Mh.mbunge Jeremiah Sumari wa Arumeru mashariki-CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh.mbunge Jeremiah Sumari wa Arumeru mashariki-CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wizzo, Nov 13, 2011.

 1. Wizzo

  Wizzo JF-Expert Member

  #1
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  wadau huyu mbunge hata hajaapishwa toka uchaguzi uishe yupo kitandani ni mgonjwa sana hivyo hatuna mwakilishi jimboni kwetu,je selikari inaonaje kama tukifanya uchaguzi mwingine tutafute muwakilishi mwingine? Sumari abaki mbunge wa viti maalum.
   
 2. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #2
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,380
  Likes Received: 3,339
  Trophy Points: 280
  Serikali inaogopa chadema watalichukua hilo jimbo maaana hata sumari alichakachu.
   
 3. Nduka Original

  Nduka Original JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2011
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 753
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yuko hospitali au yuko nyumbani?
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  nadhani kuna sheria za mtu kukosekana kituo cha kazi kwa muda fulani

  labda wanachi wa jimbo wafungue shitaka au shauri
   
 5. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #5
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,320
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  Sijui wananchi wa jimbo hilo wanawakilishwa vipi Bungeni, pia serikali wanaogopa hilo jimbo limepakana na Bengazi huenda imeshaambukizwa harakati za ukombazi. Pamoja na hayo hilo jimbo ccm itawatoka tu hata wachelewesheje inachukuliwa na peoples power
   
 6. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #6
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ukikosa mikutano(vikao) vitatu mfululizo utakuwa ushajifukuzisha,Na huyo mb kakosa vikao vi4 kwa hyo ipo wazi wananchi kuchukua hatua coz hawana muwakilishi wao
   
 7. p

  politiki JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  hili ni swala la kikatiba zaidi kuliko hiyari kwa maana katiba yetu aisemi endapo mbunge atashindwa kuwatumikia wananchi kwa sababu za kiafya
  basi nini kitokee na kwa muda gani Tume isubiri kabla ya kuitisha uchaguzi mwingine. kwahiyo ili swala ni lazima liwekwe wazi kwenye katiba ijayo
  na kuliondoa kabisa kwenye hiyari ya mtu kwa maana this is public business kama huna uwezo wa kufanya mwachie mtu mwingine aifanye.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ukikosa vikao bila na kuwa na sababu ya nmsingi. Kuugua nadhani ni swababub ya msingi. lakini technically, yeye hajala kiapo, hivyo kuna uwezekano kuwa habanwi na hizo kanuni kwa sabbau hawaja mbunge rasmi
   
 9. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2011
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Is this an open end situation? Ina maana busara haitumiki kwa huyu mbunge ku step down kama hali ya afya haimruhusu kuendelea kuifanya kazi yake?
   
 10. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #10
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wananchi wa Arumeru ni kama hawana mbunge kabisa, mtu hadi leo hajaapishwa mnategemea nini? Kazi kuiandama CDM kwa vurugu kuwa majimbo yao yatakosa maendeleo kwa wawakilishi wao kuendekeza vurugu sasa kwa hili jimbo lisilo na muwakilishi ni nani atawasemea wananchi hao?
  Mimi naona kuna haja ya kuomba muongozo wa jambo hilo kwa spika.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,561
  Likes Received: 18,292
  Trophy Points: 280
  Wizzo, sio kweli kuwa Mbunge, Mhe. Jerry Solomon, hakuapishwa, siku wabunge wanaapishwa, nilikuwepo Dodoma, nilimshuhudia kwa macho yangu mwenyewe!.

  Hili la kuugua, ni ubinadamu.

  Nawaombeni wana jf wenzangu, wakati mwingine tuweke utu mbele, thamani ya mtu ni utu, ubinaadamu ndio unatangulia na mengine yote yanafuatia, ndio maana moyoni mwangu, nafsi yangu ilimlilia hata Saadam, Osama na juzijuzi Gadhafi, licha ya yoye waliyoyafanya. Damu ya binadamu ni ile ile kwa wote, nikimaanisha damu ya Ghadafi iliyeuwawa kinyama ni sawa na Damu ya Obama au ya Baba Mtakatifu!. Hivyo nawaombeni sana tusimbeze yoyote kutokana na maradhi/kuugua, tuweke ubinaadamu mbele.

  Pasco
   
 12. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #12
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Pasco nashukuru sana kwa majibu mazuri yenye uhakika kuwa mbunge yule kaapishwa, binafsi nilikuwa najua hajaapishwa bado.
  Lakini pamoja na majibu mazuri naomba tujadili sheria inasemaje katika matukio kama hayo badala ya kubaki kumuonea huruma mtu jambo ambalo ni ubinadamu kwa binadamu yoyote mwenye akili timamu.
  Sheria inasema ikiwa mtumishi wa serikali akiumwa miezi sita mfululizo kwa maana ya kuwepo na ushahidi wa ED basi kama hajapona anapaswa kulipwa nusu mshahara kuanzia hapo. Sijui sheria inasemaje kwa wabunge wetu. Mimi naomba tujikite hapo ili tuone sheria inasemaje na imetekelezwa?
  Na hii si kwake tu hata kwa kina Mwandosya na Mwakyembe tujue hatma zao endapo hali zao zitaendelea kwa muda mrefu kuwa hivyo zilivyo.
   
 13. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #13
  Nov 13, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Tumwombee apone aendelee kuwatumikia watu wake.
  Kwa wale wenye tamaa na majimbo kubaki wazi, sheria inaruhusu hadi miezi 24 kabla ya kulazimika kuziba nafasi hiyo iwapo Tume ya Uchaguzi itaona kuna haja ya kungojea kulingana na sababu zilizoleteleza jimbo kuwa wazi
   
 14. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #14
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nashukuru kwa ufafanuzi kakalende. Hebu tupe mazingira ambayo NEC inapaswa kujiridhisha kabla ya kuchukua maamuzi au kama yameegemea kwenye utashi wa mwenyekiti wa NEC?
   
 15. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #15
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Kuwa na ubinadamu ni wito
   
 16. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #16
  Nov 13, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,636
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ccm hawana wito huo!
   
 17. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #17
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  ni mwongozo wa katiba, sheria ya uchaguzi na kanuni za uwakilishi na sio utashi wa serikali

  kwa kipindi chote na dalili za kutopata nafuu karibuni mhe. sumari angewatendea haki wana-arumeru kwa kuacha nafasi wazi hata kama kuna hofu kubwa ya chama chao kulipoteza jimbo
   
 18. only83

  only83 JF-Expert Member

  #18
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Mkuu hapo kwenye red umenivunja mbavu ile mbaya....kwa hiyo Arusha ni aka Bengazi ha ha ha ha ha ha!! good idea!!!
   
 19. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #19
  Nov 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,482
  Likes Received: 12,753
  Trophy Points: 280
  Hivi anaugua kitu gani? Anaulazima gani
  wa kuendelea kuwa mbunge wakati hajiwezi wala hawezi kutumikia wananji wa jimbo lake? Analipwa posho kwa kazi gani haswa?kwa nini ccm wamekaa kimya tu,ama anataka kwenda india kwa ngongo wa ccm nini ?lo
   
 20. G

  Godfrey GODI Member

  #20
  Nov 13, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 62
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pasco, suala hapa si kuapishwa au kutokuapishwa. Mantiki ni je mbuge huyo anafanya kazi za kibunge kama alivyochaguliwa na wananchi? Sheria zinasema nini juu ya mbunge aliye mgonjwa kwa muda mrefu? Kama sheria imedokeza na watekelezaji wa sheria hawataki kuzitekeleza, basi huko ni kuwanyima wananchi uwakilishi. Lakini kama hakuna kipengele chochote kinachomtaka mbunge ajiuzulu endapo ataugua kwa muda mrefu, basi hayo ni mapungufu yaliyomo katika sheria zetu na hususani katiba. Katiba mpya inaweza kuja, tuwasilishe mapungufu hayo.
   
Loading...