Mh. Rais jitafakari madaraka yamekulevya; Wapinzani si maadui wa wananchi kama unavyofikiria

Hata Lissu akistaafu active politics, asiwe kiongozi wa Chadema hakuna atakayemuuliza
Tambua hakuna MTU ambaye anaweza kujipambanua kama asiye na mapenzi ya chama chochote. Issue hapa in active participation in politics.
Jaji mstaafu hakuomba uraisi mpaka alipostaafu, haingewezekana akawa Raisi akiwa Jaji Mkuu.
IGP hakuomba ubunge mpaka alipostaafu, hawezi kuwa mbunge wakati ni IGP
Mwanasheria mkuu hakuomba ubunge mpaka alipostaafu, hawezi kuwa mbunge wakati ni AG.
Lissu astaafu uongozi Chadema, then agombee maana hawezi kuwa Rais TLS wakati in kiongozi wa Chama.
Kama Mwanasheria wa Chama CDM anagombea basi turuhusu na CCM nao walete mwanasheria wao,
Turuhusu vyama vingine pia
Turuhusu waziri wa sheria nae agombee.
Turuhusu na Mwanasheria mkuu wa Serikali nae agombee
Turuhusu na Jaji mkuu nae agombee
Vyama vya kitaaluma visingiliwe kisiasa.
Kwa sasa Chama cha madaktari hakiwezi kuongozwa na Mashinzi akiwa bado ni Katibu Mkuu wa Chadema au Dr. Kigwangala akiwa Naibu Waziri Afya

Kwani katiba ya TLS inasemaje kuhusu hayo uliyoandika? Kama hana sifa hawatomchagua, Magufuli au mtu mwingine yeyote hana haki ya kuwapangia. Waacheni watimize matakwa ya katiba yao.
 
Kwa fikra zake magufuli ni kwamba wapinzani ndio chanzo umaskini Tanzania na ndio wanazuia maendeleo ya nchi!!! Pole sana wa tz na hasa wapenda mageuzi.
 
Kama kushindwa kujielewa na kukosa strategy utoke vipi, basi unaishia udaku na roho mbaya ambayo haina kikomo...yaani unatengeneza uhasama.

Unaishia kuongelea maswala very trivials, kwa hio wote waliokua ndani ya chama cha wanasheria wanategemea kuteuliwa na Muheshimiwa kupewa nafasi ya ujaji.. au madhumuni yao kulinda haki na katiba? Nimechanganyikiwa.

Dah CCM chama changu, lkn hapa tumechemsha vibaya vibaya..
Mkuu umenikosha sana.

Wenzio wa Lumumba wangekua hivi, hii nchi tungeikomboa
 
Nashangaa, mbona wakuu wa mikoa na wilaya wamejaa makada wa chama na hakuna tatizo
 
Muda huu tujikite kwenye masuala ya kitaifa ndiyo tujadili. Tumuhukumu rais kwa ahadi zake Na si maneno anayoyasema. Katiba iko wazi kama ataenda kinyume sheria na utaratibu utafuatwa. Hivi sasa ni kuwapima wanasheria wake mfano Ag na waziri wake wa sheria. Hawa wawili lazima watakuwa karibu na rais kwa Ushauri Na miongozo. Rais naye anatakiwa kupokea Ushauri wa watu walio karibu naye kabla hajatengeneza speech.
 
Mwanzoni sikutaka kuamini kama ile kauli ya Dr. Mwakyembe ilikuwa yake, nilijua atakuwa alitumwa na mh. Rais kupima kina cha maji.

Mimi siyo muongeaji sana ninachotaka kukuambia mh. Rais ipo siku hautakuwa Rais na utakuwa ni raia kama mimi tu, na itakuwa ni bahati mbaya sana kwako pale unaemtendea mabaya ukiisi unamkomoa baadae ndo akawa ni rais na ikawa ni mlipa kisasi kuzidi wewe utasaga meno.


Mfalme hajalibiwi na yeye ndiye anajua
 
Back
Top Bottom