Mh. Mabumba, Mh. Manyanya & Mh. Mwigulu, Msituharibie CCM yetu!

[/COLOR]Hapo kwenye red ndo mtoa mada nakushauri yafuatayo.
CCM ilifanya kosa kubwa sana la kukubali kuvamiwa na maharamia wa siasa, ivi ni nani aliruhusu mahalamia kwenye chama chetu? Ni Mkapa au Kikwete? wewe mtoa mda nakuona una uchungu na chama chetu lakini maharamia ambao inabidi watekereze hayo uliyowashauri hawana uchungu wowote maana hayawagusi,wanatumia chama chetu CCM kama chombo tu cha kufanikishia huo uharamia wao. Ivi huyo Stella Manyanya au Mwigulu chemba si wanakaa karibu na maharamia kama ADEN RAGE, ABOOD unategemea nini toka kwa hao?

Mkuu tuaiangalie upumbavu kafanya nani tukubali kuwa tulikosea na tuanze kurekebisha sasa, Haya mambo ya kusimamia misimamo duni ni upumbavu! tukubali tumekosea tujirekebishe na si kwa kuwafukuza watu uanachama bali kwa kuonyana na kurekebishana!
 
Kuna vitu vingi kwa mda mrefu vimekuwa haviendi sawa ndani ya chama chet, kwanza nakubali kuwa mimi ni mwanachama cha mapinduzi kwa sababu bado sijarudisha kadi yenu, kuna mambo kadhaa nataka chama kijue.

Migomo inayoendelea nchini chama kinafanya kosa kubwa sana kuhusianisha na magwanda, Nimemsikia mbunge Eng stalla akisema mgomo umesababishwa na chadema, Ni kweli inawezekana lakini tukumbuke;

a) mgomo wa vyuo tulisema chadema
b) Waalimu tulisema chadema
c) Wakulima waliandamana Tulisema chadema
d) kwenye migodi waliuawa tulisema CDM
e) Madaktari tunasema chadema
f) Wafanya kazi tutasema chadema
g) Ulimboka tunasema kapigwa na chadema

Hayo hapo juu ni baadhi tuu na husemwa na wabunge wa ccm bungeni! Nchemba anaunga mkono hoja ni nikijana msomi tunaemtegemea.

Kama hayo yoote yanasababishwa na CDM je sisi tunamtetea nani, tunajenga chuki ya bure.

Kumbukeni woote wanakuwa wamepatwa na matatizo na niwananchi wetu kwa nini tushindwe kuwasikiliza badala yake tunatumia nguvu na kuweka lawama kwa wapinzani!? Kumbukeni ccm tunajeshi na vyombo vyote vya usalama tunashindwa vipi kubaini haya maovu? chadema wanazidi kukubalika nchini pamoja na kuwapa kashfa zote hizi!

MNAWAPA WENYEWE UMAARUFU AMBAO HAWASTAHILI KUPEWA!

USHAURI WANGU
1. Tuache kuhusianisha migomo na chadema tutazidi kujizika
2. Raisi arudi tena kuongea na ma dr ni watoto wake huwezi kuwakimbia, hili HALIKIMBILIKI MR RAISI
3. Wanaofanya unyama wakupiga watu wakamatwe haraka.
4. Wabunge woote wajadili mambo ya nchi zaidi na si ushabiki wa vyama.
6. Ikiwezekana waite wapinzani kwa siri wakupe ushauri wao
7. Tufanye juhudi za kutimiza ahadi zetu badala ya kuweka majungu na watoto kama Mnyika na Sugu.

Plz Chama changu yafanyeni haya tunaweza kupona

Ni ushauri mzuri sana wasiwasi wangu ni hawa jamaa zako CCM wanamasikio ya kusikia? Au ndo sikio la kufa halisikii dawa? Hebu tungoje tuone kama wataufuata huu ushauri wako mzuri sana.
 
Ni ushauri mzuri sana wasiwasi wangu ni hawa jamaa zako CCM wanamasikio ya kusikia? Au ndo sikio la kufa halisikii dawa? Hebu tungoje tuone kama wataufuata huu ushauri wako mzuri sana.

mkuu tuwashauri tuu hata kama chama kitakufa wajue wao ndo chanzo kikubwa cha kuua chama!
 
Kuna vitu vingi kwa mda mrefu vimekuwa haviendi sawa ndani ya chama chet, kwanza nakubali kuwa mimi ni mwanachama cha mapinduzi kwa sababu bado sijarudisha kadi yenu, kuna mambo kadhaa nataka chama kijue.

Migomo inayoendelea nchini chama kinafanya kosa kubwa sana kuhusianisha na magwanda, Nimemsikia mbunge Eng stalla akisema mgomo umesababishwa na chadema, Ni kweli inawezekana lakini tukumbuke;

a) mgomo wa vyuo tulisema chadema
b) Waalimu tulisema chadema
c) Wakulima waliandamana Tulisema chadema
d) kwenye migodi waliuawa tulisema CDM
e) Madaktari tunasema chadema
f) Wafanya kazi tutasema chadema
g) Ulimboka tunasema kapigwa na chadema

Hayo hapo juu ni baadhi tuu na husemwa na wabunge wa ccm bungeni! Nchemba anaunga mkono hoja ni nikijana msomi tunaemtegemea.

Kama hayo yoote yanasababishwa na CDM je sisi tunamtetea nani, tunajenga chuki ya bure.

Kumbukeni woote wanakuwa wamepatwa na matatizo na niwananchi wetu kwa nini tushindwe kuwasikiliza badala yake tunatumia nguvu na kuweka lawama kwa wapinzani!? Kumbukeni ccm tunajeshi na vyombo vyote vya usalama tunashindwa vipi kubaini haya maovu? chadema wanazidi kukubalika nchini pamoja na kuwapa kashfa zote hizi!

MNAWAPA WENYEWE UMAARUFU AMBAO HAWASTAHILI KUPEWA!

USHAURI WANGU
1. Tuache kuhusianisha migomo na chadema tutazidi kujizika
2. Raisi arudi tena kuongea na ma dr ni watoto wake huwezi kuwakimbia, hili HALIKIMBILIKI MR RAISI
3. Wanaofanya unyama wakupiga watu wakamatwe haraka.
4. Wabunge woote wajadili mambo ya nchi zaidi na si ushabiki wa vyama.
6. Ikiwezekana waite wapinzani kwa siri wakupe ushauri wao
7. Tufanye juhudi za kutimiza ahadi zetu badala ya kuweka majungu na watoto kama Mnyika na Sugu.

Plz Chama changu yafanyeni haya tunaweza kupona

ushauri wako ni mzuri mno...ila ni kosa kubwa sana kwa rais wetu kumpa cheo mtu kama STELLA MANYA NYA ambaye aliongea uchuzi wa aina yake jana bungeni....haileti tija hata kidogo ...ccm bado itaonekana imechanganyikiwa ,imedodda,haina jipya ,ni danguro,ni mfu,haisikii,ipo ipo tu bora liende ,imekata tamaa,walafi ,.hawana jipya kama style ya manyanya itaendelea kuongoza hii nchi .Kwa watu wenye hekima kama zangu mtu kama manyanya asingeongoza mkoa kwa maneno ya jana.Na kama ingekuwa mpinzani ndo aliyasema hayo hooooooo yangemkuta ...hii ndo ccm bwana miaka 50 ya uhuru......inasikitisha pamoja na ushauri huu ,,bado kazi ipo kama bado tunaongozwa na watu style ya MANYANYA......
 
Ni kweli ni sauti ya mtu aliye nyikani,mtu ambaye anajadili na kuusema ukweli ambao ni kitu hadimu katika chama hiki kikongwe kinachokufa. Mabumba na Mwigulu,jana haikua mara ya kwanza kusababisha malumbano ya kijinga,lakini inaonyesha hakuna watu wa kuwakemea ktk chama chao. Wote ni wabunge wanaotoka ktk majimbo masikini lakini badala ya kuwatetea wananchi wao,wanajipendekeza kwa wakuu wa chama na watawala.
Sauti ya mtu aliaye nyikani..........Hivi kuna anayesikiliza huko kunakohusika?:israel:
 
hatumsemi vibaya mkuu tunataka anusulu chama kisife kabisaa, ionekana kuna watu tunajali bado!

mbona una ogopa bila sababu
jk ni malaika?
Aliyetaka jk hasisemwe kafa yeye!

Ccm hamna jipya hivi,kila kitu cdm!
 
Sijui kama watakusikia umeongea mambo mengi yenye ukweli na uzalendo ,huyo Mabumba nilikuwa naye New Southern Hampshire University-CED program namshangaa alivyogeuka kuwa mwehu
 
mwigulu chemba ni tatizo namba 1,na ndie anamshauri vibaya rais wakati uwezo wake ni mdogo
 
Nadhani hapo ni kama kumshauri mbuzi akuvushe barabara!

Na kushauri usiangaike na hicho chama kimesha jifia!

Juzi ametoa hotuba kasimama, usishangae hotuba ijayo kuitoalea msituni, usiulize msitu gani.

Yaan damu yamtu ina changanya sana.
 
Kuna kiongozi wajuu wa ccm aliwahi kusikika akisema,{ UKITAKA MAMBO YAKO YAWE MAZURI NJOO CCM}hapa ndipo maharamia walipo jipenyeza ndani ya ccm.Na walijipenyeza kwakuwa kauri hii haikuchuja nani waingie ccm ili mambo yao yawe mazuri
 
Ni siku nyingine tena, mwenzetu Mh. Mabumba alipokuwa amekalia kiti cha Bunge alijitelezesha na kujiingiza katika tope lililomchafua na baadaye akashindwa kutoka humo hadi watani zetu wakaanza kutucheka na mbaya zaidi wananchi tunaowategemea wanaanza kutuona kuwa sisi hatuna watu makini na kwamba pengine tupo si kwa ajili ya haki na maendeleo yao.

Mh. Mabumba: Hivi ulipomwambia Mh. Mnyika kuwa ‘anawashwa, akae chini’ ulimaanisha nini na ulitumia kanuni ipi kuachilia tusi hilo na kwa faida ya nani. Unafikiri kuwa CCM tunapata sifa kwa kutoa matusi au kujibu kwa matusi Wapinzani wakati umepewa dhamana ya kuongoza kikao cha juu sana katika nchi- cha muhimili wa Taifa? Yaani mwangwi wa sauti yako ya “Kaa chini!!... cheap popularity !!....” imekuexpose kuwa huwezi kuongoza vikao vya namna hiyo wala ku-controll heated debates. A Moderator will never dream to be defamatory.

Mh. Eng. Manyanya: Ulianza vyema kumpa pole Dr. Ulimboka na pia si vibaya ulipoonyesha masikitiko ya Wananchi kukoswa huduma muhimu za Afya tokana na mgomo. Lakini imeshangaza ulimwengu, kwa heshima uliyonayo kama Msomi, Mbunge na Mkuu wa Mkoa kujiingiza katika kauli tata na za mipasho hadharani.
Ni kitu gani kilikupeleka uendelee hadi kufikia kutamka waziwazi ndani ya Bunge hitimisho kuwa CHADEMA wanahusika katika kumteka na kumjeruhi Dr. Ulimboka? Ukasema kwamba wao ndio wenye magandwa kama wale waliomteka Daktari. Aidha ulijisukumiza katika shimo hatari kwa kuanza kumbeza Dr. Ulimboka aliye katika matibabu ya kuokoa maisha yake kwa kumfananisha hadharani na Muuaji Hitler; Eng. what a scrawny analysis, fallacious, insalubrious talk & dodgy statements!

Injinia, je huwezi kufikiri kwa nini hata katika speech ya Rais, aliongelea mgomo usio halali lakini aliwaomba Madaktari warudi kazini na kuhusu Ulimboka alitoa kauli za kuagiza vyombo vya dola kuwatafuta wahusika (wawe ni wa CCM, CHADEMA, CUF au wasio na Chama sisi hatujui) na shauri hilo lifikishe mbele ya haki. Wewe unaanza kumhukumu mtu kama huyo aliyepona kuuawa na kumwita Muuaji katika hali aliyo nayo sasa kwa faida ya nani? Unafikiri kuwa wananchi wataipenda CCM zaidi kwa kuongea hivyo wakati wananchi wote wanalaani kwa namna yeyote mtu kutekwa na kupigwa au kuuwawa hata kama ana makosa maana kwa nini asifikishwe katika vyombo vya dola kama ana kesi ya kujibu?

Mh. Mwigulu:
Ulishashauriwa siku za nyumakuwa kwa level yako kama Mbunge na Kiongozi wa Kitaifa wa CCM (NEC – Uchumi & Fedha), kabla ya kuongea ebu tulia na kufikiri kidogo. Ile statement uliyo quote Bungeni ya Wapinzani wakisema “endeleeni kudai haki zenu sisi tunawaunga mkono”, huwezi kuitumia kuthibitisha kuwa CHADEMA wamehusika na tukio la kumteka Daktari wala kuongoza migomo isiyo halali! Hata mimi na wengi wetu wana CCM tunasema kuwa moja ya majukumu yetu ni kuwaunga mkono Wananchi kudai haki zao. Rejea Lengo namba 5 la CCM;
“Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii hifadhi ya masiha yake na mali yake kwa mujibu wa sheria” na “pia namba 7 ;
“Kusimamia haki na maendeleo ya Wakulima, Wafanyakazi na Wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea; na hasa kuona kuwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake.

Mh. Mwigulu, kwa utetezi au upingaji wa kauli hiyo tu, Wananchi wataweza kutofautisha kuwa ni nani yuko kwa ajili ya haki zao na ni yupi hayuko nao. Hakika mnasababisha watu kutuchukia na Chama chetu bila kujua maskini! Taarifa yako Bungeni leo tena haikuwa na mashiko. Sikilizeni, Kazi yetu CCM inatakiwa kuwa kusukuma kwa ushawishi Madaktari & Serikali kukutana na kutatua mgogoro uliopo. Pili, ni kuhakikisha kuwa yeyote aliyeshiriki jaribio la kumwondoa uhai Dr. Ulimboka anafikishwa mbele ya haki. Kama tuna madai juu ya Ulimboka tuyafaili afikishwe polisi na mahakamani ayajibu. Na kamwe iwe marufuku yeyote mwana CCM kushabikia dhuluma, vitisho, utekaji wa wananchi na kujichukulia sheria mkononi hata kama ana hatia. Anayebisha basi avuliwe uanachama wa CCM maana yu kinyume na lengo letu la CCM namba 16.

“Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna aina yoyote ya dhuluma, vitisho, ubaguzi , rushwa , uonevu na au upendeleo”. Halafu tuelewe kuwa kuwa na nia ya kusikiliza madai ya madakrari ni tofauti na kwamba yametekelezwa.

Nauliza hivi ni Madaktari wangapi leo hii wameshapewa hayo magari au hata kujaza fomu za mikataba hiyo nchini kote, waliokwisha pewa makazi, ambao wameshaanza kupokea hiyo allowance mpya wanazosema na mishahara ya juu wakati tunajua kuwa kuna Madaktari wengi sana kote nchini (hii si issue ya Muhimbili tu) ambao bado wana madai ya arrreas za mishahara yao ya toka mwaka jana!

Kwa nini mnapenda sana kumpa taarifa zisizo kamili Rais wetu eti yote kasoro mawili tu ndiyo yametekelezwa? Wabunge muitishe taarifa za ma- RMO's kama hawana madai ya Madaktari ya siku nyingi tena ya vile viwango vya zamani na hayajalipwa? Ndani ya CCM tupo wengi ambao hatuvumi lakini tupo. Msituharibie CCM yetu- Arhrhghh!!

Jueni kuwa CHADEMA wanapoona tunakubali kuvaa viatu walivyotuazima wanafurahi sana! Watch out our role & strategies are completely different:yawn:!

HAWA WOTE WANAJUSTFY POSHO TU. si tayari wameshavuta? unadhani watafanya nini,
kwa ukweli ulioueleza Mh. hebu tuambie tuna mpango wa kuendelea kweli. hawa ndiyo waheshimiwa wabunge tena wa chama tawala, ambao tulidhani wangekuwa kila wanaposimama tunesikia mawe ya kutisha kama bunge la OBAMA badalla yake tunasikia akina Mashauzi wa Bungeni, loo poleeniiiiiiiii..... mungu awalaani na awape yale mnayoyaoomba kwa wenzenu.
inatupa taabu sana kuelewa kwamba kundi kubwa la wabunge wa CCM lipo bungeni kwa ajili ya kusign Posho na si kuwawakilisha wanavijiji wao inasikitisha. sana sana
 
tatizo la ccm ni wagumu wa kufikiri wanafikiri hiki kizazi ni cha mwaka 47,ambacho kila walichokuwa wanawaambia wanaitikia ndo mzee(kwa wasukuma ndoho taabu),umewapa ushauri mzuri ila kwa ukiziwi wao umepoteza muda but good ujumbe umefika
 
ushauri wako ni mzuri mno...ila ni kosa kubwa sana kwa rais wetu kumpa cheo mtu kama STELLA MANYA NYA ambaye aliongea uchuzi wa aina yake jana bungeni....haileti tija hata kidogo ...ccm bado itaonekana imechanganyikiwa ,imedodda,haina jipya ,ni danguro,ni mfu,haisikii,ipo ipo tu bora liende ,imekata tamaa,walafi ,.hawana jipya kama style ya manyanya itaendelea kuongoza hii nchi .Kwa watu wenye hekima kama zangu mtu kama manyanya asingeongoza mkoa kwa maneno ya jana.Na kama ingekuwa mpinzani ndo aliyasema hayo hooooooo yangemkuta ...hii ndo ccm bwana miaka 50 ya uhuru......inasikitisha pamoja na ushauri huu ,,bado kazi ipo kama bado tunaongozwa na watu style ya MANYANYA......
Ni kweli mkuu na huenda hawa jamaa wanalaana, Hawaoni kinachoendelea!?
NAPE
MAKAMBA
NCHEMBA
Vijana ninyi mmeshindwa kufanya kazi????
 
tatizo la ccm ni wagumu wa kufikiri wanafikiri hiki kizazi ni cha mwaka 47,ambacho kila walichokuwa wanawaambia wanaitikia ndo mzee(kwa wasukuma ndoho taabu),umewapa ushauri mzuri ila kwa ukiziwi wao umepoteza muda but good ujumbe umefika

wacha tuwashauri mkuu hata kama watatuita mavuvuzela kama kawaida yao kauli za dhalau, au tunawivu wakike,
Utasikia mnauchungu mkajifungue na woote wanapiga makofi. JK hizi kauli wananchi wanazisikia sana hata kama wako kinya!
 
kwa engeneer manyanya bila shaka itakuwa ni “pre menopausal syndrome” imemuanza vibaya!! naambiwa na wataalam hapa walio katika mgomo kuwa ni tatizo la kifiziolojia ambalo huwapata baadhi ya wanawake kwa uwezo wao wa kiakili kushuka ghafla kutokana na kupungukiwa kichocheo (hormone)cha kike aina ya estrogeni
baada ya kufikia kikomo cha hedhi. umri wa tatizo hili ni,kati ya miaka 45 na 55(ndio umri wa stella bila shaka).kama nilivosema huwapata baadhi ya wanawake wa umri huu kwa style hii ya manyanya,ambapo mtu hukosa uwezo wa kutafakari mambo na kupungukiwa ghafla staha na uvumilivu. baada ya muda huu kupita atarejea kawaida, so naomba tumuhurumie na ttumuombee.
kuhusu mabumba na mwigulu bado nachunguza wana tatizo gani , kama kuna ajuae ntashukuru nikifahamishwa
 
Kuna kiongozi wajuu wa ccm aliwahi kusikika akisema,{ UKITAKA MAMBO YAKO YAWE MAZURI NJOO CCM}hapa ndipo maharamia walipo jipenyeza ndani ya ccm.Na walijipenyeza kwakuwa kauri hii haikuchuja nani waingie ccm ili mambo yao yawe mazuri

Sijui akina @Nape kaipata hii, chama wamehalibu wenyewe, msisingizie Upinzani, kwani tuseme ukweli nchi hii umeanza lini upinzani kuwa mkubwa kiasi hiki, TUACHE UNAFIKI CCM TUTAPONA!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom