Mh. Mabumba, Mh. Manyanya & Mh. Mwigulu, Msituharibie CCM yetu!

Nadhani hapo ni kama kumshauri mbuzi akuvushe barabara!

Na kushauri usiangaike na hicho chama kimesha jifia!

Juzi ametoa hotuba kasimama, usishangae hotuba ijayo kuitoalea msituni, usiulize msitu gani.

Yaan damu yamtu ina changanya sana.

Mkuu ni kweli ni dalili za JK kuchanganyikiwa ndo maana Vijana tunaamua kumshauri ili asipate matatizo ya kuchanganyikiwa!
 
mwigulu chemba ni tatizo namba 1,na ndie anamshauri vibaya rais wakati uwezo wake ni mdogo

Raisi naye lazima ajue kuna wanafiki wanamfanye yeye Mfalme JUHA, wanamtoa nguo hadharani raisi wetu, Hawa watu lazima watakuwa wanatumwa kumharibia JK!
 
mbona una ogopa bila sababu
jk ni malaika?
Aliyetaka jk hasisemwe kafa yeye!

Ccm hamna jipya hivi,kila kitu cdm!

Mkuu sisi sote ni watanzania si kuwa naogopa hapana, Ila hiki chama kimefika pabaya ona sasa hata wakulima mbeya leo wamefunga barabara, Ni nani aliye na nafuu nchi hii zaidi ya mafisadi wanaotanua tuu!
 
Kweli. Chuo kimoja hapa nchini wlikuwapo wanafunzi 15 mwaka fulani. Mwisho wa mwaka disco ikawakumba wanafunzi 13 wakabaki wawili ambao walisuppliment. Hakuna aliyefaulu moja kwa moja first seat. Wawili hao wakapita baadaye, mmoja mganda na mmoja mhindi. Waliendelea hao wawili mpaka shule ikaisha. Mwishoni kuna zawadi ya mwanafunzi bora wa kwanza na wa pili. Unaona? Walibadilishana haohao. Kwa statistics walikuwa wanaambiwa 50% of the class have scored above a pass mark and 50% have scored below a pass mark. Kumbe ni mmoja kapata 51% na mwenzake kapata 49%. Hiyo ndiyo halisia ya hao unaowasema.

Hahahahaaaaaaaaaaaa! Mambo ya electrical engineering haya! Mkuu hii kama sio ya Professor LUHANGA (VC wakati huo) wa UDSM, basi leo 'nishinde dhana zangu zikeshe zimelala mwezi mzima'
 

Najua ccm itakufa siku moja lakini walau ife kifo kizuri mkuu,
Chama hakiwezi kufa kwa aibu kubwa na sisi tufurahie ufaji huo, mbona tunavijana wengi sana, hata propaganda zinatushinda, tunaleta mambo ya hovyo kabisa, utamwambia nani uli ailitekwa na CDM akuelewe??
 
Mawenge bwana!
Juzi tumeona kwenye tv uchaguzi pale kawe mlivyo chezeana faulo,
kwa style hii nani wa kushauriana hapa kama ni kushauri nyie mnatakiwa kubadili system nzima kuanzia chini mpaka juu
manake hadi huku chini kwenye chaguzi zenu mnachakachuana sasa hawa wakubwa huku juu mnategemea nini???
Hebu mkae tu pembeni sababu msha proove nyie ni dhaifu!
 
Huyu bwana anajaribu sana afikie viwango vya wabunge kama J.J Mnyika, Tundu LIssu, Mh. Mnyaa, Godfrey Zambi, Zitto, HKigangwala, David Kafulila, Moses Mchali n.k. Kwenye uibuaji pamoja na uchanganuzi wa mambo mbalimbali ya kitaifa. Kwa bahati mbaya sana hana uwezo wa kujenga hoja ambazo zinakuna na kupata baraka za wengi ( powerful arguments).
Hawezi kujenga hoja ambayo itasimama yenyewe bila kuzalilisha au kumuathiri mtu au kikundi fulani kinachohitaji heshima.
Mara nyingi nimekuwa nikimuana akiibua hoja ambazo zinajikita zaidi kwenye uzalilishaji, kitu ambacho naona hakiendani na experience pamoja na elimu kubwa aliyonayo huyu mbunge.
Bila kutambua athari za approach anayotumia huyu mbunge wa CCM, amekuwa akipata support ya kiti kinachoongoza mjadala wa bunge kwa wakati huo. Sijajua kama wanafahamu huku nje ya bunge watazamaji tunaona kinyaa pamoja na kuhisi kichefuchefu kila mara huyu bwana anaposimama na kuanza kutema uchafu ili kupoteza muda, tabia hii ikiendekezwa itazidi kuwagharimu sana wanachama wa CCM.
Mfano mzuri wa gharama zitakazotokezea kwenye scandal ya EPA; ni leo hii J.J Mnyika alivyoambiwa awasilishe ushahidi unaoonesha kwamba Mwigulu Nchemba anahusika na kesi za EPA. Bila kujua ya kwamba wananchi watasaidia katika kukusanya na kumpatia J.J Mnyika ushahidi wote unaoweza kusaidia kuonesha kwa kiasi gani Mwigulu anahusika kwa moja kwa moja kwenye wizi wa EPA pale benki kuu, akiwa kama mtumishi.
 
Mbunge Mwigullu Mchemba amesema, Wabunge wa Chadema wengi ni Ndugu na kwamba sitting Plan yao bungeni haina tofauti na wanavyokaa katika vikao ya kifamilia na kiu-koo.
 
una fikiri mwigulu ana akili sasa na kajichomea mwenyewe kwenye ishu ya benki kuu
 
Nadhani magamba wamekosea kumpa ubunge huyu jamaa mwigulu nchemba angefaa awekwe kwenye kitengo cha propaganda cha ccm .mweupe sana bungeni katika uchangiaji wake nilimsikiliza mbatia leo nikamsikiliza na yeye leo.Alikuwa kituko nadhani yeye hapashwi kuwepo bungeni.
 
Mwingilu Nchemba aliwahi kunukulikuwa Arumeru Mashariki alipoulizwa kwamba kwanini Yeye na Lusinde wanafanya kampeini za matusi badala ya kutangaza sera za CCM. Mwingulu alijibu kuwa "Watanzania hawataki kusikiliza sera, wanafurahia kusikiliza matusi"

Just imagine mbunge mwenye mindset hiyo ataongea nini bungeni zaidi kutukuna?!
 
Hiyo kauli ni aibu na alishindwa kuithibitisha. Mwigulu anaiaibisha ccm. Leo nimefurahi jinsi Mnyika na wenzake walivyowabana wapotoshaji kupitia kanuni za Bunge.
 
Mbunge Mwigullu Mchemba amesema, Wabunge wa Chadema wengi ni Ndugu na kwamba sitting Plan yao bungeni haina tofauti na wanavyokaa katika vikao ya kifamilia na kiu-koo.

Ndio ukweli na halina ubishi haiwezekani kati ya viti maalum 20 , mkoa wa kilimanjaro peke yake utoe vita 11 na wote ni wan a ndugu, kweli huyu Mwigulu ni mwiba mkali kwa CDM kila siku anawaumbua kama watoto.
 
Sasa Zambi naye wapi na wapi! Si huyu ndiye anayetuhumiwa na Kafulila kula rushwa. Anyway, kuna huyu mwingine Juma Ngamia nilidhani ana akili nzuri kumbe naye ana akili za kingamia tu. Asubuhi anaambiwa madaktari bingwa wameanza mgomo, yeye anasema hawawezi kufuata maneno ya vyombo vya habari. Tumbafu zake ngamia mkubwa huyu. CCM wote makalio tu.
 
Stella Martin Manyanya alikosa utu jana.Alitakiwa awe na utu kama kiongozi wa kiserikali na Mbunge.Amemsemea 'mbaya' mgonjwa na mwathiriwa wa mateso yaliyotanguliwa na utekaji. Ni afadhali angeishia 'kuropoka' kuwa CHADEMA ndio waliomteka Dr.Ulimboka.Amemdhalilisha Dr.Ulimboka ilhali mwenzake ni mgonjwa.Stella amekosa staha.

Stella Martin Manyanya (ambaye si Injinia kama anavyojiita) ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.Yeye pamoja na Mh. Jasson Rweikiza ni wateule wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Baraza hilo tangu 2010.Kama Mjumbe wa Baraza la Chuo,Stella amekuwa 'fisadi toto'.

Kiutaratibu,Wajumbe wa Baraza la Chuo watokao mikoani kuhudhuria vikao vya Baraza la Chuo hulipiwa usafiri,malazi na chakula achilia mbali posho ya kikao husika.Gharama huongezeka kadiri Mjumbe anavyotokea mbali zaidi. Huu ndio upenyo wa Stella kufisidi. Mara zote husema anatokea Rukwa hata kama yuko Dar es Salaam au Dodoma-Bungeni.

Kuna siku nilikuwa naye Ofisi Ndogo za Bunge Dar es Salaam.Alipokea simu na kusema kuwa yuko Rukwa na kesho yake angetokea huko(Rukwa) kuhudhuria kikao cha Baraza la chuo. Nilishtuka sana hadi naye akatambua.Anafisidi fedha za Chuo bila kujali. Namsubiri kikao cha Baraza la Chuo cha tarehe 27/7/2012 nimpe ukweli wake. More to come...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom