Mh. Rais Magufuli; Iongezee uwezo STAMIGOLD

Barrick zamani Acacia kuna dogo mmoja namjua wa undeground mining alipelekwa Australia miaka 3 alikuwa junior geologist, Acha Sierra Leone, Mid level managers wengi walipelekwa Capetown University kufanya Management Courses.

Huwezi kupanda mbigiri ukavuna mchicha hata siku moja. Training an Development ndio ina add value to production

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu, nafikiri ifike hatua sasa watanzania na sisi tuone umuhimu wa training and development kwenye maeneo ya kazi kama nguzo muhimu ya kupata matokeo bora ya kazi.

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Hiyo sasa ni kazi ya labour officers, Ministry, Sijawahi kusikia kampuni ya Mhindi,Mchina anapeleka mfanyakazi kuongeza ujuzi.

Mfano kuna position kama Mine Shift boss, Mine Captain, rigger, expeditor hata uwe na phd bila field training huwezi kuperform. Na hao wa Acacia wengi ndio wanaajiriwa Congo,Zambia,Sierra Leone, UAE, Australi, Namibia, SA sababu kubwa ni Training & Dev waliyopewa na kampuni.

Wala sidhani kama ni kazi ya labour officers, nafikiri ni suala la vipaumbele tu vya taasisi na taasisi au kampuni na kampuni.

usitembee juu ya ardhi kwa majivuno
 
Inaitwa wishful thinking.Kutamani Stamigold au Kampuni yoyote ya Umma ifanye vizuri mithili ya Kampuni zilizokomaa kiutendaji wa Kibepari,ni ndoto!!
Game ya Capitalism Ina Kanuni zake, tunahitaji miaka kujifunza inavyooperate,hatuwezi kufanikiwa Kwa kubypass hizi process.Tuna tabia ya Uchawi, Kuanzia Viongozi hadi Wananchi WA kawaida.Tuwaulize Wachina walifaulu toka Communism hadi mapinduzi yao ya Viwanda na technology tunayoyaona.Kwa Ufupi,unacholipa Stamigold siyo pesa,ni AKILI ambazo ziko disciplined kufanya Kazi Kibepari,zikiwa hazina fikra za Kijamaa!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuwa nikiwaza kwa muda sasa tokea sakata la Makinikia ya ACACIA na Barrick Gold.

Nimewaza ikiwa Makampuni haya yalikuwa na yamekuwa yakitengeneza faida kubwa kiasi ambacho tumeelezwa na yangeweza kulipa kodi ya Matrilioni tuliyoelezwa na bado makampuni hayo yakabaki na faida nzuri baada ya kutoa gharama zauendeshaji, basi Tanzania tuna dhahabu yenye thamani kubwa sana.

Kwa mantiki hiyo, namshauri Rais Magufuli; akiona inafaa, aijenge uwezo wa hali ya juu kampuni ya kizalendo ya STAMIGOLD kwenye eneo la mtaji, vifaa mitambo na rasilimali watu.

Hii itasaidia kwa maana kwamba, faida hiyo kubwa, na ile ambayo ingelipwa kama kodi na ajira za kutosha vyote vitabaki hapa hapa nchini kwa maendeleo ya Watanzania.

Naomba kuwasilisha hoja.

Huu ndiyo uzezeta kamili naozungumziaga pale naposema siyo kazi ya serikali kufanya biashara. Biashara ya migodi ina namna yake ya financing ambayo ni mikopo mikubwa ya benki na amana za wanahisa. Nikisema mikopo mikubwa namaanisha mikopo mikubwa kiasi ambacho mabenki yetu ya nchini hayawezi kutoa hata yakijipanga kama consortium. Kwa mfano, uwekezaji wa barrick tz ni usd billion 4, karibu sawa na makusanyo yote ya tra kwa mwaka mmoja.

Mabenki haya yanatoa mikopo kwa makampuni yenye kujulikana uwezo wao, km acacia, barrick, anglo, newmont, rio tinto etc. Wewe hata ukiwa umegundua reserve kubwa kiasi gani, kama hauna reputation, hawatakukopa, na ndiyo maana tunawaambia kila mara kuwa makampuni ya uchimbaji mkubwa yapo machache duniani kuliko makampuninya uundaji magari.

Sasa wewe nenda kama stamico kaombe mkopo ukisema umetaifisha migodi ya barrick, uka fumble fumble kuyaendesha na yamekushinda na eti sasa unaomba mkopo ujiongeze uwezo, halafu tuone kama watakupa senti tano
 
Nafikiri ungejaribu kwanza kufanya uchunguzi kule Tulawaka ambapo kampuni yetu mama ya stamigold inachimba dhahabu, hapo ndio ungepata picha kamili kama tunaweza au hatuwezi..

Tukiweza kutenganisha siasa na serikali, siasa na utendaji, siasa na utalaamu tutafanikiwa lakini tofauti na hapo hakuna tutakachofanikiwa..

Umelenga kwenye tatizo. Maamuzi ya kisiasa hayaangalii gharama, ufanisi wala faida.
Mara zote wanasiasa huzingatia kuimarisha madaraka yao kwa njia zozote, ziwe haramu au halali na bila weledi. Hiyo ndiyo sababu ya mashirika mengi ya uma kufa.
Wanasiasa walio wengi ni wapuuzi fulani tu wanaopewa heshima kubwa kwa sababu ya ujinga wa wananchi.
Ill miradi ya uma ifanikiwe ni muhimu kuondoa usimamizi wa moja kwa moja we wanasiasa.
 
Ni kweli mkuu, hizi dialogue zinatakiwa zifanyike na watawala wajue hata sisi wananchi tunajua wapi kwenye tatizo.

Lakini pia ni lazima tujue wanasiasa wetu wanapambana ili hayo mambo yasitenganishwe na siasa, maana yatakapotenganishwa na siasa watakosa kwakula, mfano suala la IPTL ambalo kwa 90% lilitakiwa lihusishe wataalamu matokeo yake wanasiasa wakaingia kati na wote ni mashaidi namna mgao ulivyotembea kwa wanasiasa.

Tufanyeje sisi wananchi wenye uchungu ili haya mambo ya kitaalamu na maendeleo yarudi kwa wataalamu na wanasiasa wabaki kwenye siasa zao?, ukumbuke pia wanasiasa ndio wameshikiria mpini na hawataki kuuachia na kama ujuavyo wataalamu wengi tayari wanaweza kuishi kutokana na utaalamu wao hivyo hawajihusishi kabisa na siasa yenye unafiki na ujinga mwingi.. Tunafanyeje kubadiri mfumo huu?
 
Kuna jamaa yangu anafanya kazi kule anasema wamefunga kule Tulawaka kwa wiki mbili na sababu ni kupungukiwa mafuta na gharama za uendeshaji kwa ujumla,ni kweli kuna umuhimu wa kupeleka nguvu kubwa kwenye cha kwetu na kua na usimamizi wa hali ya juu.hata hii migodi mingine tunapaswa tuchimbe wenyewe na mzungu awepo tu kama mfanyakazi na mkodisha mitambo tumlipe kulingana na tutakachopata.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA

ukweli ni kwamba Tulawaka inashindwa kurun kwasababu ya siasa, Huwezi kurun mgodi kwa kutegemea hela zitoke wizarani au nani sijui huko wizarani aizinishe fungu wewe ndio ununue kipuri/spea na uendeshe shughuli za kila siku. Kwenye Mamlaka na mgodi ni General manager wa mgodi husika na timu yake, wao hupanga bajeti kulingana na operation zao na mwisho wa siku hupewa fungu kwa daily operation na contractor wote wakubwa hulipwa kupitia system kwa wakati husika na sio blah blah tulizozoea za kulipa supplier na contractor kupitia halmashauri na wizara zetu.

Migodi yote duniani inaendeshwa kwa mfumo wa outsource kwa maana ya kufanya kazi na contractors tofauti tofauti ili kusustain operation za mgodi, kuanzia drilling, haulage, blasting,catering service,huku kote unahitaji supplier na contractors tofauti tofauti. Contractor wengi utakaowapata huku ni international contractors and international mining suppliers ambao hawaishi kwa longolongo tulizozizoea, wakiona unasumbua kwenye malipo wanaachana na wewe na wakikutana kwenye mining indaba huko au bauma huwa wanaambiana mwisho wa siku hakuna atakayefanya kazi na wewe na hapo lazima uanguke.

Siasa na uswahili kwenye mambo ya kitaalamu ni hasara kubwa kwenye Taifa letu na moja ya changamoto kwenye ukuaji wa uchumi wetu..
 
Mkuu kwa kiasi kikubwa uko sahihi lakini ili hayo yawezekene, inahitajika utashi wa kisiasa na kuwekeza mtaji mkubwa. Nakubaliana nawe mkuu, na yote haya yanaweza kufanyika tukiamua na viongozi wetu wakiwa na mtizamo wa namna hiyo.

Mkuu unafikiri ni lini hawa viongozi wetu watakuwa na mtizamo wa namna hiyo?
Maana pia tulishindwa kuendesha viwanda mpaka vikafa kwa sababu hizi hizi za kisiasa, na leo tunajaribu kuvirejesha je tumebadirika au tunaenda kuweka mitaji mikubwa halafu ije ipotee kizembe na tuanze kushikana mashati tena?
 
Kuna kitu kinaitwa Mining Indaba, na Bauma mara nyingi haya ni maonyesho muhimu ya masuala ya migodi duniani, Mining Contractors na Mining Companies na wadau wengi wa migodi hukutana huko mara kwa mara kujionea na kubadirishana uzoefu wa masuala tofauti tofauti ya Migodi na kuangalia fursa tofauti tofauti kuanzia operations,management ya migodi, na exploration.

Ni vizuri pia kama tuko serious tuwe tunahudhuria haya maonyesho ili kujionea na kujifunza juu ya hivi vitu, Kuendesha Mgodi au Migodi in large scale and modern technology sio kitu cha kufikirika bali ni kitu kinachohitaji akili,uzoefu na utashi wa kazi. Mining ni biashara sio siasa, Viwanda ni biashara sio siasa pia, Siasa ibaki kuwa siasa na utaalamu au technology ibake kuwa ilivyo tusichanganye, na tukishindwa kuchora huo mstari basi tutaendelea kupoteza muda tu..
 
ukweli ni kwamba Tulawaka inashindwa kurun kwasababu ya siasa, Huwezi kurun mgodi kwa kutegemea hela zitoke wizarani au nani sijui huko wizarani aizinishe fungu wewe ndio ununue kipuri/spea na uendeshe shughuli za kila siku. Kwenye Mamlaka na mgodi ni General manager wa mgodi husika na timu yake, wao hupanga bajeti kulingana na operation zao na mwisho wa siku hupewa fungu kwa daily operation na contractor wote wakubwa hulipwa kupitia system kwa wakati husika na sio blah blah tulizozoea za kulipa supplier na contractor kupitia halmashauri na wizara zetu.

Migodi yote duniani inaendeshwa kwa mfumo wa outsource kwa maana ya kufanya kazi na contractors tofauti tofauti ili kusustain operation za mgodi, kuanzia drilling, haulage, blasting,catering service,huku kote unahitaji supplier na contractors tofauti tofauti. Contractor wengi utakaowapata huku ni international contractors and international mining suppliers ambao hawaishi kwa longolongo tulizozizoea, wakiona unasumbua kwenye malipo wanaachana na wewe na wakikutana kwenye mining indaba huko au bauma huwa wanaambiana mwisho wa siku hakuna atakayefanya kazi na wewe na hapo lazima uanguke.

Siasa na uswahili kwenye mambo ya kitaalamu ni hasara kubwa kwenye Taifa letu na moja ya changamoto kwenye ukuaji wa uchumi wetu..

Safi. Siyo tu uswahili ni hasara, bali unaweza kusababisha vifo migodini.
 
Nafikiri ungejaribu kwanza kufanya uchunguzi kule Tulawaka ambapo kampuni yetu mama ya stamigold inachimba dhahabu, hapo ndio ungepata picha kamili kama tunaweza au hatuwezi..

Tukiweza kutenganisha siasa na serikali, siasa na utendaji, siasa na utalaamu tutafanikiwa lakini tofauti na hapo hakuna tutakachofanikiwa..
Naunga mkono hoja mkuu....
Mfano mzuri ni Mgodi wa Tulawaka ulioachwa chini ya Meneja mkuu na viongozi wengine wakiwa ni watanzania...... Mgodi huo umekua na matumizi mabovu ya fedha pamoja na wizi wa dhahabu ambayo imekua ikizalishwa.
 
Kuna jamaa yangu anafanya kazi kule anasema wamefunga kule Tulawaka kwa wiki mbili na sababu ni kupungukiwa mafuta na gharama za uendeshaji kwa ujumla,ni kweli kuna umuhimu wa kupeleka nguvu kubwa kwenye cha kwetu na kua na usimamizi wa hali ya juu.hata hii migodi mingine tunapaswa tuchimbe wenyewe na mzungu awepo tu kama mfanyakazi na mkodisha mitambo tumlipe kulingana na tutakachopata.

JAH RASTAFARI MORNING AFRICA
Mkuu......
Uliwahi kumuuliza huyo jamaa yako sababu ya kukosa Diesel ya Generators na gharama za uendeshaji ilhali mgodi unazalisha?
Ebu pata majibu kwanza hapo na kisha ndipo uzungumzie kuhusu serikali kuwekeza fedha kwenye migodi
 
Barrick zamani Acacia kuna dogo mmoja namjua wa undeground mining alipelekwa Australia miaka 3 alikuwa junior geologist, Acha Sierra Leone, Mid level managers wengi walipelekwa Capetown University kufanya Management Courses.

Huwezi kupanda mbigiri ukavuna mchicha hata siku moja. Training an Development ndio ina add value to production

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo dogo leo hii ndie Meneja mkuu kwenye mgodi wa Shanta uliopo Chunya Mbeya.
Na mgodi unafanya na kuzalisha vizuri chini ya huyo dogo.
 
Hiyo sasa ni kazi ya labour officers, Ministry, Sijawahi kusikia kampuni ya Mhindi,Mchina anapeleka mfanyakazi kuongeza ujuzi.

Mfano kuna position kama Mine Shift boss, Mine Captain, rigger, expeditor hata uwe na phd bila field training huwezi kuperform. Na hao wa Acacia wengi ndio wanaajiriwa Congo,Zambia,Sierra Leone, UAE, Australi, Namibia, SA sababu kubwa ni Training & Dev waliyopewa na kampuni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu....
Umegusa mule mule wallah....
 
Mkuu......
Uliwahi kumuuliza huyo jamaa yako sababu ya kukosa Diesel ya Generators na gharama za uendeshaji ilhali mgodi unazalisha?
Ebu pata majibu kwanza hapo na kisha ndipo uzungumzie kuhusu serikali kuwekeza fedha kwenye migodi
Mafuta ya kuendeshea mitambo huisha na kupelekea kampuni zilizokodiwa na mgodi mama kushindwa kujiendesha.na sababu ni kutokulipwa kwa wakati gharama zao ili waweze kuendesha shughuli.now kuna watu wako nje hawaingii mgodini na wanadai miahahara ya miezi kadhaa.ktk mgodi huo ninao rafiki zangu wa karibu wa miaka yote wawili.na hivi naandika hapa mmoja wapo ninae hapa
 
Tusidanganyane kitu kikishaitwa cha umma ni hovyo tu. ata angewapatia mtaji kiasi gani hawataweza kudumu kwa muda mrefu, Mwalimu alifanya yote hayo lakini alishindwa serikali kufanya biashara sio falsafa yake duniani kote.
 
Mafuta ya kuendeshea mitambo huisha na kupelekea kampuni zilizokodiwa na mgodi mama kushindwa kujiendesha.na sababu ni kutokulipwa kwa wakati gharama zao ili waweze kuendesha shughuli.now kuna watu wako nje hawaingii mgodini na wanadai miahahara ya miezi kadhaa.ktk mgodi huo ninao rafiki zangu wa karibu wa miaka yote wawili.na hivi naandika hapa mmoja wapo ninae hapa
Mkuu nadhani haujanielewa, ebu ngoja nifafanue hoja yangu hapa.......
Wakati kampuni ya Barrick inaondoka kwenye mgodi wa Tulawaka, waliacha mashine na mitambo yote kwaajili ya uchimbaji wa dhahabu......
Wao Barrick waliweza kujiendesha kwa kutengeneza faida maradufu ambayo nakumbuka miaka ya 2009 waliwahi kuitaja Tulawaka kama Super Profit Mine........
Sasa hapa swali langu ni, kwanini mgodi unaishiwa na Diesel na hata fedha za kuwalipa subcontractors?
Kwanini mapicha picha na visingizio vimeanza baada ya Barrick kuondoka na kukabidhi mgodi kwa Stamico?
 
Sijui kama unaelewa maswali haya ungewauliza wao..nimekupa kinachoendelea mpaka sasa kulingana na kauli za staff wa humo ndani mgodini.maswali yako yana msingi lakini unapaswa ufunge safari ukawaulize maana ni undani wa kushindwa kwao kazi au kuyumba kiutendaji.hata staff wa chini ukiwauliza watakwambia uongozi ndo unajua
 
Back
Top Bottom