Mh. Mabumba, Mh. Manyanya & Mh. Mwigulu, Msituharibie CCM yetu!

Ni siku nyingine tena, mwenzetu Mh. Mabumba alipokuwa amekalia kiti cha Bunge alijitelezesha na kujiingiza katika tope lililomchafua na baadaye akashindwa kutoka humo hadi watani zetu wakaanza kutucheka na mbaya zaidi wananchi tunaowategemea wanaanza kutuona kuwa sisi hatuna watu makini na kwamba pengine tupo si kwa ajili ya haki na maendeleo yao.

Mh. Mabumba: Hivi ulipomwambia Mh. Mnyika kuwa ‘anawashwa, akae chini’ ulimaanisha nini na ulitumia kanuni ipi kuachilia tusi hilo na kwa faida ya nani. Unafikiri kuwa CCM tunapata sifa kwa kutoa matusi au kujibu kwa matusi Wapinzani wakati umepewa dhamana ya kuongoza kikao cha juu sana katika nchi- cha muhimili wa Taifa? Yaani mwangwi wa sauti yako ya “Kaa chini!!... cheap popularity !!....” imekuexpose kuwa huwezi kuongoza vikao vya namna hiyo wala ku-controll heated debates. A Moderator will never dream to be defamatory.

Mh. Eng. Manyanya: Ulianza vyema kumpa pole Dr. Ulimboka na pia si vibaya ulipoonyesha masikitiko ya Wananchi kukoswa huduma muhimu za Afya tokana na mgomo. Lakini imeshangaza ulimwengu, kwa heshima uliyonayo kama Msomi, Mbunge na Mkuu wa Mkoa kujiingiza katika kauli tata na za mipasho hadharani.
Ni kitu gani kilikupeleka uendelee hadi kufikia kutamka waziwazi ndani ya Bunge hitimisho kuwa CHADEMA wanahusika katika kumteka na kumjeruhi Dr. Ulimboka? Ukasema kwamba wao ndio wenye magandwa kama wale waliomteka Daktari. Aidha ulijisukumiza katika shimo hatari kwa kuanza kumbeza Dr. Ulimboka aliye katika matibabu ya kuokoa maisha yake kwa kumfananisha hadharani na Muuaji Hitler; Eng. what a scrawny analysis, fallacious, insalubrious talk & dodgy statements!

Injinia, je huwezi kufikiri kwa nini hata katika speech ya Rais, aliongelea mgomo usio halali lakini aliwaomba Madaktari warudi kazini na kuhusu Ulimboka alitoa kauli za kuagiza vyombo vya dola kuwatafuta wahusika (wawe ni wa CCM, CHADEMA, CUF au wasio na Chama sisi hatujui) na shauri hilo lifikishe mbele ya haki. Wewe unaanza kumhukumu mtu kama huyo aliyepona kuuawa na kumwita Muuaji katika hali aliyo nayo sasa kwa faida ya nani? Unafikiri kuwa wananchi wataipenda CCM zaidi kwa kuongea hivyo wakati wananchi wote wanalaani kwa namna yeyote mtu kutekwa na kupigwa au kuuwawa hata kama ana makosa maana kwa nini asifikishwe katika vyombo vya dola kama ana kesi ya kujibu?

Mh. Mwigulu:
Ulishashauriwa siku za nyumakuwa kwa level yako kama Mbunge na Kiongozi wa Kitaifa wa CCM (NEC – Uchumi & Fedha), kabla ya kuongea ebu tulia na kufikiri kidogo. Ile statement uliyo quote Bungeni ya Wapinzani wakisema “endeleeni kudai haki zenu sisi tunawaunga mkono”, huwezi kuitumia kuthibitisha kuwa CHADEMA wamehusika na tukio la kumteka Daktari wala kuongoza migomo isiyo halali! Hata mimi na wengi wetu wana CCM tunasema kuwa moja ya majukumu yetu ni kuwaunga mkono Wananchi kudai haki zao. Rejea Lengo namba 5 la CCM;
“Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii hifadhi ya masiha yake na mali yake kwa mujibu wa sheria” na “pia namba 7 ;
“Kusimamia haki na maendeleo ya Wakulima, Wafanyakazi na Wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea; na hasa kuona kuwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake.

Mh. Mwigulu, kwa utetezi au upingaji wa kauli hiyo tu, Wananchi wataweza kutofautisha kuwa ni nani yuko kwa ajili ya haki zao na ni yupi hayuko nao. Hakika mnasababisha watu kutuchukia na Chama chetu bila kujua maskini! Taarifa yako Bungeni leo tena haikuwa na mashiko. Sikilizeni, Kazi yetu CCM inatakiwa kuwa kusukuma kwa ushawishi Madaktari & Serikali kukutana na kutatua mgogoro uliopo. Pili, ni kuhakikisha kuwa yeyote aliyeshiriki jaribio la kumwondoa uhai Dr. Ulimboka anafikishwa mbele ya haki. Kama tuna madai juu ya Ulimboka tuyafaili afikishwe polisi na mahakamani ayajibu. Na kamwe iwe marufuku yeyote mwana CCM kushabikia dhuluma, vitisho, utekaji wa wananchi na kujichukulia sheria mkononi hata kama ana hatia. Anayebisha basi avuliwe uanachama wa CCM maana yu kinyume na lengo letu la CCM namba 16.

“Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna aina yoyote ya dhuluma, vitisho, ubaguzi , rushwa , uonevu na au upendeleo”. Halafu tuelewe kuwa kuwa na nia ya kusikiliza madai ya madakrari ni tofauti na kwamba yametekelezwa.

Nauliza hivi ni Madaktari wangapi leo hii wameshapewa hayo magari au hata kujaza fomu za mikataba hiyo nchini kote, waliokwisha pewa makazi, ambao wameshaanza kupokea hiyo allowance mpya wanazosema na mishahara ya juu wakati tunajua kuwa kuna Madaktari wengi sana kote nchini (hii si issue ya Muhimbili tu) ambao bado wana madai ya arrreas za mishahara yao ya toka mwaka jana!

Kwa nini mnapenda sana kumpa taarifa zisizo kamili Rais wetu eti yote kasoro mawili tu ndiyo yametekelezwa? Wabunge muitishe taarifa za ma- RMO's kama hawana madai ya Madaktari ya siku nyingi tena ya vile viwango vya zamani na hayajalipwa? Ndani ya CCM tupo wengi ambao hatuvumi lakini tupo. Msituharibie CCM yetu- Arhrhghh!!

Jueni kuwa CHADEMA wanapoona tunakubali kuvaa viatu walivyotuazima wanafurahi sana! Watch out our role & strategies are completely different:yawn:!

Intelligente, Gracias!
 
If you're truly a ccm member then kudos. That silly party has exclusively become a lynch mob tell ya.

It's a miracle you're still there and wishing anything good for that sincere useless party.
 
Ni siku nyingine tena, mwenzetu Mh. Mabumba alipokuwa amekalia kiti cha Bunge alijitelezesha na kujiingiza katika tope lililomchafua na baadaye akashindwa kutoka humo hadi watani zetu wakaanza kutucheka na mbaya zaidi wananchi tunaowategemea wanaanza kutuona kuwa sisi hatuna watu makini na kwamba pengine tupo si kwa ajili ya haki na maendeleo yao.

Mh. Mabumba: Hivi ulipomwambia Mh. Mnyika kuwa ‘anawashwa, akae chini' ulimaanisha nini na ulitumia kanuni ipi kuachilia tusi hilo na kwa faida ya nani. Unafikiri kuwa CCM tunapata sifa kwa kutoa matusi au kujibu kwa matusi Wapinzani wakati umepewa dhamana ya kuongoza kikao cha juu sana katika nchi- cha muhimili wa Taifa? Yaani mwangwi wa sauti yako ya "Kaa chini!!... cheap popularity !!...." imekuexpose kuwa huwezi kuongoza vikao vya namna hiyo wala ku-controll heated debates. A Moderator will never dream to be defamatory.

Mh. Eng. Manyanya: Ulianza vyema kumpa pole Dr. Ulimboka na pia si vibaya ulipoonyesha masikitiko ya Wananchi kukoswa huduma muhimu za Afya tokana na mgomo. Lakini imeshangaza ulimwengu, kwa heshima uliyonayo kama Msomi, Mbunge na Mkuu wa Mkoa kujiingiza katika kauli tata na za mipasho hadharani.
Ni kitu gani kilikupeleka uendelee hadi kufikia kutamka waziwazi ndani ya Bunge hitimisho kuwa CHADEMA wanahusika katika kumteka na kumjeruhi Dr. Ulimboka? Ukasema kwamba wao ndio wenye magandwa kama wale waliomteka Daktari. Aidha ulijisukumiza katika shimo hatari kwa kuanza kumbeza Dr. Ulimboka aliye katika matibabu ya kuokoa maisha yake kwa kumfananisha hadharani na Muuaji Hitler; Eng. what a scrawny analysis, fallacious, insalubrious talk & dodgy statements!

Injinia, je huwezi kufikiri kwa nini hata katika speech ya Rais, aliongelea mgomo usio halali lakini aliwaomba Madaktari warudi kazini na kuhusu Ulimboka alitoa kauli za kuagiza vyombo vya dola kuwatafuta wahusika (wawe ni wa CCM, CHADEMA, CUF au wasio na Chama sisi hatujui) na shauri hilo lifikishe mbele ya haki. Wewe unaanza kumhukumu mtu kama huyo aliyepona kuuawa na kumwita Muuaji katika hali aliyo nayo sasa kwa faida ya nani? Unafikiri kuwa wananchi wataipenda CCM zaidi kwa kuongea hivyo wakati wananchi wote wanalaani kwa namna yeyote mtu kutekwa na kupigwa au kuuwawa hata kama ana makosa maana kwa nini asifikishwe katika vyombo vya dola kama ana kesi ya kujibu?

Mh. Mwigulu:
Ulishashauriwa siku za nyumakuwa kwa level yako kama Mbunge na Kiongozi wa Kitaifa wa CCM (NEC – Uchumi & Fedha), kabla ya kuongea ebu tulia na kufikiri kidogo. Ile statement uliyo quote Bungeni ya Wapinzani wakisema "endeleeni kudai haki zenu sisi tunawaunga mkono", huwezi kuitumia kuthibitisha kuwa CHADEMA wamehusika na tukio la kumteka Daktari wala kuongoza migomo isiyo halali! Hata mimi na wengi wetu wana CCM tunasema kuwa moja ya majukumu yetu ni kuwaunga mkono Wananchi kudai haki zao. Rejea Lengo namba 5 la CCM;
"Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii hifadhi ya masiha yake na mali yake kwa mujibu wa sheria" na "pia namba 7 ;
"Kusimamia haki na maendeleo ya Wakulima, Wafanyakazi na Wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea; na hasa kuona kuwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake.

Mh. Mwigulu, kwa utetezi au upingaji wa kauli hiyo tu, Wananchi wataweza kutofautisha kuwa ni nani yuko kwa ajili ya haki zao na ni yupi hayuko nao. Hakika mnasababisha watu kutuchukia na Chama chetu bila kujua maskini! Taarifa yako Bungeni leo tena haikuwa na mashiko. Sikilizeni, Kazi yetu CCM inatakiwa kuwa kusukuma kwa ushawishi Madaktari & Serikali kukutana na kutatua mgogoro uliopo. Pili, ni kuhakikisha kuwa yeyote aliyeshiriki jaribio la kumwondoa uhai Dr. Ulimboka anafikishwa mbele ya haki. Kama tuna madai juu ya Ulimboka tuyafaili afikishwe polisi na mahakamani ayajibu. Na kamwe iwe marufuku yeyote mwana CCM kushabikia dhuluma, vitisho, utekaji wa wananchi na kujichukulia sheria mkononi hata kama ana hatia. Anayebisha basi avuliwe uanachama wa CCM maana yu kinyume na lengo letu la CCM namba 16.

"Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna aina yoyote ya dhuluma, vitisho, ubaguzi , rushwa , uonevu na au upendeleo". Halafu tuelewe kuwa kuwa na nia ya kusikiliza madai ya madakrari ni tofauti na kwamba yametekelezwa.

Nauliza hivi ni Madaktari wangapi leo hii wameshapewa hayo magari au hata kujaza fomu za mikataba hiyo nchini kote, waliokwisha pewa makazi, ambao wameshaanza kupokea hiyo allowance mpya wanazosema na mishahara ya juu wakati tunajua kuwa kuna Madaktari wengi sana kote nchini (hii si issue ya Muhimbili tu) ambao bado wana madai ya arrreas za mishahara yao ya toka mwaka jana!

Kwa nini mnapenda sana kumpa taarifa zisizo kamili Rais wetu eti yote kasoro mawili tu ndiyo yametekelezwa? Wabunge muitishe taarifa za ma- RMO's kama hawana madai ya Madaktari ya siku nyingi tena ya vile viwango vya zamani na hayajalipwa? Ndani ya CCM tupo wengi ambao hatuvumi lakini tupo. Msituharibie CCM yetu- Arhrhghh!!

Jueni kuwa CHADEMA wanapoona tunakubali kuvaa viatu walivyotuazima wanafurahi sana! Watch out our role & strategies are completely different:yawn:!
Mkuu wangu ni rahisi sana kujaribu kujitofautisha na wengine kwa kutumia kitabu. Katiba ni sawa na Biblia au Kuran haina maana waumini wake pia ni wazuri kiasi hicho. Akili mu kichwa! mnachokifanya nyie ndio tafsiri ya utu wenu, hiyo katiba tutaitumia tu kupima Uzalendo wako.

Nyie wenyewe mliipitisha Bajeti ya serikali ambayo sekta ya Afya ilitengewa kiduchu na mkapiga makofi na vifijo kuipitisha, leo wewe tena unakuja hapa kuunga mkono madaktari wakati unajua fedha iliyotengwa haitoshi kufanya hata nusu ya madai ya madaktari na kama yakifanyika basi yatakomba fungu la manendeleo (development).

Je, mliunga mkono bajeti hiyo na kuipiga vita ile ya Upinzani kwa ushabiki tu au? maanake tofauti yetu na hawa kina Mabumba, Manyanya na Mwigulu ni kwamba hawa wameonyesha sura zenu halisi kwa maneno makali wakati nyie mkijificha nyuma ya ngozi ya kondoo ndio mmetuumiza zaidi kuipitisha bajeti ambayo itawaumiza wananchi wote. Kuwa na digrii ya Uinjinia ndio ni kigezo za mtu kutokuwa hana hekima wala busara?..

Kama kweli una nia njema na una uchungu na madaktari ombeni sijui ndio mwongozo hiyo bajeti irudishwe kwa rais kabla hajaipitishwa na kuboreshwa ili iweze kukidhi mahitaji yote muhimu.. Sio longolongo za kulaumiana wakati ukweli CCM wote roho zenu chafu, mnatazama sana maslahi yenu badala ya Taifa japokuwa kitabu chenu kinawaumbua..Haya maneno matupu hayawezi vunja mfupa, kaa kweli wewe unawapenda wananchi wako pambana na matumizi mabaya ya serikali.
 
Nimekuwa nikifuatilia matangazo ya moja ya moja (TBC) ya bunge kwa muda mrefu, ni ukweli uliowazi kuwa wapinzani wengi mfano Dr Slaa, Zitto, Mnyika, Mdee n.k wamepata umaarufu walionao kupitia bunge huku kwa upande mwingine bunge hilo hilo likishusha sifa nzuri ya CCM, bunge hili la JMT pia ndo chanzo cha kupanda kwa CHADEMA na kushuka kwa CCM.

Sasa naona wabunge wa CCM haswa haswa ndugu MWIGULU NCHEMBA wamekuja na style fulan hivi ya ujibuji mabigo kwa wapinzani wa serikali, lakin kwa bahati mbaya nahisi wamekosea sana katika kuziimplement hizo strategies zao, badala ya wao kuwin majority support sasa wanaonekana wehu!
Mfano ndugu MWIGULU NCHEMBA badala ya kujenga hoja ya kuitetea serikali yake yeye amekuwa bingwa wa kutuonesha makosa madogo madogo ya kiubinadamu mfano kusahaulika au kuongezeka kwa maneno ktk hotuba za wapinzan na baadhi ya makosa ya kiuchapaji.

USHAURI WANGU KWA WABUNGE WA CCM:-
Hebu jaribuni kuongea yale wananchi tunayopenda kusikia ili muweze kuwin support yetu, sidhani kama wabunge wa CCM hawana hoja za msingi na za maana za kuongea bungeni, sidhan kama ndugu MWIGULU NCHEMBA hoja zake ni za makosa ya kiuchapaji tu, HEBU WABUNGE WETU JITAHIDINI KUTOA HOJA ZA KUWAJENGEA HESHIMA NA SI ZILE ZINAZOWAFANYA MUONEKANE WEHU!
Shukrani.
 
Manyanya Eng. nilizipenda hoja zake vibaya mno, ila kwa sasa naona amejifunza mipasho, nasikitika kaharibiwa sana na huyu mchumi wetu numberi one.

Pole sana Engineer...angalia sana kama wengine walivyokwambia CCM inakuharibia, maana ki ukweli juzi ulinichefua sana sikutegemea maneno yasiyo na mantiki na tija kwa taifa yatoke kinywani mwako.
 
napenda sana tunavyojenga hoja wanajf but ukimuongelea sana m2 unampa umaarufu. wao wamerusha mawe wamesikia kelele wanajua yametupata. let us not finish our time sharing stupid facts
 
Mwigulu.... ninakuchukia sana na tena ninachochukia ccm na viongozi wake ni pale ambapo mwananchi yeyote anayeonekana anawachambua na kuyaweka madhaifu ya ccm peupe, ccm wako radhi kumzima. Mmojawapo ni wewe Mwigulu unaelewa ukweli wa yanayoelezwa ila kwa makusudi unawapumbaza wananchi kwa hila za maneno.
 
Anachonikera Mwigulu, ni uongeaji wake wa kupayuka, kuongea kwa jazba, kuongea kwa dharau akioneha kuwa yeye ni bora kuliko watu wengine. Kweli kuiba wake za watu nayo ni laana ambayo huweza mgahrimu mttu maisha yake yote, hana pa kuomba suluhu
hivi huyu chemba hana cha kuwaombea bungeni wananchi wa jimbo lake?
 
Nimekuwa nikifuatilia matangazo ya moja ya moja (TBC) ya bunge kwa muda mrefu, ni ukweli uliowazi kuwa wapinzani wengi mfano Dr Slaa, Zitto, Mnyika, Mdee n.k wamepata umaarufu walionao kupitia bunge huku kwa upande mwingine bunge hilo hilo likishusha sifa nzuri ya CCM, bunge hili la JMT pia ndo chanzo cha kupanda kwa CHADEMA na kushuka kwa CCM.

Sasa naona wabunge wa CCM haswa haswa ndugu MWIGULU NCHEMBA wamekuja na style fulan hivi ya ujibuji mabigo kwa wapinzani wa serikali, lakin kwa bahati mbaya nahisi wamekosea sana katika kuziimplement hizo strategies zao, badala ya wao kuwin majority support sasa wanaonekana wehu!
Mfano ndugu MWIGULU NCHEMBA badala ya kujenga hoja ya kuitetea serikali yake yeye amekuwa bingwa wa kutuonesha makosa madogo madogo ya kiubinadamu mfano kusahaulika au kuongezeka kwa maneno ktk hotuba za wapinzan na baadhi ya makosa ya kiuchapaji.

USHAURI WANGU KWA WABUNGE WA CCM:-
Hebu jaribuni kuongea yale wananchi tunayopenda kusikia ili muweze kuwin support yetu, sidhani kama wabunge wa CCM hawana hoja za msingi na za maana za kuongea bungeni, sidhan kama ndugu MWIGULU NCHEMBA hoja zake ni za makosa ya kiuchapaji tu, HEBU WABUNGE WETU JITAHIDINI KUTOA HOJA ZA KUWAJENGEA HESHIMA NA SI ZILE ZINAZOWAFANYA MUONEKANE WEHU!
Shukrani.
bado wanaendekeza akili ndogo kutawala akili kubwa-mhe. mch.peter msigwa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom