King Kong III
Platinum Member
- Oct 15, 2010
- 64,380
- 99,190
nini cha ajabu mkuu, ni lugha ya kigeni hiyo!! Mbona hamshangai mzungu akiboronga kiswahili?? Tuache hizoo kasumba za kikoloni................!lugha ya kimombo ilikuja kwa meli ....................
nimeipenda mkuu, ni kweli hatujitambui kwamba na sisi waafrika tunahati miliki ya dunia hii, yote hii shauri ya kutawaliwa na wakoloni.....tatizo kubwa la waafrika ni kujidharau baada ya kudharauliwa kwa miaka mingi na wazungu. Waafrika ni watu pekee ambao hudharauliwa kuliko watu wengine wowote wale duniani. Dharau hiyo imeendelea hadi katika lugha zetu, lugha za kiafrika zinaonekana si lugha za watu wasio na umuhimu wowote. Si walaumu watu wanaoona kuwa kutokujua kiingereza ni tatizo kubwa... Kwa sababu wamefanywa hivyo, si kwa matakwa yao, bali watu weupe wamewafanya wawe hivyo. Utumwa wa kiakili na kutawaliwa kiakili. Ukoloni wa akili ni mbaya kuliko ukoloni tuliouzoea.
Nimewahi kuzungumza na watu wa mataifa mbalimbali kama vile wajapani, wakorea, wajerumani, wachina, wahindi na waafrika wanaotokea katika nchi zinazozungumza lugha ya kifaransa. Baadhi yao wanazungumza kiingereza vizuri wengine hawana uwezo mkubwa. Kwangu sioni tatizo lolote, wala sishangai. Namshangaa, kwa hakika, sana mtanzania ambaye lugha yake ya taifa ni kiswahili analinganisha ubora wa mtu kwa kutumia lugha ya kiingereza.... Lugha ya wakoloni wake...
Suala la ajabu kabisa ni pale mzungu anapokea lugha ya kiswahili, au mtanzania anapokosea kuzungumza lugha ya kiswahili na anaonekana hajafanya kosa kubwa, lakini akikosea kiingereza tunalalamika.... Nasikitika kuishi kwenye jamii isiyojitambua na kuishi kama makopo matupu yenye mabaki makubwa ya ukoloni katika akili yake... Hatari!!!!
Nina wasiwasi na ubora wa elimu wa nchi yetu... Haiwezekani miaka hamsini baada ya uhuru watu wake "huru" wana mawazo yaliyochakaa kiasi hiki... Tuna safari ndefu ya kuutambua utu wetu, kuutambua utamaduni wetu na kuutambua uafrika wetu.
Mwafrika usipojitambua hutatambulika... "know thyself" socrates.
Ukiamua kutumia lugha fulani itumie vizuri Kwa sababu hakuna anayekulazimisha kuongea. Kuna vipindi chungu nzima vya kiswahili Kwa nini alikubali kwenda kushiriki hiki cha lugha za wazungu?
Ukiamua kutumia lugha fulani itumie vizuri Kwa sababu hakuna anayekulazimisha kuongea. Kuna vipindi chungu nzima vya kiswahili Kwa nini alikubali kwenda kushiriki hiki cha lugha za wazungu?
Ukiamua kutumia lugha fulani itumie vizuri Kwa sababu hakuna anayekulazimisha kuongea. Kuna vipindi chungu nzima vya kiswahili Kwa nini alikubali kwenda kushiriki hiki cha lugha za wazungu?
Tatizo kubwa la Waafrika ni kujidharau baada ya kudharauliwa kwa miaka mingi na Wazungu. Waafrika ni watu pekee ambao hudharauliwa kuliko watu wengine wowote wale duniani. Dharau hiyo imeendelea hadi katika lugha zetu, lugha za Kiafrika zinaonekana si lugha za watu wasio na umuhimu wowote. Si walaumu watu wanaoona kuwa kutokujua Kiingereza ni tatizo kubwa... kwa sababu wamefanywa hivyo, si kwa matakwa yao, bali watu weupe wamewafanya wawe hivyo. UTUMWA WA KIAKILI na KUTAWALIWA KIAKILI. Ukoloni wa akili ni mbaya kuliko ukoloni tuliouzoea.
Nimewahi kuzungumza na watu wa mataifa mbalimbali kama vile Wajapani, Wakorea, Wajerumani, Wachina, Wahindi na Waafrika wanaotokea katika nchi zinazozungumza lugha ya Kifaransa. Baadhi yao wanazungumza Kiingereza vizuri wengine hawana uwezo mkubwa. Kwangu sioni tatizo lolote, wala sishangai. Namshangaa, kwa hakika, sana Mtanzania ambaye lugha yake ya taifa ni Kiswahili analinganisha ubora wa mtu kwa kutumia lugha ya Kiingereza.... LUGHA YA WAKOLONI WAKE...
Suala la ajabu kabisa ni pale Mzungu anapokea lugha ya Kiswahili, au Mtanzania anapokosea kuzungumza lugha ya Kiswahili na anaonekana hajafanya kosa kubwa, lakini akikosea Kiingereza tunalalamika.... Nasikitika kuishi kwenye jamii isiyojitambua na kuishi kama makopo matupu yenye mabaki makubwa ya ukoloni katika akili yake... HATARI!!!!
Nina wasiwasi na ubora wa elimu wa nchi yetu... haiwezekani miaka hamsini baada ya uhuru watu wake "huru" wana mawazo yaliyochakaa kiasi hiki... tuna safari ndefu ya kuutambua utu wetu, kuutambua utamaduni wetu na kuutambua Uafrika wetu.
MWAFRIKA USIPOJITAMBUA HUTATAMBULIKA... "Know thyself" Socrates.