo litalojitokeza baada ya uchaguzi ni kuvunjwa moyo kwa wapenzi wa Chama hicho, kutokana na vyombo vya habari kutoa matumaini makubwa sana kuliko hali halisi. Kwa maana hiyo pamoja na kazi nzuri ya Mh Slaa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa Wabunge na kujulikana kwa chama, wapenzi wao hawatayaona hayo kama ni maendeleo au ushindi bali ni kinyume chake. Hii ni hatari sana kwa chama maarufu cha upinzani kujihakikishia uhai wake baada ya uchaguzi.
Ushauri wangu kwa vyombo vyote vya habari vinavyoiunga mkono CHADEMA kutopika takwimu na badala yake kuandika hali halisi. Kwa mfano hakuna hata siku moja vyombo hivyo vya habari vimeeleza kinaga naga ni maeneo gani Mh Slaa hana umaarufu kabisa.
Chaguo ni lenu kujenga chama au kubomoa.