Nishituke nini? Sina cha kushituka coz' kama kushituka, nishashtuka sana nakushangaa wewe unaeshituka leo!!! By the way, nami sina shaka kwamba kilimo chetu hakiwezi kukuzwa na wageni lakini nitakuwa mwehu nikiukana ukweli kwamba hata sisi wenyewe tumeshindwa kukikuza! Ninaposema sisi wenyewe, simaanishi serikali; bali mimi na wewe! Kiasi cha miaka miwili iliyopita nilileta mada hapa JF, kwamba hivi kweli Tanzania tuna ardhi ya kutosha au hatuna akili za kutosha!!?? Nikawaomba wana-JF kila mmoja anitajie ana ekari ngapi za ardhi alizozipata yeye mwenyewe(yaani sio mashamba ya kurithi) kwa juhudi zake!! Niliuliza hivyo huku nikiamini kwamba kupata ardhi Tanzania hakuhitaji mtu kuwa tajiri!!! Na concern yangu hapa ilikuwa kwamba, angalau kila Mtanzania angekuwa na ekari mbili za ardhi, basi suala la kwamba tuna ardhi ya kutosha lisingekuwepo lakini linakuwepo kwavile naamini hatuna akili za kutosha za kuitumia ardhi iliyopo!! Ndugu yangu, wewe una ardhi ekari ngapi?!Viwanda hakunasiyeliona hilo na mabenki pia baadhi,hata elimu pia,tumegwaya kuanzisha mijadala shirikisho la afrika mashariki ni hatari kwa ardhi yetu,shukrani S.Sita. hoja ilikuwa wakenya na wengineo wanataka ardhi yetu watanzania tuwe makini,leo Mh Rais unawaambia wageni kabisa wawekeze kwenye kilimo! mtanzania kashindwa,kilimo kwanza hewa! serikali inafeli na itaendelea kufeli kwa muenendo huu,cha kushangaza hustuki!
wewe umesema ugal wa yanga tulikula kwa sababu ya vita nikakuhoj mbona waganda hawakula huo ugali wakat wao ndo waliathirika zaid sasa unabadili maneno unasema tulikuwa tangia uhuru? Tuyamalize Wewe amini ujamaa ndo suluhu mie niamini kivingine!
ni kweli Mh JK amenishtua. leo amewakaribisha wa Turkish kuwekeza nchini kwenye sekta mbalimbali ikiwamo kilimo! yani kwa miaka zaidi ya 50 ya kuwa huru na kujitawala,leo tunamkaribisha bepari aje kuwekeza kwenye kilimo! ilitakiwa tuwaambie tuna hotculture products bora,pamba bora kahawa bora,korosho bora,ngano bora katani bora,ndizi bora tunahitaji soko wafungue milango. wawekeze kwenye kilimo!?!wasaidie kilimo kwanza au!? kilimo kwanza kimeshindwa hadi mnakaribisha mabepari kuwekeza kwenye kilimo! shame on us, shame to the government. Sikubaliani hata chembe na Mh JK hata chembe katika hili,totally sounds like a fail government
Mkuu huu utandawazi tunaingia kichwa kichwa,uwekezaji wa kibepari kwenye ardhi ya kijamaa,ungeongea kuvunjwa vyama vya ushira ambao ni mfumo wa kijamaa ningekuelewa,Mwalimu nae alikosea sio kila kauli yake ni sahii.wachina ndani ya ujamaa ndo umewafikisha walipo,baada ya ugali wa yanga vilimwa hadi viwanja vya mpira,na hakika hali ile hakurudia tena,sku hizi blah blah tu mkuu
Kizotaka,
Wanasema safiri uyaone. Kabla ya kusafiri kwenye nchi za watu hata mimi nilikuwa na maoni kama ya Songoro. Nimekwenda Costa Rica na pia Guatemala. Guatemala ndiyo iliyonifungua macho. Kule kuna mashamba makubwa makubwa ya ndizi yanamilikiwa na makampuni ya Wamarekani. Kule pia kuna a landless people. Wenyewe wanaitwa "campesino." Au Campers kwa kiingereza. Hawa wanakodishwa na haya mashamba makubwa ya kibiashara na wanalipwa minimum wage. Lakini they are a landless people. They are poor. Sasa ukifikiria kuwa hapa Marekani kuanzia New York hadi California kila super market wanauza ndizi, ungedhani kuwa hawa wakulima wa ndizi ni matajiri sana. Vivyo hivyo kampuni za nanasi Costa Rica. Hizi ni za wawekezaji wa Kimarekani. The people of Costa Rica do not benefit mutually from their pineapples
that we buy in the super markets here in the US. Sasa nasema, kama hicho ndicho kilimo CCM wanataka kutuletea Tanzania afadhali tubaki na our unused land for years to come kuliko siku moja tuamke tukute Watanzania wamekuwa ma campesinos katika nchi yao na ardhi imechukuliwa na Wamarekani na Waturuki eti kwa sababu tunashabikia uwekezaji.
ni kweli Mh JK amenishtua. leo amewakaribisha wa Turkish kuwekeza nchini kwenye sekta mbalimbali ikiwamo kilimo! yani kwa miaka zaidi ya 50 ya kuwa huru na kujitawala,leo tunamkaribisha bepari aje kuwekeza kwenye kilimo! ilitakiwa tuwaambie tuna hotculture products bora,pamba bora kahawa bora,korosho bora,ngano bora katani bora,ndizi bora tunahitaji soko wafungue milango. wawekeze kwenye kilimo!?!wasaidie kilimo kwanza au!? kilimo kwanza kimeshindwa hadi mnakaribisha mabepari kuwekeza kwenye kilimo! shame on us, shame to the government. Sikubaliani hata chembe na Mh JK hata chembe katika hili,totally sounds like a fail government
Taasisi za nje au mataifa ya nje yanayotaka kuweza katika kilimo nchini yatatakiwa kufanya hivyo kwa kuingia mikataba na vijiji na maeneo husika ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaoishi katika maeneo husika wanafaidika na uwekezaji mkubwa wa kilimo.
Tatizo Watanzania wanataka wawe wajamaa wakati ujamaa umewashinda, hapo hapo wanataka pia wawe wabepari wakati misingi ya ubepari hawaitaki. Siasa za ki-propaganda zimewafanya wanasiasa hata kutokuwa na mwelekeo halisi. Wanashindwa kuachana na misingi ya kijamaa kwa sababu tu ya kuogopa kufuta legacy ya kisiasa iliyoachwa na Mwl. Nyerere.
Ukizisoma ilani za uchaguzi za vyama vikuu nchini kuhusiana na kilimo. Vyote vimeacha grey area kuhusiana na specifics kuhusiana na mabadiliko katika sekita ya kilimo.
angalia hiki kipengele cha ilani ya Uchaguzi ya CHADEMA, kujua mashimo ya mwelekeo wake kuhusiana na kilimo.
Hiki ndicho tunachokiongelea hapa ambacho watu wanadai Rais Kikwete amewashitua.
Jasusi , Tatizo langu ni vyama kutokuwa specific katika maelezo yao. Ninavyofahamu, chini ya mpango wa CCM, kijiji kinarusiwa kuuza au kugawa ardhi ya ekali 100 mpaka 500 bila idhini ya serikali kuu (stand to be corrected). Lakini ukiangalia hapa tunaongelea mwekezaji wa maelfu ya ekali ambapo mwenye jicho katika maamuzi ni serikali kuu.Ngwa'namapalala,
Afadhali huo msimamo wa Chadema mara kumi na hiki anachofanya Kikwete. Chadema imezingatia kushirikishwa kwa wakazi wa vijijini, Kikwete anasema wakazi wa vijijini ni watu wa pembezoni ambako kufaidika kwao kutakuwa kama vile mbwa anapotupiwa mfupa pale bwana mkubwa anakula uhondo mezani. Tena siyo hivyo tu, kwa sera za Kikwete, akija " mwekezaji" mkazi anafukuzwa wangu wangu kumpisha mkombozi ardhini. Kama anavyosema Kibanga anampinga Mkoloni, tunakaribisha vita kwa sera hizi potofu za CCM.
Hapo tupo pamoja ndugu yangu. Ukiangalia yanayotokea Loliondo, Mbarali na Kisarawe, ambako mwekezaji alipewa mamia ya eka na wakazi kulazimika kuhama unajiuliza ni sera gani hizi? Kuna jamaa pale Kisarawe alikuwa anajipatia dola 150 kwa mwezi akiuza mkaa. Lakini eneo lake akapewa mwekezaji ambaye alimwajiri kwa mshahara wa dola 75 kwa mwezi. Sasa huyu jamaa badala ya kupiga hatua amerudi nyuma na mwekezaji wa jathropa wala hatamshirikisha kwenye faida yake. Huu ni uwekezaji ambao hautuletei manufaa kabisa.Jasusi , Tatizo langu ni vyama kutokuwa specific katika maelezo yao. Ninavyofahamu, chini ya mpango wa CCM, kijiji kinarusiwa kuuza au kugawa ardhi ya ekali 100 mpaka 500 bila idhini ya serikali kuu (stand to be corrected). Lakini ukiangalia hapa tunaongelea mwekezaji wa maelfu ya ekali ambapo mwenye jicho katika maamuzi ni serikali kuu.
Tuna choice mbili, either tuwe kama wajamaa au tufuate uwekezaji wa kipepari ambao misingi yake ni wachache kuwa super rich regardless kwa serikali kuwa na tight land law.
Ninakubaliana na wewe, Viongozi wetu wasipokuwa makini na swala la ardhi, tunaweza tukajikuta tuko kama Kenya lakini vile vile utakuwa ni ujinga kuogopa kufanya maamuzi ambayo yataonekana ni mabaya kisiasa.
Mkuu kitu kimoja ambacho ninakiona pia nchini ni kuwa na watanzania ambao hawana ujuzi na pia siyo wabunifu. Kwangu mimi huwa nasema kila siku, siasa za Mwl.Nyerere zimeilemaza jamii sana. Jamii haikuwekwa kwenye tanuru la mashindano ya soko huria kijamii, kisiasa na kiuchumi matokeo yake mdiyo haya. Tumekuja kuingia kwenye soko huria nila maandalizi ukichukulia kuwa, tulikuwa ndani ya uchumi wa kijamaa kwa karibia miaka 30. Ndiyo maana hata kilimo kwanza hakikufanikiwa.Hapo tupo pamoja ndugu yangu. Ukiangalia yanayotokea Loliondo, Mbarali na Kisarawe, ambako mwekezaji alipewa mamia ya eka na wakazi kulazimika kuhama unajiuliza ni sera gani hizi? Kuna jamaa pale Kisarawe alikuwa anajipatia dola 150 kwa mwezi akiuza mkaa. Lakini eneo lake akapewa mwekezaji ambaye alimwajiri kwa mshahara wa dola 75 kwa mwezi. Sasa huyu jamaa badala ya kupiga hatua amerudi nyuma na mwekezaji wa jathropa wala hatamshirikisha kwenye faida yake. Huu ni uwekezaji ambao hautuletei manufaa kabisa.
hoja yako ni nzuri ila umepoteza ladha kwa sababu hawa wawekezaji wako kutoka sehemu mbalimbali za dunia ila umeona kwa waturkish tu? sikubaliani na JK ila pia sikubaliani na intention behind you.
Watanzania ni watu wa kulialia tu muda wote. Sasa kama wewe uliyetakiwa uje kuwa mwekezaji ndiyo umeamua kuwa mchumia tumbo wa CHADEMA, unaanzisha thread zako za kiPropaganda, ulitaka serikali ifanyeje?
Ngwa'namapalala,
Afadhali huo msimamo wa Chadema mara kumi na hiki anachofanya Kikwete. Chadema imezingatia kushirikishwa kwa wakazi wa vijijini, Kikwete anasema wakazi wa vijijini ni watu wa pembezoni ambako kufaidika kwao kutakuwa kama vile mbwa anapotupiwa mfupa pale bwana mkubwa anakula uhondo mezani. Tena siyo hivyo tu, kwa sera za Kikwete, akija " mwekezaji" mkazi anafukuzwa wangu wangu kumpisha mkombozi ardhini. Kama anavyosema Kibanga anampinga Mkoloni, tunakaribisha vita kwa sera hizi potofu za CCM.
Mwl Nyerere baada ya kulihutubia bunge huru la South Afrika alihijiwa na Waandish wa habari akaulizwa ni jambo gani anadhan alikosea katika utawala wake nae alisema alichokosea ni kuamini kuwa mfumo wa Ujamaa ungeweza kustawisha Kilimo, chini ya kilimo cha mfumo wa kijamaa ilifikia hatua tukala unga wa Yanga toka kwa mabepari wa kimarekani, hata wachina wameachana na kilimo cha kijamaa, Ubepari na soko huria ndo mpango mzima, Tembeleeni botswana muone kilimi kilivyostawi!