Mh r.mengi wana migodi wasikufanye msukule wao!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh r.mengi wana migodi wasikufanye msukule wao!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 28, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,158
  Likes Received: 5,589
  Trophy Points: 280
  Mh mengi tunashukuru kwa kutujulisha mambo yatokanayo huko migodin..labda kwa kifupi tu ni kweli wanasaidia ila shida iliopo wanachotoa ama ulichoonyeshwa ni pesa ndogo sana kutegemea na pesa wanazochota na kulepeka huko kwao........
  Mh mengi wanachollilia watanzania ni kiasi kinachoondoka ardhi yao na si wanachotoa kam a ulivyosikia wametengeneza madarasa kadhaa,..vyoo nk lakini wanachota ngapi umepewa mchanganuo wanachopata na wanachotoa??

  Mungu ibariki tanzani
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Namshauri Mengi aende Tarime pia aone maafa yaliyosababishwa na wachimba madini kwa wakazi wa eneo hilo.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,158
  Likes Received: 5,589
  Trophy Points: 280
  Huko ndiko kumenifanya nimtolee uvivu mzee wangu nasikitika leo wamewapa zaidi ya dk 50 wanaelezea kazi za mgodi si ,ngetangaza misiba kama bango bure mpate fadhila...hao wanajali pesa wanaondoka na kuwaacha maskin watanzania...nenda tarime mzee wangu ujue wachimba madini yako na karaha za wananchi...
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  bado sijaelewa motive ya mengi kwenda kule migodini!!! sijui ndio anammaliza dogo kabisa au kweli kuna interest

  i would rather see him visiting Nyamongo kama ndio hivyo
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,158
  Likes Received: 5,589
  Trophy Points: 280
  Tatizo hii sekta imeingiliwa na watu wakubwa wa seriklini wana share nao na wengine wansimamia ulinzi wa nch ni vigumu kuwambia ukweli...picha za north mara hadi kipofu ameziona hakuna siku kikwete katoa pole,..anasubiri ajali watu wafe akimbize kelele zake
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Usisahau kuwa Mengi ni CCM.
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,158
  Likes Received: 5,589
  Trophy Points: 280
  MTOA HABARI MWANAHABARI YOYOTE AMA MTU WA KARIBU NA MENGI NAOMBA U PASTE UMPELEKEE HII!!

  ADELINA John Katunzi, hataweza kusahau na kusamehe mzungu David Human, ndani ya mgodi wa dhahabu wa GGM (Geita Gold Mine).

  Anashikilia kuwa mzungu huyo alitumbukiza mkono ndani ya chupi yake na kugusa uke wake kwenye lango la kutokea mgodini humo, wilayani Geita.

  Adelina alifukuzwa kazi wiki mbili toka afanyiwe operesheni kutokana na ugonjwa wa apendiksi (kidole tumbo). Operesheni ilifanyiwa hospitali ya Mwananchi jijini Mwanza.

  Akijua hajajaza fomu za kudai mafao yake kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF), Adelina alikataa kurudisha kitambulisho cha kazi, ili awe anakitumia kuingia mgodini kufuatilia madai yake.

  Ilikuwa katika kukurukakara za kutaka arejeshe kitambulisho, mkuu wa ulinzi, David Human aliishiwa subira, kwani angeweza kungoja mlinzi wa kike aje kumpekua Adelina.

  Badala yake alitumbukiza mkono sehemu nyeti za mwanamke huyo kwa madai ya kutafuta kitambulisho, "kitendo kilichofanya nilie kwa sauti huku walinzi watatu wa lango kuu wakishuhudia," anasimulia Adelina.

  Katika ushahidi wake mahakamani, unaoendana na ule wa mashahidi wengine watatu (walinzi) wa upande wa mashitaka, Adelina anadai alisukumwa na kubanwa kwenye ukuta, akakamatwa mikono, na Human akatumbukiza mkono kwenye chupi yake na kugusa sehemu zake nyeti.

  Lakini polisi, katika maelezo yaliyosomwa mahakamani walidai kuwa Human alikamata "makalio, matiti na uke" wa Adelina. Mtetereko huu unasadikiwa kuathiri sana kesi hiyo.

  Katika hukumu yake ya tarehe 18 Agosti 2008, hakimu Zabron M. Kesase wa mahakama ya wilaya Geita, anasema "...ni shahidi wa kwanza (Adelina) anayepaswa kulaumiwa kwa kusababisha yote haya."

  Hakimu Kesase alisema katika hukumu, "Angekuwa (Adelina) amerejesha kitambulisho kwa wakubwa zake, yote haya yasingetokea. Hivyo namwona mshitakiwa hana hatia na namwachia huru."

  Katika kesi hiyo Na. 147 ya 2007 hakimu ananukuu hati ya mashitaka inayosema mshitakiwa alimshika Adelina matiti, makalio na sehemu nyeti.

  Hakimu anajenga hoja kwenye tofauti za kauli ya hati ya mashitaka na ushahidi uliotolewa mahakamani, kwamba hakuna hata mmoja, hata Adelina mwenyewe, aliyesema mshitakiwa alishika makalio au matiti ya Adelina.

  Haikufahamika iwapo polisi waliandika kwa makusudi, hati ya mashitaka inayotofautiana na madai ya Adelina ili kujenga mashaka yawezayo kumsaidia mshitakiwa.

  Adelina alifukuzwa kazi tarehe 5 Machi 2007. Barua ya kumfukuza ilisainiwa na Meneja Mark Jackson wa kampuni ya ATS ambayo inatoa huduma za chakula mgodini. Ingawa Adelina alikuwa analipwa na ATS, vitambulisho vyote vya wafanyakazi mgodini ni vya GGM.

  Sababu za kumfukuza zinaelezwa kuwa ni "kampuni kukosa imani" naye. Basi.
  "...unafahamishwa kwamba uongozi umeamua kukatisha mkataba wako wa ajira kuanzia leo tarehe 17/02/2007 baada ya kukosa imani na wewe kwenye kazi yako…" anaeleza Jackson.

  Barua ilimtaka Adelina kurudisha vifaa vyote vya kampuni alivyokabidhiwa na kuahidiwa kulipwa haki zake anazostahili.

  Adelina anakiri alirudisha vifaa vyote vya kampuni isipokua kitambulisho. "Nilikataa kurudisha kitambulisho kwa sababu nilikuwa nawadai mafao yangu kutoka mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF).

  "Na pale mgodini huwezi kuingia bila kitambulisho; nilijua watanizuia kuingia kwa kuwa nawadai," anaeleza.

  Baada ya Adelina kugoma kutoa kitambulisho, meneja Mark Jackson, anadaiwa kuwaamrisha walinzi watatu waliokuwa kwenye lango kuu wachukue kitambulisho kwa nguvu.

  Walinzi hao, Richard Maganga, Niclaus Misenya na Amos Makongoro walikataa kutii amri ya Jackson kwa madai kuwa angekaguliwa na kushughulikiwa na mlinzi wa kike na siyo wao wanaume.

  Kilichofuata ni Jackson kupiga simu kwa mkuu wa walinzi, David Human na Adelina akazuiwa kutoka nje ya lango.

  Adelina anasimulia, "Alipokuja David akaniuliza, ‘wewe ndiye Adelina John?' Nikamjibu ndiye mimi. Akaniambia kwa ukali, ‘lete kitambulisho.' Nikamwambia siwapi mpaka mnilipe haki zangu zote."

  Adelina anasema, wakati huo alikuwa ameweka kitambulisho kwenye matiti; ndipo alikihamisha na kukitumbukiza kwenye chupi kwa mbele.

  "Alipoona nimeweka kitambulisho kwenye chupi akanikamata na kutumbukiza mkono; alishindwa kukitoa kitambulisho badala yake akanishika ukeni," anasimulia Adelina huku chozi likitiririka kutoka jicho lake la kulia.

  Purukushani hizi ziliishia pale Adelina alipokubali kuingia kwenye gari la mgodi na kwenda moja kwa moja hadi ofisi ya mwanasheria wa GGM akiongozana na Human na meneja wa ATS.

  Adelina anasema mwanasheria alimsihi akabidhi kitambulisho, pendekezo ambalo alikubali, lakini akamfafanulia kuwa anaweza kumshitaki aliyemwingiza mkono katika sehemu za nyeti.

  Kwa mwaka wa nne sasa, mwanamke huyu mwenye umri wa miaka 31, mtariki na mwenye watoto wawili, hajalipwa mafao yake.

  Richard Maganga, mmoja wa mashahidi upande wa mashitaka na ambaye ushahidi wake ulifanana kabisa na ule wa Adelina, naye tayari amefukuzwa kazi tangu mwaka 2008. Alikuwa amefanya kazi ya ulinzi mgodini kwa miaka minane.

  Ingawa alikuwa mlinzi, barua yake ya kufukuzwa ilimhusisha Maganga na wizi wa mafuta ya mashine/mtambo wa kunyanyulia mizigo.

  "David alitulazimisha mimi na wenzangu wawili tumnyang'anye Adelina kitambulisho chake, lakini tulikataa," anaeleza Maganga nakukana tuhuma za wizi akihoji, "Kama ni wizi si wangenipeleka mahakamani?"

  "Sasa Adelina alipopeleka kesi mahakamani nilitoa ushahidi kama nilivyoshuhudia. Ushahidi wangu ulizingatia kilichotendeka kama Adelina alivyoeleza. Bila shaka hilo ndilo lilinifukuzisha kazi," anasema Maganga.

  Kama ilivyo kwa Adelina na Maganga, ndivyo ilivyo kwa Emmanuel Lesilwa. Alianza kazi 2004. Aliachishwa kazi 16/05/2008.

  Anadai alifanyiwa operesheni ya apendiksi mwaka 2007, katika hospitali ya Mwananchi iliyoko mjini Mwanza, ambayo ndiyo inatibu wafanyakazi wa mgodi wa GGM.

  Aliporudi kazini meneja wake, Felix Adolf alimwabia utendaji wake umeshuka na akamwachisha kazi hata kabla kidonda cha operesheni kupona.

  Usalama kazini ni mdogo. Sababu za kufukuzwa au kuachishwa kazi ni dhaifu. Uelewa wa wafanyakazi jinsi ya kujitetea, kulinda na kupigania haki zao ni haba.


  ANAJUA UPUUZI WA HAWA WAZUNGU AMA ANAWAONYESHA TU KWENYE TV DK 40 ZA UPUUZI...HAWANA ADABU KABISA
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kamwe sintosahau... ila nina imani naye kwamba ameshakuwa daring enough ku-defy some of CCM bigwigs!!!

  Mengi ni mmoja kati ya wachache wa CCM wanaoweza kufanya maamuzi magumu huku akijua kuna watu atawaudhi....

  My gut feelings zinanionyesha kwamba kuna personal issue ndogo anaiaddress
   
 9. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,959
  Trophy Points: 280
  Kaka huna habari tu? au hujasoma signs? aidha Mkulu kanunua shares au yuko njiani kununua shares za Barrick Gold Africa, so kilichobaki ni kusafisha Barrick image to the public! Hao ndo wafanya biashara kaka! Kuanzia leo hamna bad publicity on Barrick :), Mengi na Barrick ni dugu moja
   
 10. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii thead imeanzia katikati mbona PDiddy? Sisi wengine hatupo huko, lakini nimeweza walau kung'amua kuwa Mengi ametembelea migodi, au?

  Kwa nini umempa cheo cha "mheshimiwa"? Si kwamba yeye si mzee wa kuheshimiwa,la, lakini kwa sababu hiki cheo siku hizi kimegubikwa na kila aina ya mambo yasiyofurahisha, sikipendi.
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,158
  Likes Received: 5,589
  Trophy Points: 280
  Ni hivi mkuu mzee ameenda migodini majuzi akapaka sana watu waheshimu wawekezaji atuwapendi tuwe nao kama ndugu wanatusaidia wakaonyesha na vijishule vyao vyoo bafu nk..sasa mzee akuishia hapo akadai kumbe yale malumbano ya bungeni ati wanasiasa wanaenda kuomba hela wakitoka wankuwa tofauti wakati wakiwa mgodini wanakuwa kitu kimoja ..mmh kishwa kikapata moto...ni huyu mzeewangu kweli leo kawapa zaidi ya dk 50 migodini na wale wazungu wakielezea matatizo wanayokumbana nao wanaangaishwa na watu awana amani..utakuwaje na amani na jambazi..ama fisadi

  naona reginald antaaka kuanza kutuchafua sasa

  reginald usifike uko
   
 12. r

  rosebella Member

  #12
  Mar 29, 2010
  Joined: Jun 23, 2008
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Adeline amenisikitisha sana. hawa watu hawafai jamani wanafanyisha binaadamu mapenzi na mbwa siwapendi kabisa
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,551
  Likes Received: 18,226
  Trophy Points: 280
  .
  De Novo, there is one and only motive, kuwaambia Watanzania kuwa yeye ni mmoja wa wamiliki wa Barick.

  Just thinking aloud, baada ya IPO ya ABG kule LSE, Mzee atakuwa ni mmoja waliograb hizo share, baada tuu ya kurejea nchini, akabisha hodi kukagua alichonunua.

  Tangu Barick wameanza huduma, ndio mara yangu ya kwanza kuonyeshwa mtu wa kawaida, akisindikizwa mgodini na kuchimba kwa mfano in front of TV Crew.
   
 14. mtuwatu

  mtuwatu Member

  #14
  Mar 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  du,dunia imekwisha haya mambo yanatisha ukisoma!!!
  Mungu tubariki sisi na watoto wetu ...amen.
   
 15. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Swadakta.... mwenye nacho...
   
 16. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #16
  Mar 29, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  PASCO, nini maoni yako baada ya kuona mzee Mengi kama mtu wa kawaida wa kwanza akisindikizwa mgodini na kuchimba kwa mfano infront of TV crew....
   
 17. mtuwatu

  mtuwatu Member

  #17
  Mar 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jamaani mimi sioni post za leo kuhusu hii mada,iz zea sam sing'i rong'?
   
 18. mtuwatu

  mtuwatu Member

  #18
  Mar 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 95
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yawezekana akawa na share,na sio jambo baya kabisa na mimi naamini kabisa huyu mfanyabiashara amenunua share kutoka kwa kampuni ya barrick gold mine maana walitangaza nia yao ya kutaka kuuza share zao kwa 70% kama sijakosea takribani miezi miwili iliyopita,na hii ni baada ya kuwaza aibu itakayowakumba pale ambapo dunia nzima itakapo gundua kwamba miaka yote hiyo wakiwa tz walikua wakitoa 4% kwa tz - 3% serikali kuu na 1% vijiji miliki.
  Kwahiyo sio jambo la ajabu kwangu mimi kuona mengi amenunua maana yy anatengeneza pesa na anawaza kila siku atapataje pesa nyingi zaidi.
  Good for Mengi ana mawazo ya kibepari - safi sana.
  Mimi shida yangu ni kwa serikali kujifanya hawajui matatizo yatokanayo na migodi afu na hiyo tabia ya kuwaruhusu hawa wawekezaji kubadirisha majina kila siku ili kukwepa kodi - kama walivyofanya hao kutoka Barrick Gold Mine(BGM) kuwa African Barrick Gold(ABG).
  Nauulaani umaskini kwa jina la ........., ila sijui kwanini Mungu anaruhusu haya yatokee kwa kipindi kama hiki anyway - yeye Mungu alietupa utajiri huu anajua kwanini inatokea kwa watu wake laiti kama hawa wakanada wangekuwa wanatendewa mambo kama haya tunayofanyiwa hapa kwetu ...............dunia yote ingejua na actions zingechukulia fasta sana.

  Mengi kila la kheri kama umeingiza hela yako humo African Barrick Gold. Ila tambua macho ya watanzania wengi ni kutaka kuona faida ya kuwa na migodi nchini mwetu!!!!!
   
Loading...