Mh rais usihutubie kabla ya kusoma hapa

Mh rais usihutubie kabla ya kusoma hapa

Mwananzengoo

Member
Joined
Jun 8, 2014
Posts
56
Reaction score
25
Hizi kauli za watuhumiwa wa escrow, Mhe. Kikwete unajitenga vipi nazo ?

Najaribu sana kuilazimisha akili yangu izione kauli za waheshimiwa watuhumiwa wa uchotaji wa fedha za akaunti ya Tegeta escrow kuwa za kawaida, lakini inashindikana. Hapa zimesemwa kauli nyingi ambazo zinaonyesha kujiamini kunakovuka mipaka kwa watuhumiwa wa escrow. Majibu haya ya kujiamini yameanza tangu kuibuliwa kwa kashifa hii nzito inayotia doa kubwa utawala wa awamu ya nne nje na ndani ya nchi.

Majibu ya AG bungeni yalionyesha kujiamini kana kwamba Kuna mtu mkubwa anahusika na hiyo issue. Hiyo ilisindikizwa na mbunge mmoja kuitwa tumbili. Nasikia kuwa Mhe Rais wakati akijibu ombi la kujiuzulu alimpongeza na kutambua uadililifu wake.

Mhe. waziri Tibaijuka naye katoa kauli inayomtaka rais ajitenge nayo, pale aliposema kuwa akijiuzulu rais atamshangaa. Hii inaonyesha boss anafahamu madudu haya. Kujiamini kwa mama huyu kunaacha maswali mengi zaidi ya majibu.

Watanzania wameshangazwa na waziri Tibaijuka kuandaa mkutano wa waandishi wa habari kwa hela ya serikali ili kuzungumzia tuhuma zake binafsi. Wadau hawakubaliani na hoja kwamba tuhuma hizi ni za mtu binafsi. Nyerere alipata kusema kuwa, " Watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM."
 
unajua sana kupiga gitaa, kwa bahati mbaya unampigia mbuzi! hela alizogawa rugemalila sio zake, ni mgao wa hisa za watu waliokuwa nyuma ya mgongo wake, na ndio kwa hivo hivo kwa miradi mingi humu nchini, richmond, downs melemeta etc etc, wanaotambulika ni wasimamizi tu, wenye mali ni vigogo wa nchi, ndio maana wanaojua wakawambia walipie kodi hela walizopewa.
 
kamwamu ninakupa big up kwa coment iliyosimama. Hawa akina Rugemalila ni picha tu inayowekwa mbele, nyuma yake kuna vigogo wengi sana. Mm hii issue ya Prof Tibaijuka na wenzake kugawiwa hela nyingi hizo kama karanga haiingii akilini. Watakuwa wana HISA wakubwa wa IPTL.
 
Last edited by a moderator:
Comments nzuri Sana. Hii inaonyesha waTZ wanauelewa wa kutosha mh asikurupuke na hotuba za enzi za uhuru.
 
Mwananzengoo

Ndugu,hawa wameshatuona mabwege sana, hivi mtu huyu hata kama yuko safi kiasi gani lakini kuna jambo la kutueleza hapa,mimi naomba anieleze haya mawili tuu, la kwanza hivi hapa Tanzania kuna benki yoyote mtu unaweza kwenda uka droo BILIONI MOJA NA MILIONI MIA SITA kwa siku moja??? benki gani,kama milioni kumi tuu huwa naambiwa lazima ipitie benki kuu jee huyu inakuwaje??? moja kwa moja inatia shaka kama transaction hii ilikuwa halali.
la pili hebu tujiulize hivi benki tajwa hapo ina huo mtaji kwamba mteja mmoja anaweza aka droo hela ndefu hivyo na bado benki ikasimama isitetereke?? mtaji wao ukoje wana kiasi gani hawa , kama sio hii hela ililetwa tuu ikapitia hapo???

nikijibiwa hayo naweza kuwa na maswali mengine mawili ya nyongeza.
 
Last edited by a moderator:
Bila kupepesa macho mkulu ni victim namba moja pamoja na familia yake. Halikwepi hili kwa namna yoyote. Hii ni kutokana na media mbalimbali kuandika juu ya mkwewe, mnikulu, jaji rwehumbiza anakofanyia kazi ritzone, katibu wake na watendaji wakuu wa serikali kupata mgao. Ushahidi mwingine ni pale TISS ilipozimia wakati mabilioni yakitolewa benki tena kwa cash na sio hundi. Wahusika hawa mungu aliwachepusha njia kuu waliyokuwa wamepanga kupita na waktoa cash. Na hapo ndipo tuliposikia juu ya uhamishaji wa fedha kwa magunia. Hii ni aibu mbaya kwa taifa mbele za mataifa.
Kwanini atokomoe?. Tulimkosea nini hadi atuibie pesa zetu?. Lakini kwetu yamekuwa mazoea sasa, eti kila rais anayeondoka anajichotea fedha zetu benki kuu na kuwaachia wa chini yake nao kujichotea na kuiacha nchi bila fedha. Haivumiliki na haikubaliki hata kidogo. Na kama vipi naye aachie ofisi ili achunguzwe na kushtakiwa.
Kutokana uhusika wake ndio maana anashindwa kuchukua hatua. Achukue tu hata kama zitamsabaratisha na ccm yake.
 
Lowassa hakusubiri masaa 48 ili awajibike, je hawa wa iptl ni wapi wanapata nguvu na courage ya kusurvive mpaka leo?


Mungu nipe uhai nishuhudie anguko rasmi la CCM mwakani.

japo mimi si mwana chadema, nathubutu kusema PEOPLE'S POWER!
 
angefanya kama alivyofanya obama jana wa tz wanamaswali mengi yanayoitaji majibu ya papo kwa papo
 
Watanzania wengi sasa hivi wanaakili ya kujua kila kinachofanyika hapa nchini hii ishu Jk anaijua fika na yeye ni muhusika pia ndio maana anashindwa kutoa maamuzi lakini mwisho unawafikia hakuna pa kutokea mtaniambia
 
Kwa haya yanayoendelea, ikulu SI mahali patakatifu any more...

wasihusike kwa kigezo gani?. Wao si ndio waliokuwa wanazihifadhi?. Nduru na wale watoto wa vigogo wanaofanyakazi hapo BoT must find their way out. Yes waje uraiani tuwahukumu kama vibaka. I swear, I will be the first to throw stones on them. Nyambafu zao.
 
Lowassa hakusubiri masaa 48 ili awajibike, je hawa wa iptl ni wapi wanapata nguvu na courage ya kusurvive mpaka leo?


Mungu nipe uhai nishuhudie anguko rasmi la CCM mwakani.

japo mimi si mwana chadema, nathubutu kusema PEOPLE'S POWER!

wakati akijiuzulu lowasa ufisadi ulikuwa haujaota mizizi lakini hivi sasa ufisadi ni sehemu ya majukumu ya watawala wengi serikalini
 
Back
Top Bottom