Ushauri wangu kwa Waziri Prof Mbarawa juu ya changamoto na "uozo" wa Uwanja wa ndege wa JNIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ushauri wangu kwa Waziri Prof Mbarawa juu ya changamoto na "uozo" wa Uwanja wa ndege wa JNIA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by barafu, Jul 18, 2017.

 1. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,173
  Likes Received: 24,596
  Trophy Points: 280
  image.jpeg image.jpeg


  Imekuwa ni kawaida kuwepo kwa malalamiko mengi sana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA).Malalamiko haya ni ya wadau wa usafiri wa anga wa ndani na nje ya nchi.

  Imekuwa ni kama tatizo sugu,kila mara na kila wakati watu wanaotumia uwanja wa JNIA wamekuwa wakilalamika sana juu ya hali,uduni wa huduma,uchafu,kadhia ya joto na mambo mengi yenye kukera na kupoteza taswira nzuri ya uwanja wetu.Hiki ni kioo na sura ya Taifa,lakini uwanja huu unatia aibu.

  Rais amefanya ziara za kushitukiza kama mara mbili,lakini holaa watu hawana cha kubadilika,Mh.Waziri Mbarawa kazungukia pale zaidi ya mara tatu,naambiwa wakati mwingine akienda rasmi,na wakati mwingine kimyakimya bila vyombo vya habari,lakini bado watu hawabadiliki.Mambo ni yaleyale ya "bussiness as usual".Hapa kuna tatizo sio bure.

  Kumekuwa na tatizo "sugu" linalotokana na "usugu" wa viongozi waliokabidhiwa mamlaka ya kuongoza kiwanja/viwanja vya ndege Tanzania.Haiwezekani kwa malalamiko yale yote na tuhuma za abiria wa ndani na nje ya nchi,lakini kila kiongozi akifika hapo anakuta mambo ya hovyo ni yaleyale au zaidi ya yale aliyoyakuta mwanzoni.Hapa pana tatizo kubwa

  Kwa taarifa rasmi kutoka watu wa ndani ya mamlaka hiyo,ni kuwa toka mwaka 2015 mpaka sasa 2017,kuna Wakurugenzi wanne (04) waliopewa nafasi ya kuongoza uwanja wa JNIA na wote kwa sababu moja au nyingine wameshindwa na kuondolewa kwenye kiti hicho.Yaani ndani ya kipindi cha miaka miwili,wakurugenzi wanne wamekalia kiti na kuondoka.Hii ni uthibitisho kuwa suala la "Management" limewashinda.

  Hii ni kusema ndani ya taasisi hiyo,uweledi na umakini katika suala la "Management" ni butu.Wanajaribiana uongozi kama kiatu cha mtumba,anajaribu huyu na huyu bila mafanikio.Sasa huwezi kufanya majaribio yasiyo na kikomo,matokeo yake inakosekana "Sustainability" katika kufikia kile ambacho nchi washindani katika masuala ya "aviation" wanakifikia.

  Kwa taswira hii,bila shaka ni ni moja kati ya mamlaka ambayo walio na dhamana,hawana utaratibu wa kuandaa viongozi wa baadae kwa kufuata uweledi na si kujuana na kupendeleana.Waziri Prof.Mbarawa usipofanya uamuzi mgumu,kila siku utakuwa unakutana na madudu na kuondoa uongozi,mwisho wa siku kunakuwa hakuna maendeleo endelevu.

  Haiwezekani,mtu anaharibu kitengo hiki,halafu anapelekwa kitengo kingine,ukifumba na kufumbua anaibukia kwenye ukurugenzi wakati huku nyuma rekodi yake ni chafu na ya hovyo,ila sababu ana ndugu au rafiki,basi anapanda kwa kasi kuelekea katika vyeo.Aviation haiitaji "vilaza" na "wanaogushi" uweledi,mwisho wa siku tunaabika kama Taifa na si mtu mmoja.

  Kwa msongamano wa abiria wa kuja na kuondoka katika uwanja wa JNIA,uchafu,uzembe,uweledi mdogo wa viwango vya kimataifa kwa wafanyakazi wa uwanja,mikataba inayotia shaka pamoja na uzembe kwa level ya Management ya TAA kama Operator wa kiwanja,mambo haya yanaweza kuwa kama hatua kuelekea kupunguza changamoto hizi.

  (1)Mh.Waziri Prof Mbarawa unaweza kufanya "Secondment".Kuchukua watu wenye uweledi wa masuala ya "management",waliobobea ili waje kusaidiana na watu wenye uwelewa wa mambo ya aviation na kuiondoa mamlaka hii,kutoka hapo ilipokwama kwenda hatua nyingine.Jambo hili liliwezekana kwa Mchechu,kutoka katika sekta ya fedha mpaka kwenye mambo ya nyumba NHC,na kwa kiasi fulani ikaonekana kuna mabadiliko.Achana na hizo degree za kuchukua asubuhi pale GongolaMboto Kampala na kuzikabishi kiwanja kikubwa kama hicho.

  (2)Kwa kupunguza suala la msongamano wa abiria nyakati za "Peak hours",ambapo kwa JNIA naambiwa inaanza saa 1500hrs-1730hrs.Kupunguza msongamano huu,TCAA kama regulator wa usafiri wa anga na TAA kama Operator wa viwanja vya ndege,wawashauri "Airlines" wanaokuja Tz,kubadili kidogo "slots" zao ili kupunguza uwezekano wa ndege zote kubwa kuingia kwa wakati unaokaribiana.

  Haiwezekani jengo kama lile,lipokee abiria zaidi ya 2000 kwa wakati mmoja.Muda huohuo Emirates analeta Boeing 7777-300ER inashusha abiria 410,Ethiopia analeta B777-300 abiria 400,Qatar na Dreamliner abiria 350,S.Africa abiria 180,Oman Air 150,Mozambique,Air Zimbabwe,Etihad,Kenya Airways na RwandAir.Hawa wote wakishuka ndani ya muda huo...Lazima uwanja uzidiwe.Hivi ndivyo imefanyika katika viwanja vingine duniani,kueleza hali ya uwanja na kuomba mabadiliko kidogo ya ratiba.


  (3)Ukarabati wa mara kwa mara wa miundombinu chakavu.Hakuna ubishi kuwa kwa sasa uwanja wetu umezidiwa na uchakavu,na hii ni kutokana na uzembe wa muda mrefu,ama wa serikali yenyewe au management ya kiwanja.Kuandikia dokezo la ununuzi wa AC lakini mtu anatia ndani hela yote.AC nzuri zinanunuliwa zile za VIP LOUNGE wanakopita wakubwa,huku kwa kina mie,inapotezewa.Jengo la TBII tumelitumia toka 1980's.Nakumbuka lile la TBI tulizindua na Mzee Songambele wakati huo mkuu wa mkoa wa Dsm.Ukarabati/Matengenezo ya hapa na pale,yafanyike kwa umakini na si kwa zima moto.Zabuni za wanaopewa kukarabati zifuate taratibu na si kupeana kama sasa.

  (4)Kuboresha uweledi wa Wafanyakazi wa Kiwanja.Huwezi kuwa mfanyakazi wa kiwanja cha kimataifa halafu unakuwa "locoloco" tu.Unakutana na mtu wa security anafungua begi huku anakutupia lugha chafu,wanafikiri kuwa mlinzi basi ni kutoa lugha za vitisho na kukaripia.Hii ni kwa sababu hawa wanakuwa hata nchi nyingine hawajfika kujua wenzao wanafanyaje kazi.

  Msiwe wabahiri,pelekeni training hawa watu hata wajue huko duniani watu wanahudumiaje mteja.Wazungu wanesama "Travelling is like reading a book,those who do not travell,read only one page".Watumishi wengi wa JNIA wanaonekana wamesoma "page" moja tu.

  (5)Ajiri watu wenye uweledi na mishahara yenye unafuu.Kuna skendo hapo kuwa wengi wa security officers na "wacheza mpira".Yaani mkubwa mmoja hapo ni kiongozi wa team ya mpira ya wizara ya uchukuzi,ili apate team ya kwenda SHIMIWI kwa urahisi na apige panga posho za SHIMIW,anapachika wacheza mpira kitengo cha security,ambao atawatumia wakati wa michezo.Hii inasababisha kuwepo na watu wasio serious sana na kazi sbb wanajua wao wapo pale kwa mkono wa mkubwa na wanajishikiza tu ili wakati wa mshindano wawe na sifa za kuunda team ya uchukuzi.Si ajabu ukakutana na security anakutolea lugha chafu kama mgambo wa jiji

  (6)Ipeni TAA mamlaka kamili kama mlivyofanya kwa idara nyingine za Uchukuzi kama TCAA.Mamlaka hii kuwa "Semi-Autonomous" inapunguza uwezo wake wa kufanya mambo kwa haraka.Hivyo kuzorotesha utendaji wa kazi na utatuzi wa changamoto za hapa na pale.Serikali kuchukua kila kitu katika mapato ya mamlaka hizi,na kuondoa uwezo wa zenyewe kujipangia bajeti za matumizi ya ndani ni makosa.Huwezi kuwa na uwanja mkubwa kama huo,halafu pesa ya kununua "Conveyer Belt" inasubiliwa kuombwa hazina.Sasa nini umuhimu wa Gvt Agency Acts iliyoanzisha haya mashirika ya umma?

  Ni kweli watu walikuwa wapigaji,watu wamejipa safari za nje,watu wamejipa training kiundugu,lakini hizi kwa sasa zinawez kutafutiwa dawa na kuthibitiwa.Ipeni mamlaka hii uwezo wa kujiendesha.

  (7)Pitia mikataba yenye utata.Hii ni pamoja na hicho kimgahawa cha ajabujabu hapo nje,mara ya mwisho juzi nimeshuka hapo bado kipo.Unajenga kibanda juu ya maandishi ya "NO PARKING",tena kwenye eneo la kiwanja?Ni aibu sana.Migahawa na maduka kule juu departure Lounges...Fuatilia wale watu wanalipa kweli kodi?Hebu fuatilia hiyo kampuni ya Porters,ina uhalali kweli au ni biashara za watu?

  (8)Serikali iharakishe ufunguzi wa Uwanja wa Terminal Three.
  Hii inaweza kuwa suluhisho,itapunguza msongamano na aibu zinazopatikana Terminal Two.Wizara na serikali kwa ujumla,itilie mkazo uwanja huu uishe kwa wakati ili kukabiliana na changanoto za TBII.

  Mwisho,ninakutakia yote mema Ami Prof Mbarawa.Katika watu ambao wanajitahidi katika kuongoza bila mihemko ya hapa na pale,wewe ni mmoja wao.Ninakutakia kila la heri.Huu ni mtazamo wangu,sina chuki na mtu.Yaliyo na umuhimu yabebe,ushauri unaweza kupokelewa au kukataliwa.

  barafu wa JF,mapumzikoni Arusha Tz
   
 2. n

  nsereko m JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2017
  Joined: Jul 28, 2015
  Messages: 3,092
  Likes Received: 2,131
  Trophy Points: 280
  sawa.
   
 3. i

  isupilo JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2017
  Joined: Jan 25, 2015
  Messages: 281
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 180
  Duuh!!Haya ndio mabandiko,sio lawama tu bila ushauri
  Mkuu barafu upo vizuri sana....Hizi hoja unaweza mpa hata mbunge wa kwetu Kalenga azifikishe bungeni,hata sisi tumsikie...Angapata sifa sana kwa mapoint kama haya
   
 4. misasa

  misasa JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 5, 2014
  Messages: 6,524
  Likes Received: 3,254
  Trophy Points: 280
 5. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,173
  Likes Received: 24,596
  Trophy Points: 280
  Shwari mkuu!!Nipo sasa nyumbani...Nimekuja mara moja
  Si unajua "Northern Circuit" sasa ni "high Season"
   
 6. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #6
  Jul 18, 2017
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,169
  Likes Received: 2,218
  Trophy Points: 280
  Mbarawa ni the next president of Zanzibar...

  Huo uwanja mi nimeusema hadi nawaonea huruma viongozi wake.. kilio cha fees ya parking at least wamepunguza buku endapo ndege itachelewa baada ya Lisaa limoja hongera kwa hilo maana mmetuibia sana.

  Hicho ki fast food kuna siku nilitaka nikiondoshe hapo bei ya chakula hapo haishikiki kama Tel aviv kha!
   
 7. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,173
  Likes Received: 24,596
  Trophy Points: 280
  Naona unamtabiria makubwa ndugu yangu,Ami Prof.Mbarawa...Iwe kheri
  Hiyo fastfood hapo inatia aibu...ipo juu ya maandishi ya "NO PARKING",unaenda nje then unarudi,unaikuta hapo hapo
   
 8. bily

  bily JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 8,053
  Likes Received: 4,044
  Trophy Points: 280
  Mi sijajua kama wale wanasafiri huku duniani kuona ata viwanja vingine vilivyo smart kuanza watu wa chini mpaka wenye vyeo vikubwa mf Frankfurt, Amsterdam nk .
   
 9. Ndjabu Da Dude

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2017
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,785
  Likes Received: 514
  Trophy Points: 280
  Hao watu wenye "uweledi" utawapima vipi zaidi ya hizo "degree za kuchukua asubuhi pale GongolaMboto Kampala"?
   
 10. HORSE POWER

  HORSE POWER JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 22, 2015
  Messages: 1,298
  Likes Received: 698
  Trophy Points: 280
  Tuna safari ndefu kweli kweli.Huu uhuni wa kucheza na maslahi nadhani sasa Ku ahitajika adhabu ya kifo.Hakuna namna.

  Sent from my TECNO-Y3+ using JamiiForums mobile app
   
 11. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,639
  Likes Received: 2,062
  Trophy Points: 280
  Mkuu asante sana kwa bandiko hili lenye uweledi mkubwa
  Nimecheka sana eti degree za GongolaMboto
  Lakini hivi inakuwaje mtu anajenga eneo chini pameandikwa No Parking!??
  Na hapa ni uwanja wa Kimataifa tena nje na wanapita watu,vipi huko sirini anakuwa amepiga uovu mara ngapi?

  Waziri husika chukua ushauri huu
   
 12. Maboso

  Maboso JF-Expert Member

  #12
  Jul 18, 2017
  Joined: Feb 18, 2013
  Messages: 4,305
  Likes Received: 2,632
  Trophy Points: 280
  Mengi umeyaongea ila suluhisho la kudumu litatatuliwa na terminal three itakapofunguliwa. Ujenzi wa terminal three umezingatia changamoto nyingi zilizopo terminal two hasa kwa wasafiri wa kimataifa. Kikubwa ni kuishauri serikali ikamilishe haraka ujenzi wa terminal three.
   
 13. redio

  redio JF-Expert Member

  #13
  Jul 18, 2017
  Joined: Aug 27, 2016
  Messages: 998
  Likes Received: 888
  Trophy Points: 180
  Mtoa, mada kunamambo uzungumza kweli, lakini mengine aliyekupa taarifa amekudanganya nawewe umeamua labda kwakujua au mihemko Ku udanganya umma.

  Kwanza wewe sio pekeyako unae safiri kupitia JNIA. Kwaiyo kuongea mambo kama uwanja mchafu, unalindwa na wachezampira, Ac hakuna, mi nadhani ata uyo waziri atakushangaa!!

  Ule uwanja una AC zakutosha tena zinafanyakazi kwa uhakika, Timu iliyokwenda shimiwi mwaka huu ni wachezaji wawili tena wakuvuta kamba.

  Maeneo Mengi ya uwanja yako safi, maranyingine wageni hasa wazungu wamekua wakifurahia hali ya usafi, utakuta wamekaa chini,wakilala, kujinyoosha kwenye sakafu kwakua sakafu inang'aa kama kioo na viti vipo wazi.

  Kinacho leta taabu ni miundombinu haiendani na wingi wa abiria. Suluhisho ni kukamilika kwa uwanja Mpya. Wakurugenzi hata watolewe ulaya ningumu kupata mabadiliko unayo yahitaji. Kaunta za uhakiki wa tiketi mbaka immigration zipo chache, Ngazi za umeme zinasumbua kwakuzidiwa,na mengine mengi sasa utalaumu watendaji au uongozi?

  Sent from my TECNO W4 using JamiiForums mobile app
   
 14. kenstar

  kenstar JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2017
  Joined: Aug 24, 2015
  Messages: 2,309
  Likes Received: 1,385
  Trophy Points: 280
  Ni mawazo mazuri yakifanyiwa kazi, hasa peak hours kuhudumia ndege sita kwa pamoja ni shida lazima foleni iwepo, sioni ubaya wa hio restaurant nje hapo sababu sio kila abiria anajua juu kuna restaurant labda vibao elekezi viwe vingi vya kuwaelekeza sababu abiria upata shida wapi pa kula,bei ya parking ni kubwa ipunguzwe, maslai ya wafanyakazi yaboreshwe ukiona sehemu upati lugha nzuri customer care mbovu jua kuna njaa wanaweza wanafanya kazi lakini wamejaa stress za maisha, hawana motisha penye unyevunyevu kila mtu yuko happy na kazi yake, joto ni kali kweli sababu ya peak hours Ac zinashindwa kumudu wingi wa watu muda huo labda ziongezwe nguvu wakati huo wa peak na zipunguzwe kabla au baada ya peak hours ili zisiumize watu,pia serikali isiwe inachukua hela zetu kupeleka hazina iache baadhi ya asilimia zingine kwenye vyanzo vya mapato ili iwezeshe ukusanyaji zaid, auditing ndo ifanyike kwa mkazo zaid, weledi wa mtu autokani na chuo alichosoma anaweza kasoma gongo la mboto lakini kichwani kiweledi wa kazi yuko vizuri, labda km tunaangalia vyeti kuliko uwezo wa mtu.


  Sent from my TECNO-L8Plus using JamiiForums mobile app
   
 15. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,173
  Likes Received: 24,596
  Trophy Points: 280
  Mkuu redio
  Vyanzo vyangu vya taarifa sio vya kitoto...Vimeshiba kwa taarifa bila majungu.
  Hiyo timu ya mwaka hu imeenda hivyo baada ya kuwa na sera ya "Ubanaji wa Matumizi ya serikali"
  Lakini wakati wote,sehemu ya michezo ndio ilikuwa eneo la upigaji,watu waanawekwa kama security ili wakati wa msimu wa michezo,waende kama wanamichezo.

  Hii ilikuwa ni sehemu ya upigaji,kama mtu alipaswa kwenda na kupewa posho ya laki tatu,anapewa laki mbili,moaj inabanwa,na kwa sababu ni muajiliwa wa muda sabb ya michezo,hawezi kukwepa.Hii inasemwa na walio ndani ya mamlaka imesababisha sekta ya security kujaa wanamichezo walioajiliwa kwa muda kwa ajili ya msimu wa michezo.

  Siongei jambo nisilo na taarifa nalo za undani.Hakuna sehemu nimesema mimi nasafiri peke yangu,angalia usieleze jambo litakloibua mengine ukaukimbia mjadala
   
 16. Halima Msasambuaji

  Halima Msasambuaji JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2017
  Joined: Aug 24, 2016
  Messages: 473
  Likes Received: 1,153
  Trophy Points: 180
  barafu hongera kwa chakula cha ubongo, bandiko limeenda shule
   
 17. i

  isupilo JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2017
  Joined: Jan 25, 2015
  Messages: 281
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 180
  Hii inashangaza sana.Unajiuliza watu hawaendi nje huko na kujifunza?Aibu sana
  Hao security ndio wale wenye suruali za dark blue?wana lugha mbovu sana na wanadhani kukaa kwenye zile mashine na mageti basi wamemaliza kila kitu
   
 18. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,173
  Likes Received: 24,596
  Trophy Points: 280
  Ndio haohao....
   
 19. samurai

  samurai JF-Expert Member

  #19
  Jul 18, 2017
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 4,265
  Likes Received: 4,235
  Trophy Points: 280
  watu wasio na uwezo kichwani + Uzoefu kimataifa = matatizo mengi kwa Tanzania.

  Mkuu Barafu tunaongea mpaka tunakuwa Wagonjwa sasa, Mfumo mzima wa Tanzania kwa asilimia kubwa umejaza Vilaza ambao humeza hata wale wasio vilaza, Ukilaza kuanzia juu mpaka Chini umeleta uozo mkubwa kwenye mifumo karibia yoote ya nchi hii..
   
 20. barafu

  barafu JF-Expert Member

  #20
  Jul 18, 2017
  Joined: Apr 28, 2013
  Messages: 6,173
  Likes Received: 24,596
  Trophy Points: 280
  Hii ndio changamoto kuelekea maendeleo endelevu
   
Loading...