Egwugu
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,558
- 8,553
Mh. hongera sana, sielewi kama unaelewa msingi wa pongezi zangu. Ninamaanisha, hawamu hii ya tano mmeweza kuelewa kwamba mkoa wa Kagera na watendaji wa serikali ni "mizigo", wababaishaji, wazembe, wezi n.k .. Kimsingi si waadirifu hata kidogo.
Na naona hili umeweza kulibaini vizuri sana na hii inatokana na safari ambazo umeshazifanya katika mkoa huu, nadhani hii ni mara ya nne kama sikosei na kila ukirudi mambo ni yale yale. Nakusihi mh. Waziri mkuu, tumbua. Kuna watu manunda, hayasikii mvua wala jua, hebu fanya kuwaweka benchi kwanza wakuu kadhaa wa Idara hasa hasa hapa manispaa.
Mie nakusihi tu, kwamba najua unakereka sana na aina ya viongozi eneo hili, usipate kigugumizi kuwafyekelea ziwani. Wanafanya vile eti kisa ni mbali na Dar/Dom na kwasababu huu mkoa uko pembezoni kabisa na kwamba hata media zingine hazifiki kama maeneo ya karibu na Ikulu
Ondoka na vichwa kadhaa mh