Mh Membe peleka Form ya kujitoa EAC

Mh Membe peleka Form ya kujitoa EAC

waziri wa uhusiano wa africa mashariki Mr. vi atakula wapi Tz ikijitoa? manake mwenyewe yupo kimya kweli tunasikia mara mkutano wa africa mashariki Nairobi sisi na Burundi hatupo, huu wa juzi Kigali JK hayumo(bora huu hakwenda wangekunjana na Kagame manake ameshamtukana na kumdhalilisha sana) na bahati mbaya hakuna kauli yoyote si kutoka kwa Membe wala Sitta mwenye Wizara, we have the right to know what's going on.
 
Yote yanawezekana japo busara pia zinahitajika kujua kwanza mzii wa haya mambo ila ushauri wako nimeupenda tu.
 
waziri wa uhusiano wa africa mashariki Mr. vi atakula wapi Tz ikijitoa? manake mwenyewe yupo kimya kweli tunasikia mara mkutano wa africa mashariki Nairobi sisi na Burundi hatupo, huu wa juzi Kigali JK hayumo(bora huu hakwenda wangekunjana na Kagame manake ameshamtukana na kumdhalilisha sana) na bahati mbaya hakuna kauli yoyote si kutoka kwa Membe wala Sitta mwenye Wizara, we have the right to know what's going on.
Jk ni mtu wa subira sana nadhani anapaswa kupata taarifa sahihi juu ya mtazamo wa kagame na wenzake hii ni pamoja na kujilizisha plani B yao walivyoiseti.
 
Hakuna kampuni ya bima,supermarket,bank,toka tanzania inayofanya biashara kenya ila za wakenya zimejaa tanzania.Ni bora tujitoe
 
we must be united, for this case of that madman kagame, we selukamba mwambie mjomba wako kagame akome kabisa.
 
Hakuna kampuni ya bima,supermarket,bank,toka tanzania inayofanya biashara kenya ila za wakenya zimejaa tanzania.Ni bora tujitoe

Usiwalaumu waKenya kwa uzembe na upuuzi wenu watanzania. This is free market era, kama hutimizi wajibu, kama hauko aggressive hakuna wa kukuonea huruma. Nyie endeleeni kutembeza mabakuli kwa wazungu badala ya kujenga uchumi na kuimarisha biashara na majirani zenu.

Tena Tz ikojitoa itakuwa imewasaidia sana majirani maana inawatesa mno, majirani zenu wanateseka sana kwa kututegemea sisi. Bandari dhaifu, reli hakuna na hivyo wanajikuta wakitumia gharama kubwa sana kufanya biashara pasipo na ulazima. Tunawasababishia bei kubwa za bidhaa kwa upuuzi wetu wa kushindwa kuwekeza kwenye reli na bandari. Hawaoni haja ya kuwa na jirani dhaifu, hakusaidii wakati wa raha, hakusaidii wakati wa shida. Kwa Rwanda, Burundi, Kongo, Zambia, Malawi wanaona Tanzania kama jirani dhaifu anayeshindwa kutumia fursa Mungu alizompa. Ukijitoa kwenye ushirikiano nao watashirikiana na nchi zingine na mambo yao yataenda. Timiza kwanza wajibu wako ndio uanze kulaumu majirani zako.
 
toa tanganyika..wacah kutusemea sisi wzanzibari... hatuwapendi vichogo kamanini.. wacha kusema kwa behalf zetu... toa tanganyika yako sio tanzania
Unafikiri sie tuna muda na watu wavivu kama nyie?Kwanza mnatupa faida gani ktk huu muungano zaidi ya kutunyonya tu!Hata mkitaka kuondoka leo..kwaherini wanyonyaji na wabaguzi wakubwa nyie.
 
umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Tanzania ni mwenda pole, na mwenda pole hajikwai. Hoja yako haina mashiko kwa sababu wewe hauko mipakani mwa tanzania. Umoja wa afrika ya mashariki ya sasa, umeundwa kwa mkataba mgumu sio rahisi kuuvunja vile wewe unavyotaka, siku zote tanzania inatumia diplomasia zaidi na sio kukurupuka. Chadema inatokea wapi hapa ama unataka kukidhalilisha kwa mambo ya kukurupuka unapoandika uzi huu? Tunapozungumzia mambo ya nnje ya mipaka yetu tunazunguza kama nchi kwa ujumla na sio chama. Mwisho : Vunja kwanza ndoa yako, na mahusiano na familia yako, ndipo uje na uzi wakuvunja eac. Pia kumbuka waziri husika wa eac ni samwel sitta, na wala sio bernard membe.

well said!
 
Ni kweli umoja ni guvu, utengano ni udhaifu...lakini kumbuka wameshaanza kututenga kijiichake. pili, kuna aina mbali mbali za umoja, kuna umoja unaondwa kuangamiza wengine na kuna umoja unaoundwa kuokoa wote.. kumbuka Tanzania imejengwa kwa misingi ya ujamaa, pia Umoja na Amani.. na katika harakati zote tokea uhuru Tanzania imepinga uonevu iweje leo tukubali kuonewa tena hadharani. hamna haja ya kuwa na umoja usio na faida, ndio maana nikasema haki na uoja wetu tuelekeze katika Umoja wa Afrika.. ngoja nikupe mfano.. wewe unaedai wa mpakani.. mfano Uganda ikadai kagera ni yao utaipeleka kesi EAC.. hapo utaliwa maana wanaushirika wao.. Kenya ikisema Rombo ni yao utapeleka Kesi EAC.. kwa kura itakula kwako lakini ukiipeleka AU hai itapatikana zaidi..
Chadema ni chama changu Tanzania ni nchi yangu... tatizo lako ni uelewa finyu wa demokrasia. na chadema kama ilivyo ccm , cuf , tlp ncccr tunawajibu wa kujenga nchi sio chama...
namuheshimu sana MH sitta , sijamtaja maana, ukiuwa EAC na wizara yake inakwenda na maji ndio maana sijamtaja.. pia angalia hii wizara na michango kwenye huu umoja, na pia wizara ni kubebesha wa TZ mzigo wa kodi.. nimetaja Nimemtaja Membe maana hiyo wizara ya Sitta ingefaa kuwa dawati kwenye ofisi ya Mambo ya njee..
hii haitakuwa mara ya kwanza EAC kuvunjika, hivyo ya pili sitashangaa...
mwisho asante sana, mimi nitamchumbia dada yako, nitamuoa , utakuwa shemeji yangu na kisha nitajenga nitaijenga nchi ya Afrika, ndoto ya wapigania uhuru, ndoto watumwa.. Ubarikiwe Mheshimiwa

Nina wasiwasi mwenye uelewa finyu ni wewe mkuu.
 
Kwanza kabisa Ndugu KIJANA wa CHADEMA -- TANZANIA hata siku MOJA haijawa kuwa MWANACHAMA wa ECOWAS (ECOWAS ni Muungano wa KIUCHUMI wa NCHI za Afrika Magharibi eg NIGERIA; GHANA etc) kwahiyo haitawezekana

Pili;Tanzania pia ni Wanachama WA SADCC sio lazima wakimbilie UMOJA wa AFICA 9AU)

Tatu: POLITICS ni DIPLOMACY... Sasa kama Rais wetu hata weza kumjibu Rais wa nchi yoyote KIDIPLOMASIA kuhusu issue yoyote iwe ya KISIASA; KIBIASHARA; KIUCHUMI; KIUTAWALA then atakuwa na Mapungufu... Sababu ukimya huo utadhihirisha jinsi UONGOZI wetu ULIVYO na DOSARI; UNYONGE; UFINYU wa MAELEWA

Nne; Kumbuka kuwa - VITA vya UGANDA kiongozi wa NCHI ya TANZANIA hakuwa huyu wa Sasa yaani Jakaya Kikwete; Tulikuwa na Uongozi Bora Shupavu wenye kujua Diplomasia - Kwahiyo Usilinganisha Madaraka ya Ungwe Moja na Ungwe Nyingine na kusema ni kitu kimoja...

Kuhusu Usuluhishi wa HALI huko KENYA; Kulikuwa na sababu mbalimbali ambazo lazima AMANI lazima ingejadiliwa na kukubaliwa; Sababu ya viongozi hao kufikia MWISHO wa Masuala yao.

Kama ni RAIS wa TAIFA na MPENDA AMANI ni FURSA kujibu chochote NCHI zinazoonyesha kutokuwa na IMANI na NCHI yetu kujibiwa KIDIPLOMASIA... As you know by what is going in this WORLD - ALL WAR REPRESENTS A FAILURE OF DIPLOMACY
tunaruhusiwa kuwa na mitazamo tofauti na hii ndio democrasia.
napingana na wewe kuanzia mstari wa kwanza hadi wa mwisho.diplomasia ni fani(weledi) ambao sio kila mwanadamu amejaliwa. ila kwa J.K nadhani kiwango chake cha diplomasia kiko juu kuliko yeyote kati ya waliopita na ni wa kipekee katika historia ya africa.
huenda mkaona ninampamba lakini kama ni mwanahistoria mzuri wa bara la africa utaniunga mkono katika hili.
labda nikupe mfano kidogo wa kipindi cha nyerere, wakati wa mgogoro baina ya nyerere/idi amin(uganda VS tanzania) IDDI AMIN alikuwa anaongea saaana na kutoa vitisho mithili ya anavyofanya KAGAME hivi sasa.
mwalimu nyerere hakuwa anamjibu IDI AMIN, ila majibu yake yalikuja kwa vitendo na wote tunafahamu nini ulikuwa mwisho wa idi amin. mtakapotaka JK awe anajibu kila linaloelekezwa kwake!!!! mtataka awe anawajibu hata wendawazimu(triple K wote ni wendawazimu na wauaji) na anachokifanya hivi sasa ni kuwaonyesha kuwa ''HE IS OF THE NEXT LEVEL'' unapoongelea uongozi na busara. ukimya hutoa mshindo kuliko kelele unazozitaka.

kuhusu ushupavu wa kiongozi na ushindi vitani,, labda nianze kwa kukuuliza umri wako. huenda vita vya uganda ukawa haujui vilipiganwa vipi na ushindi ulipatikanaje.. kwa kukupa ukweli ni kwamba'' kama uganda ingekuwa haina mgawanyiko mkubwa na vikundi mbalimbali kuwepo msituni vikipigana dhidi ya IDI AMIN, ile vita ya kagera ingekuwa na matokeo tofauti na wala nyerere asingethubutu kuingia vitani na uganda ambayo haina mgawanyiko. take it from me brother, vikundi vya wapiganaji wa msituni (museven na kagame miongoni mwao) vilitoa mchango mkubwa sana katika ushindi wa vita ile na ndio maana MUSEVEN anamuona nyerere kama mungu wa pili.
uganda leo hii imegawanyika kuliko kipindi cha idi amin
rwanda ya leo imegawanyika kuliko kipindi chochote katika historia yake
wajaluo wa kenya wana kilio cha ndani kwa ndani dhidi ya wakikuyu na jambazi kenyata
hata sisi hatuko pamoja kama tulivyokuwa kipindi cha nyerere lakini tuna unafuu mkubwa maana''HATA KAMA TUNATOFAUTIANA KIITIKADI ZA VYAMA lakini mwisho wa siku tunakunywa na kula pamoja, tunauguzana pamoja, tunalia na kucheka pamoja, tunahuzunika na kufurahi pamoja, tunazikana NA MWISHO WA SIKU TUNABISHANA BILA KUPIGANA.
huwezi kupata chemistry kama inayopatikana hapa tanzania kokote miongoni mwa majirani zetu.
namuunga mkono JK na hii inaonyesha jinsi alivyo jasiri na mwanadiplomasia wa kweli ukilinganisha na wendawazimu waliomzunguka
 
toa tanganyika..wacah kutusemea sisi wzanzibari... hatuwapendi vichogo kamanini.. wacha kusema kwa behalf zetu... toa tanganyika yako sio tanzania

mimi sijazaliwa tanganyika wala sijazaliwa zanzibar,...nimezaliwa Tanzania hivyo naongelea TZ acha fikra za kizamani
 
Wazo kuu la Jumuia yoyote ile ni kukubaliana ktk kutokukubaliana! Kwa nini tujitoe? Kama tofauti ndogo ndogo zitaruhusiwa kuwa sababu ya kujitoa tunaweza kujikuta tukijitoa kwenye Jumuia zote ambako ni Wanachama. EAC tunaihitaji kama yenyewe inavyotuhitaji. Kama kuna matatizo/migogoro/kutoelewana nk ni vizuri tukaitafutia ufumbuzi tukiwa ndani kuliko tukiwa nje.
 
toa tanganyika..wacah kutusemea sisi wzanzibari... hatuwapendi vichogo kamanini.. wacha kusema kwa behalf zetu... toa tanganyika yako sio tanzania

Hoja hii haikustahili mchango kama uliotoa. Hoja imetolewa kiuwazi wewe unaijumuisha na utanganyika uzanzibar. Tujadiliane ili tuelimishane na kujengana kwa ufahamu.
 
Wazo kuu la Jumuia yoyote ile ni kukubaliana ktk kutokukubaliana! Kwa nini tujitoe? Kama tofauti ndogo ndogo zitaruhusiwa kuwa sababu ya kujitoa tunaweza kujikuta tukijitoa kwenye Jumuia zote ambako ni Wanachama. EAC tunaihitaji kama yenyewe inavyotuhitaji. Kama kuna matatizo/migogoro/kutoelewana nk ni vizuri tukaitafutia ufumbuzi tukiwa ndani kuliko tukiwa nje.

Asante sana Fanto wazo kuu la jumuiya yoyote ni "kukubaliana katika kutokukubalina!" Naipenda sana hii, wenzetu wangelielewa hili wala isingekuwa nongwa .. tatizo wao hawalielewi hili.. hivyo wao ndio wanakuwa wameuvunja muungano.. Kikwete aliposhauri wao waongee na waasi wangetakiwa "kukubaliana katika kutokukubalina!". sasa wao wanapojitenga inamaanisha nini no fair play..ni kweli kabisa ni vizuri sana kutafuta ufumbuzi tukiwa ndani ya jumuiya kuliko kutokuwa njee ya Jumuiya hilo nakubaliana na wewe kabisa kumbuka kuwa ndani au nje ya jumuiya zote ni njia za kimkakati.. nadhani tutaheshimiana zaidi na majirani pindi tutakapokubaliana katika kutokukubaliana..yani tukikeep distance.. ukweli ushirikiano ni lazima na muhimu kwa majirani lakini heshima na uhuru.. ndio kile kitu kagame alisema kuvuka mipaka.. sasa ni wakati wa sisi kuwaambia huu ushirkiano basi.. maana hautufikishi kwenye lengo la kuwa nchi mmoja na hamna nia ya kweli katika malengo yaliyowekwa katika EAC .. hivyo ni vyema tukaondoka kwenye EAc tubaki tukiheshimiana kama majirani.. ili wawe na uhuru zaidi wa kufanya vikao vyao vya kienyeji.. hoja yangu ni kuwa kuna kila dalili kuwa malengo ya EAC hayatafikiwa na madhumuni ya ushirkiano huu na umuhimu wake unnakosa mshiko kwasababu hamna nia na dhamira ya kweli katika wanachama wake. Hivyo wajiondoe mapema kuliko kusubiri wakati wa majeruhiii.. hasara itakuwa kubwa sana.
Asante sana Kwa mchango wako
 
Last edited by a moderator:
Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu. Tanzania ni mwenda pole, na mwenda pole hajikwai. Hoja yako haina mashiko kwa sababu wewe hauko mipakani mwa Tanzania. Umoja wa Afrika ya Mashariki ya sasa, umeundwa kwa mkataba mgumu sio rahisi kuuvunja vile wewe unavyotaka, Siku zote Tanzania inatumia diplomasia zaidi na sio kukurupuka. Chadema inatokea wapi hapa ama unataka kukidhalilisha kwa mambo ya kukurupuka unapoandika uzi huu? Tunapozungumzia mambo ya nnje ya mipaka yetu tunazunguza kama nchi kwa ujumla na sio chama. Mwisho : vunja kwanza ndoa yako, na mahusiano na familia yako, ndipo uje na uzi wakuvunja eac. Pia kumbuka waziri husika wa Eac ni Samwel Sitta, na wala sio Bernard Membe.

Yaani badala ya kujadili wazo lake zuri hivi wewe ume-critisize hoja. Wewe ndio huna uzalendo ondoa utumbo wako hapa
 
Kwanza kabisa Ndugu KIJANA wa CHADEMA -- TANZANIA hata siku MOJA haijawa kuwa MWANACHAMA wa ECOWAS (ECOWAS ni Muungano wa KIUCHUMI wa NCHI za Afrika Magharibi eg NIGERIA; GHANA etc) kwahiyo haitawezekana

Pili;Tanzania pia ni Wanachama WA SADCC sio lazima wakimbilie UMOJA wa AFICA 9AU)

Tatu: POLITICS ni DIPLOMACY... Sasa kama Rais wetu hata weza kumjibu Rais wa nchi yoyote KIDIPLOMASIA kuhusu issue yoyote iwe ya KISIASA; KIBIASHARA; KIUCHUMI; KIUTAWALA then atakuwa na Mapungufu... Sababu ukimya huo utadhihirisha jinsi UONGOZI wetu ULIVYO na DOSARI; UNYONGE; UFINYU wa MAELEWA

Nne; Kumbuka kuwa - VITA vya UGANDA kiongozi wa NCHI ya TANZANIA hakuwa huyu wa Sasa yaani Jakaya Kikwete; Tulikuwa na Uongozi Bora Shupavu wenye kujua Diplomasia - Kwahiyo Usilinganisha Madaraka ya Ungwe Moja na Ungwe Nyingine na kusema ni kitu kimoja...

Kuhusu Usuluhishi wa HALI huko KENYA; Kulikuwa na sababu mbalimbali ambazo lazima AMANI lazima ingejadiliwa na kukubaliwa; Sababu ya viongozi hao kufikia MWISHO wa Masuala yao.

Kama ni RAIS wa TAIFA na MPENDA AMANI ni FURSA kujibu chochote NCHI zinazoonyesha kutokuwa na IMANI na NCHI yetu kujibiwa KIDIPLOMASIA... As you know by what is going in this WORLD - ALL WAR REPRESENTS A FAILURE OF DIPLOMACY

Ndugu ww ndie ulokurupuka baada ya kuona kakosea alikiri kosa akaandika COMESA, af sijui na ww uko ulimwengu gani? coz saiz hyo SADCC tuliisahau kitambo ss tuna SADC
 
toa tanganyika..wacah kutusemea sisi wzanzibari... hatuwapendi vichogo kamanini.. wacha kusema kwa behalf zetu... toa tanganyika yako sio tanzania

Wewe kama si Mungiki au Konyi basi utakuwa M23. Tanganyika au Zanzibar hatubabaishi lugha yetu. Subiri na nyie kiwake kuhusu visiwa vya MIGINGO
 
Back
Top Bottom