Mh. Mwakyembe TRL ITAKUSHINDA UKIENDEKEZA KUTAKA SIFA.

Mzee wa ngano

Senior Member
Joined
May 3, 2012
Posts
184
Reaction score
55
Niliposikia huyu bwana kapewa wizara ya uchukuzi nilijua kuwa sasa kumekucha. Mimi hua siku zote namchukulia huyu muheshimiwa kama mtu wa kazi miongoni mwa watu wachache wa CCM. Nilijua anataka kufufua makampuni ya uchukuzi likiwemo TRL. Nasikitika kuwaambia watanzania kuwa hayo mambo ambayo hadi sasa kayafanya hayana mchango wowote kwa maendeleo ya TRL bali kwa wakazi wa maeneo ambayo reli inapita na zaidi sana yanaididimiza TRL. wana JF Napenda mjue kuwa TRL haiwezi kufaidika kwa ajili ya city train, train ya abiria ya kwenda Mwanza, Kigoma au Mpanda.

Hizi train zinatembea ili kutoa huduma kwa wananchi wa nchi hii. Kwa mantiki hiyo mimi sikuona kama huyu muheshimiwa sana alikuwa na sababu ya kuanza na haya mambo. Ila najua kwavile mambo haya yanagusa watanzania wLio wengi naona kaona bora ayafanye kwanza ili watu wamjue. Kakosea sana. Kama kumjua watu tulishamjua tangu enzi za sakata la richmond na anguko la Lowasa. Akiendelea kutafuta sifa zaidi anguko lake kisiasa litakuwa kubwa kuliko mtu awaye yote aliyewahi kuongoza hiyo wizara. NAWASILISHA.
 
Mbona hueleweki, kipi ulitaka afanye au ww unadhan iwe vp, kwani umeambiwa train ya kigoma na mpanda hazifanyi kazi? Na hujui treni ya mwanza ilokuwa imesimama kwa miaka mitatu imeanza kufanya kazi siku chache baada ya kuanza kwa city train, yawezekana una point ila kwa uliyoyaeleza umekaa kimajungu na hueleweki.
 
Ndugu yangu mbona kila nikisoma network inakata?.Husomeki wewe hata kidogo.Afadhalia Mwakyembe kafanya kitu kinaeleweka.Kama unaponga pinga kwa hoja wazi na sio hisia tu. ukijipanga njoo tukusome.
 
naona una point, reli iwe sawa, pata au rekebisha vichwa halaf pitisha train. lakin vip hela ya kurekebishia hayo ipo kwasasa?
 
Pamoja na kutokukuelewa lakini hebu niambie kama priority isipokuwa huduma kwa wananchi, wewe ulitaka TRL iwe na priority ipi? Biashara? sisi hatutaki serikali inayofanyabiashara, biashara ni za watu binafsi, tunataka serikali ya aina anayofanya mwakyembe, ambayo ni huduma kwa wananchi maana hasara za TRL zipo pale pale hata wakati ilipokua inadaiwa kufanyabiashara, na bado hasara hiyo tuliishi kufikia kwa kodi zetu, faida wakila wachahe, ni bora hii ambapo hatupati faida lakini wananchi wanaweza kufanya mizunguko yao ikiwemo ya city train.
 
Niliposikia huyu bwana kapewa wizara ya uchukuzi nilijua kuwa sasa kumekucha. Mimi hua siku zote namchukulia huyu muheshimiwa kama mtu wa kazi miongoni mwa watu wachache wa CCM. Nilijua anataka kufufua makampuni ya uchukuzi likiwemo TRL. Nasikitika kuwaambia watanzania kuwa hayo mambo ambayo hadi sasa kayafanya hayana mchango wowote kwa maendeleo ya TRL bali kwa wakazi wa maeneo ambayo reli inapita na zaidi sana yanaididimiza TRL. wana JF Napenda mjue kuwa TRL haiwezi kufaidika kwa ajili ya city train, train ya abiria ya kwenda Mwanza, Kigoma au Mpanda.

Hizi train zinatembea ili kutoa huduma kwa wananchi wa nchi hii. Kwa mantiki hiyo mimi sikuona kama huyu muheshimiwa sana alikuwa na sababu ya kuanza na haya mambo. Ila najua kwavile mambo haya yanagusa watanzania wLio wengi naona kaona bora ayafanye kwanza ili watu wamjue. Kakosea sana. Kama kumjua watu tulishamjua tangu enzi za sakata la richmond na anguko la Lowasa. Akiendelea kutafuta sifa zaidi anguko lake kisiasa litakuwa kubwa kuliko mtu awaye yote aliyewahi kuongoza hiyo wizara. NAWASILISHA.

Mimi binafsi namkubali mwakyembe ameweza kuanzisha City train ni kitu cha kihistoria hapa Tanzania, Pia amefufua Safari za Train za kwenda Mwanza , kweli Mwakyembe namkubali , Tuendeleee Tumpe muda zaidi afanya kazi yake kote atafika huko Mpanda na sehemu zingine ambako Train linahitajika Tumpe muda tuvute subira.
 
Dr Harrison Mwakyembe naona majukumu yake katika TRL ameyamudu, anastahili pongezi.
 
mleta mada ananikumbusha mwana JF mmoja alileta thread inayosema hivi 'humu jamvini kuna watu wana matatizo ya uelewa'. Mleta mada naona ana matatizo ya uelewa kwa hiyo haeleweki. Akajipange arudi siku za usoni.
 
mleta mada anayo hoja lakini ameshindwa kujieleza. mashirika yetu ya reli ambayo ni TRL na TAZARA yako ktk hali mbaya kifedha na ufanisi ni wa chini kabisa. utetezi kwa Mwakyembe kwasasa ni kwamba tukubaliane kwamba ameteuliwa kuongoza wizara wakati bajeti ya 2012/13 tayari imeisha andaliwa. hana fedha za kutekeleza mipango ya maendeleo zaidi ya hiyo aliyopangiwa!
 
Niliposikia huyu bwana kapewa wizara ya uchukuzi nilijua kuwa sasa kumekucha. Mimi hua siku zote namchukulia huyu muheshimiwa kama mtu wa kazi miongoni mwa watu wachache wa CCM. Nilijua anataka kufufua makampuni ya uchukuzi likiwemo TRL. Nasikitika kuwaambia watanzania kuwa hayo mambo ambayo hadi sasa kayafanya hayana mchango wowote kwa maendeleo ya TRL bali kwa wakazi wa maeneo ambayo reli inapita na zaidi sana yanaididimiza TRL. wana JF Napenda mjue kuwa TRL haiwezi kufaidika kwa ajili ya city train, train ya abiria ya kwenda Mwanza, Kigoma au Mpanda.

Hizi train zinatembea ili kutoa huduma kwa wananchi wa nchi hii. Kwa mantiki hiyo mimi sikuona kama huyu muheshimiwa sana alikuwa na sababu ya kuanza na haya mambo. Ila najua kwavile mambo haya yanagusa watanzania wLio wengi naona kaona bora ayafanye kwanza ili watu wamjue. Kakosea sana. Kama kumjua watu tulishamjua tangu enzi za sakata la richmond na anguko la Lowasa. Akiendelea kutafuta sifa zaidi anguko lake kisiasa litakuwa kubwa kuliko mtu awaye yote aliyewahi kuongoza hiyo wizara. NAWASILISHA.

....wewe ni O. Nundu?
 
Mbona mnalalama kuwa mwenye maada haeleweki? Kiukweli ni kwamba jamaa anaeleweka vizuri, tena sana ya kuwa yeye ni miongoni mwa vilaza, hajui kupangilia hoja na ni mtu wa majungu..!
 
Mleta hoja, ondoa upuuzi wako hapa. Mtu yeyote anayefanya jambo lenye maslahi na Taifa letu tunampa big-up bila kujali anatoka chama gani maana nchi haiwezi kuendeshwa na propoganda za siasa.
 
Mkuu punguza bangi.nadhani ukiamka kesho ukasoma ulichoandika mwenyewe utashangaa.si mbaya umeongeza wingi wa post
 
Mzee Ngano:Usiwe na moyo wa kukosa shukrani! Kazi aliyoifanya Mwakyembe kuhusu reli anastahili pongezi. Tafadhali elewa kuwa maendeleo ya kweli yanatokana kwa kuweka rasilimali watu mbele ya vitu vyote. Kwa vyovyoe kazi ile isingekuwa na maana kama isingelenga wananchi kwanza. Mengine yatafuata baadaye. Wananchi walioridhishwa na mwenendo wa viongozi wao ni rahisi kujumuika katika harakati za maendeleo kwa dhati. MWAKYEMBE HONGERA SANA MUNGU AKUTANGULIE MILELE!!!!!
 
Mbona hueleweki, kipi ulitaka afanye au ww unadhan iwe vp, kwani umeambiwa train ya kigoma na mpanda hazifanyi kazi? Na hujui treni ya mwanza ilokuwa imesimama kwa miaka mitatu imeanza kufanya kazi siku chache baada ya kuanza kwa city train, yawezekana una point ila kwa uliyoyaeleza umekaa kimajungu na hueleweki.

Kuna wimbo jina silijuwi ila unasema wape wape vidonge vyao. Kweli umempa Panadol maana haeleweki.
 
Mleta mada au nawewe umekumbwa na uwajibikaji aw waziri Huyu kwa namna moja AMA nyingine namaanisha umetimuliwa Huko bandari nini?maana hakuna asiyeona kazi ya Harrison labda watu wenye walakini kma wewe
 
Back
Top Bottom