Mh Rais JK, unalijua hili? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh Rais JK, unalijua hili?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyami2010, Jun 13, 2011.

 1. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  WanaJF

  Sina namna ya kumshauri Rais JK, lakini kama anaipenda Tanzania na chama chake, basi afanyishe Rapid Political Appraisal kabla ya kuwateua Ma-DC na Ma-RC:-

  Ma-DC na Ma-RC: Awateue vijana wapya, wasomi, wenye uzoefu na kazi za jamii na maendeleo na wenye mvuto kwa watu. Watazame zaidi watoto wa wakulima, ninarudia watoto wa wakulima!

  Mfano: Ili CCM irudishe Jimbo la Iringa Mjini, amteue Kaka Fredo Mwakalebera kuwa ata DC katika wilaya/mkoa wa jirani, ili asicheze mbali na Iringa Mjini. Fanya hivyo kwa majimbo yote nchi nzima!

  Fanyeni Rapid Polictical Appraisal nchi nzima, ili kuwabaini vijana waliokuwa ni chaguo la wananchi, lakini kwa sababu ya ufisadi na siasa za ovyo ovyo ndani ya CCM wakanyimwa nafasi. Kwa lugha nyingine, CCM iliwakataa vijana waliokuwa chaguo la wananchi na kuwakumbatia wazee wenye fedha lakini waliopitwa na wakati. Bahati tu, vijana wengi waliotoswa kwenye kura za maoni walionelea kuwa wavumilivu na kukubali maumivu. Matekeo ya hayo yote, yalijidhirisha kwenye uchaguzi mkuu ambapo Upinzania walijiokotea viti vya Udiwani na Ubunge. Lakini pia, kura alizopata Mh. Rais, anazijua mwenyewe!

  Rapid Political Appraisal, itawabaini pia wabunge wasasa ambao kimsingi hawana mvuto, ila wako pale kwa sababu ya fedha zao na wengine ni wazee na hawatarajii kuendelea na Ubunge 2015. Mifano ni mingi sana, na wote wanjulikana. Ukiisha jua hilo, panga timu yako ya Ma-DC na Ma-RC strategically, kisha subiri 2015!

  Angalizo: Mh. Rais, kama akiendelea na sura kama za akina Lau Masha, Bi. Monica Mbega, Bi. Maria Chatanda, Mzee Mwakipesile(Mbeya), Mzee Babu(Kagera), Mzee Said(Dar), Mzee Kalembo(Tanga) na wengine wengi, niko certainly sure 2015 CCM itapigwa tu.

  Wazee wabakie ni washauri na kazi hii wanaiweza tena sana
   
 2. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  napita tu mzee,nataka nisome maoni yatakayotolewa hapa
   
 3. Vin Diesel

  Vin Diesel JF Gold Member

  #3
  Jun 13, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 8,402
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  nadhani kaka Fredo Mwakalebera ni Freddy Mwakalebela.
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  watu bwana hamjui hata wakumpa ushauri ni nani, kwa ccm mimi nasema wacha ife!
  WACHA IJIFIE TUU!
   
 5. Yakuza

  Yakuza Senior Member

  #5
  Jun 13, 2011
  Joined: May 22, 2011
  Messages: 112
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nyami

  Ushauri wako ni mzuri na una mshiko, lakini J.K utaupokea na kuufanyia kazi?

  Kwa waliokaribu na J.K, si kwamba watu hawamshauri na si kwamba hilo unalolishauri ni geni kwake, lakini uswaiba umemzidi sana na of course matendo ni "Zero":cool2:
   
 6. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wewe kama Umetumwa na Mwakalebela kumpigia debe, hapa si mahali pake.

  Kwanza kwa lipi jipya ambalo wewe unaamini Mwakalebela analoweza kulifanya Iringa! Au ni kitu gani kinachokupa kuamini kwamba Mwakalebela atafanya zaidi ya analofanya Mbunge aliyepo?

  Mimi bado namkubali Mbunge aliyepo pale Iringa Mh. Msigwa kuliko huyo Mwakalebela mtoa rushwa na Mwizi mkubwa pale TFF.

  Tafuta njia nyingine ya kumpigia kampeni na si hapa JF.
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
   
 8. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2011
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  ushauri toka kwa mwakalebela mwenyewe huyo
   
 9. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Ushauri wa kijinga
   
 10. M

  Marytina JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  ujinga tu kwa hiyo amteue Batilda kuwa RC wa arusha?
   
 11. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Mie nawasikiliza tu!
   
 12. bwegebwege

  bwegebwege JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2011
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 1,031
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kwanza nina mashaka kama hujatumwa na Mwakalebela, lakini hata kam ahujatumwa naye bado nina mashaka kama unao uelewa halisi wa RPA!! Kama hutaweza kutueleza wanajamii hapa maana halisi ya Rapid Political Appraissal utakuwa unachekesha wafu....

  Pili this country need Rapid District Appraissal, (si RPA), RDA imekuwa very successful America ya Kusini (Mexico zaidi) maana inalenga maendeleo zaidi from the areakulingania na halis ilivyo na mahitaji halisi kule...kama unahitaji shule wasiliana nami kwa lectures (with costs of course)

  Tatu unasema JK aachane na "wazee" ukiwalenga kina Lau Masha (Hivi huyu ni mzee??), Bi. Monica Mbega, Bi. Maria Chatanda, Mzee Mwakipesile(Mbeya), Mzee Babu(Kagera), Mzee Said(Dar), Mzee Kalembo(Tanga)....Swali langu ni moja, hawa ni wakuu wa mikoa, ofcourse wanasimamia sera za chama tawala na serikali lakini umefanya utafiti wa kutosha?
  Naomba utembelee Tanga na Morogoro, waulize wenyeji jinsi Kalembo alivyosaidia maendeleo ya mikoa hiyo!! Leo Tanga inanza kurudisha heshima yake, Jiji ni safi, wale wenyeji wavivu wa vijiweni sasa vijiwe vimekwisha, wizi na makosa mengine ya jinai yamepungua kwa kiasi kikubwa na je unafahamu kwamba sasa Tanga inaingia kwenye mpango wa maendeleo mkubwa zaidi kwa kujenga "Economic Zone" maeneo ya Pongwe chini ya Wakorea? Unajua kwamba sasa Tanga inajenga Bandari kubwa itakayoserve Uganda, Rwanda na Burundi??....Mzee Kalembo ni kati ya wasimamiaji wakuu wa miradi hii...
  Nawasilisha
   
 13. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  katumwa huyu oppoturnist,
   
 14. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ninakushukuru ndugu yangu *****:violin:

   
 15. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu jamaa LAU Masha bado yuko kwenye system, du Jk ni kiboko!.
   
 16. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mi nilidhani atashauri kupunguza ukubwa wa serikali kwa kuvunja vyeo vya wakuu wa mikoa na wilaya
  ambavyo vinatatanisha kwani tayari kuwa wakurugenzi wa mikoa na wilaya, na maafisa tawala wa mikoa
  na wilaya! Which is which?

  Huu nao ni aina nyingine ya ufisadi wa pesa za wananchi kuweka vyeo visivyokuwa na tija vyenye
  ajenda ya kuwafurahisha marafiki na jamaa zao tu. Tunahitaji viongozi wa kuchaguliwa na wananchi
  wenyewe kuongoza mikoa na wilaya na si wateule wa rais wanaomtumikia rais na si wananchi.

  This is bull shit!
   
 17. only83

  only83 JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Pole mkuu..aliyekwambia JK uwa anasikiliza maoni ya watu nani? may be wewe utakuwa wa kwanza. Huyu jamaa anahitaji tution kabisa,sio semina elekezi pekee.......
   
 18. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Kuongoza TFF siyo Wilaya !! Kama basi ndivyo maendeleo ya TFF yako wapi? Maendeleo ya soka Tanzania yako wapi? Kama unataka Rais amsaidie kupata kazi huyo kakako Fredo Mwakarebera!! basi mwambie akubali kurudi Mtibwa kuzalisha sukari.Ikipungua gharama kilo tukapata kwa bei ya Elfu basi yamkini Slaa ajaye atampa uwaziri wa Kilimo.
   
 19. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Rapid district appraisall???!!!! mhhhh unataka kuleta theory za darasani kwenye real life management.

  Wengi wanashindwa sababu hiyo hiyo wanadhani vyeti tu na nadharia sahihi ndo vitaleta mabadiliko.
   
 20. makeyzan

  makeyzan Senior Member

  #20
  Jun 13, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nilivyosoma katika vitabu vya nyuma, nilivyosikia matangazo katika redio na runinga nimegundua yafuatayo katika safu ya viongozi wa nchi yetu.

  1. Mwalimu nyerere.
  kwa mawazo yangu huyu mtu alikuwa sana anapenda utaifa kwa sababu aliikomboa nchi kutoka kwa wakoloni, alichukua mali zilizokuwa zinashikiliwa na wakoloni na kuwa chini ya serekali yake na ndivyo hivyo aliingia kwenye siasa ya ujamaa akiamini ushilikiano wa pamoja wa serikali, wananchi na mali zao. kwa hiyo alikuwa anapenda maendeleo yake na taifa lake.

  2. Raisi mstaafu Hussein Mwinyi.
  huyu alikuwa pia anapenda maendeleo kwa wananchi wake kwa sababu aliruhusu uingizaji wa bithaa za nchi za nje kwa ajiri ya kukidhi haja za watu wake ijapokuwa ilileta matatizo lakini alikuwa na nia nzuri na watu wake.(kila kitu ruksa)

  3. Raisi mstaafu benjamini mkapa
  katika kipindi chake alikuta uchumi wa nchi ukiwa mbaya na kuanza kuupandisha. kiukweli alifanikiwa na mpaka anaondoka madarakani aliacha uchumi ukiwa 4% tofauti na sasa. alijenga madarasa akiongozwa na mmem na mesi, alijenga daraja, alijenga uwanja na mwisho alirudisha heshima ya wafanyakazi ambayo ilikuwa imeshuka kwa sababu ya kutokuwa na pesa za kujikimu wakati wafanyabiashara wakiringa mtaani.

  4. Raisi Jakaya Mlisho Kikwete.
  mpaka sasa mimi sijui raisi wangu anafikilia nini kuusu hii nchi ikiwa pamoja na watu wake na rasilimali zake. ndugu zangu pamoja na mambo yate yaliojitokeza katika kipindi chake mpaka sasa. JE RAISI WETU ANAFIKILIA NINI KUUSU HII NCHI HAPO BAADAE?. NISAIDIENI MAJIBU.
   
Loading...