Hakuna kiongozi yeyote makini atakayetoa hela ya serikali kwenda kufanya gambling ya madini. Ili uweze kuchimba madini inatakiwa uanze na utafiti. Global average ya discoveries, katika kila vitalu 70,000 vya utafiti wa madini ya dhahabu, ni 7 tu ndiyo huwa na dhahabu ya kuweza kuchimbwa kwa faida.
Hapa Tanzania usione hiyo migodi michache ya dhahabu, kampuni nyingi zimepoteza fedha katika utafiti, na zimeondoka zikiambulia patupu. Usisikie habari za vijiweni eti nchi yetu kila mahali ina madini, labda kama tunahesabia na mawe ya kujengea.
Kampuni kama Barrick walikuwa na bajeti ya $20m+ kila mwaka, na wamefanya utafiti kwa zaidi ya miaka 10. Hiyo ni zaidi ya dola milioni 200, wakabahatika kupata project moja tu inayoweza kuwa mgodi. Mingine yote (Bulyanhulu, Tulawaka, Buzwagi na Nyamongo) walinunua toka kwa makampuni mengine.
Je, serikali ipo tayari kutumia zaidi ya dola milioni 200, na zikipotea kusiwe na neno? Kampuni ya mafuta ya Brazil ilitumia dola milioni 760 kufanya utafiti wa mafuta Tanzania, hawakupata kitu wakaondoka. Serikali ipo tayari kutumia dola milioni 760, tukose, halafu tuone kuwa ni kawaida tu?