Nawapongeza wana Biharamulo kwa ushindi huu. Na ninashukuru Jaji ametenda haki. Ktk nchi hii kwa Tume yetu ya Uchaguzi mpaka mpinzani atangazwe mshindi anakuwa ni mshindi kweli. Wapiga kura wanakua wamepambana na uchakachuaji na wizi wa kura mpaka chaguo lao atangazwe mshindi! Ingawa sisi Wakristo tunaambiwa tusamehe,lakini sitamsamehe jaji aliyehukumu kesi ya Godbless Lema hata kama ni mhaya mwenzangu. Ilikua hukumu ya kihuni na kijuha! Lakini niseme ndani ya CCM,hao jamaa hawana aibu wala woga hata kwa Mungu! Ushenzi na umafia CCM iliofanya 2010 kulazimisha ushindi Arusha Mjini hawakuwa na hudhu wala haki ya kufungua kesi ya kulalamikia matokeo yale!!! Kama bado kungekuwa bado kuna watu huko wenye busara wangezuia hiyo kesi. Kwasababu ilikua ni kuwachokoza wapiga kura wa Arusha ambako chama chochote makini hakiwezi jiingiza ktk ujinga kama huo!