Mh. Mabumba, Mh. Manyanya & Mh. Mwigulu, Msituharibie CCM yetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mh. Mabumba, Mh. Manyanya & Mh. Mwigulu, Msituharibie CCM yetu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by babykailama, Jul 2, 2012.

 1. babykailama

  babykailama JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 241
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni siku nyingine tena, mwenzetu Mh. Mabumba alipokuwa amekalia kiti cha Bunge alijitelezesha na kujiingiza katika tope lililomchafua na baadaye akashindwa kutoka humo hadi watani zetu wakaanza kutucheka na mbaya zaidi wananchi tunaowategemea wanaanza kutuona kuwa sisi hatuna watu makini na kwamba pengine tupo si kwa ajili ya haki na maendeleo yao.

  Mh. Mabumba: Hivi ulipomwambia Mh. Mnyika kuwa ‘anawashwa, akae chini' ulimaanisha nini na ulitumia kanuni ipi kuachilia tusi hilo na kwa faida ya nani. Unafikiri kuwa CCM tunapata sifa kwa kutoa matusi au kujibu kwa matusi Wapinzani wakati umepewa dhamana ya kuongoza kikao cha juu sana katika nchi- cha muhimili wa Taifa? Yaani mwangwi wa sauti yako ya "Kaa chini!!... cheap popularity !!...." imekuexpose kuwa huwezi kuongoza vikao vya namna hiyo wala ku-controll heated debates. A Moderator will never dream to be defamatory.


  Mh. Eng. Manyanya: Ulianza vyema kumpa pole Dr. Ulimboka na pia si vibaya ulipoonyesha masikitiko ya Wananchi kukoswa huduma muhimu za Afya tokana na mgomo. Lakini imeshangaza ulimwengu, kwa heshima uliyonayo kama Msomi, Mbunge na Mkuu wa Mkoa kujiingiza katika kauli tata na za mipasho hadharani.
  Ni kitu gani kilikupeleka uendelee hadi kufikia kutamka waziwazi ndani ya Bunge hitimisho kuwa CHADEMA wanahusika katika kumteka na kumjeruhi Dr. Ulimboka? Ukasema kwamba wao ndio wenye magandwa kama wale waliomteka Daktari. Aidha ulijisukumiza katika shimo hatari kwa kuanza kumbeza Dr. Ulimboka aliye katika matibabu ya kuokoa maisha yake kwa kumfananisha hadharani na Muuaji Hitler; Eng. what a scrawny analysis, fallacious, insalubrious talk & dodgy statements!

  Injinia, je huwezi kufikiri kwa nini hata katika speech ya Rais, aliongelea mgomo usio halali lakini aliwaomba Madaktari warudi kazini na kuhusu Ulimboka alitoa kauli za kuagiza vyombo vya dola kuwatafuta wahusika (wawe ni wa CCM, CHADEMA, CUF au wasio na Chama sisi hatujui) na shauri hilo lifikishe mbele ya haki. Wewe unaanza kumhukumu mtu kama huyo aliyepona kuuawa na kumwita Muuaji katika hali aliyo nayo sasa kwa faida ya nani? Unafikiri kuwa wananchi wataipenda CCM zaidi kwa kuongea hivyo wakati wananchi wote wanalaani kwa namna yeyote mtu kutekwa na kupigwa au kuuwawa hata kama ana makosa maana kwa nini asifikishwe katika vyombo vya dola kama ana kesi ya kujibu?


  Mh. Mwigulu:
  Ulishashauriwa siku za nyumakuwa kwa level yako kama Mbunge na Kiongozi wa Kitaifa wa CCM (NEC – Uchumi & Fedha), kabla ya kuongea ebu tulia na kufikiri kidogo. Ile statement uliyo quote Bungeni ya Wapinzani wakisema "endeleeni kudai haki zenu sisi tunawaunga mkono", huwezi kuitumia kuthibitisha kuwa CHADEMA wamehusika na tukio la kumteka Daktari wala kuongoza migomo isiyo halali! Hata mimi na wengi wetu wana CCM tunasema kuwa moja ya majukumu yetu ni kuwaunga mkono Wananchi kudai haki zao. Rejea Lengo namba 5 la CCM;
  "Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya kupata kutoka katika jamii hifadhi ya masiha yake na mali yake kwa mujibu wa sheria" na "pia namba 7 ;
  "Kusimamia haki na maendeleo ya Wakulima, Wafanyakazi na Wananchi wengine wenye shughuli halali za kujitegemea; na hasa kuona kuwamba kila mtu ana haki ya kupata malipo yanayostahili kutokana na kazi yake.

  Mh. Mwigulu, kwa utetezi au upingaji wa kauli hiyo tu, Wananchi wataweza kutofautisha kuwa ni nani yuko kwa ajili ya haki zao na ni yupi hayuko nao. Hakika mnasababisha watu kutuchukia na Chama chetu bila kujua maskini! Taarifa yako Bungeni leo tena haikuwa na mashiko. Sikilizeni, Kazi yetu CCM inatakiwa kuwa kusukuma kwa ushawishi Madaktari & Serikali kukutana na kutatua mgogoro uliopo. Pili, ni kuhakikisha kuwa yeyote aliyeshiriki jaribio la kumwondoa uhai Dr. Ulimboka anafikishwa mbele ya haki. Kama tuna madai juu ya Ulimboka tuyafaili afikishwe polisi na mahakamani ayajibu. Na kamwe iwe marufuku yeyote mwana CCM kushabikia dhuluma, vitisho, utekaji wa wananchi na kujichukulia sheria mkononi hata kama ana hatia. Anayebisha basi avuliwe uanachama wa CCM maana yu kinyume na lengo letu la CCM namba 16.

  "Kuona kwamba katika nchi yetu hakuna aina yoyote ya dhuluma, vitisho, ubaguzi , rushwa , uonevu na au upendeleo". Halafu tuelewe kuwa kuwa na nia ya kusikiliza madai ya madakrari ni tofauti na kwamba yametekelezwa.

  Nauliza hivi ni Madaktari wangapi leo hii wameshapewa hayo magari au hata kujaza fomu za mikataba hiyo nchini kote, waliokwisha pewa makazi, ambao wameshaanza kupokea hiyo allowance mpya wanazosema na mishahara ya juu wakati tunajua kuwa kuna Madaktari wengi sana kote nchini (hii si issue ya Muhimbili tu) ambao bado wana madai ya arrreas za mishahara yao ya toka mwaka jana!

  Kwa nini mnapenda sana kumpa taarifa zisizo kamili Rais wetu eti yote kasoro mawili tu ndiyo yametekelezwa? Wabunge muitishe taarifa za ma- RMO's kama hawana madai ya Madaktari ya siku nyingi tena ya vile viwango vya zamani na hayajalipwa? Ndani ya CCM tupo wengi ambao hatuvumi lakini tupo. Msituharibie CCM yetu- Arhrhghh!!

  Jueni kuwa CHADEMA wanapoona tunakubali kuvaa viatu walivyotuazima wanafurahi sana! Watch out our role & strategies are completely different:yawn:!
   
 2. a

  andrews JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mwenye macho na aone na mwenye masikio askie mwenyewe ccm hakuna mtu wa namna hiyo ni wadhalimu kuliko kaburu alivyokuwa na siku ya ukombozi ikifika ccm mtajichimbia kwenye mahandaki
   
 3. Dijovisonjn

  Dijovisonjn JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 450
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  ukitaka kuona kuwa mh. spika Makinda anafaa kuwa spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania basi we mlinganishe na Mh. Mabumba
   
 4. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  CCM death is imminent, their MP's are looking more foolish and stupid as days go by.
   
 5. GreenCity

  GreenCity JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 4,667
  Likes Received: 2,146
  Trophy Points: 280
  Unaomba Wasiharibu CCM ipi tena! Iliyopo mbona ilishaharibika kitambo?
  Na kwa mwendo wa bunge kama la leo mbona watanyooka tu!
   
 6. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Well said.
   
 7. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  babykailama nikushukuru kwa uchambuzi wako mzuri. Kwa Mtanzania yeyote makini aliyeangalia bunge,hawa jamaa wamefanya mzaha mmoja mbaya sana. Wakati maelfu ya Watanzania waliolazwa ktk hospitali za umma wanasubiri suluhisho la mgomo wa madaktari,wao wanaleta mzaha,propoganda za kipuuzi,kejeri na ujinga! Sampuli hizi hazifai kushika madaraka ktk ofisi za Umma. Wanakiabisha Chama na Serikali.
   
 8. S

  Short white Senior Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwakweli ni aibu kubwa kwa CCM. Wamesahau kazi waliyotumwa na wananchi hata Kama wengine ni special seats!! Inatia hasira kuangalia udhaifu wao wa kiwango cha juu.
   
 9. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu umenenat vyema lakini unangoja nini huko ccm . ccm sio mama yako usifikiri watakusiliza angalia sana wasiku mwakyembe na kuku uli shauri yako banaa.
   
 10. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Katika mpira wa miguu timu ikizidiwa na ikianza kucheza rafu ujue itafungwa. Nadhani CCM sasa wamezidiwa hivyo wanacheza rafu. Refa [wananchi] ameanza kuwapa kadi za njano, wachunge sana kuna hatari ya kupata red card
   
 11. m

  mamabaraka Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 92
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  du hongera sana mtoa mada kwa uchambuzi yakinifu, binafsi walinikera sana hata mtoto mdogo wa miaka mitano hadi kumi anaweza kuona mbichi na mbivu bungeni. Wabunge wanasahau kuwa bunge la sasa si sawa na la mwaka 47, wananchi kote vijijin na mijini wanasikiliza na kuangalia bunge. Ukiongea pumba tunaona.
   
 12. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  We know we shall win as we are confident of the victory.
  M4C
   
 13. d

  dada jane JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ee Mungu ikumbuke Tanzania.
   
 14. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Naamini wabunge wengi wa CCM huwa wanafikiri kwa kutumia MASABURI
  Pangekuwa na namna ya kuwalaza bakora za ukweli ningejitolea kuwatandika kwa kuanza na hao viongozi wa bunge....!
  Wanakera sana.!
  Laana za wananchi na ziwe juu yao!
   
 15. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  kweli Bob Marley alisema
   
 16. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa hawa watu wajichanganya na kufanya propaganda za kuiiangamiza CCM yao kwa ulimbukeni wao eti wasomi! Inakuwaje Mwigulu anadai CDM inaunga mkono mgomo na mwenzake Manyanya wa chama hichohicho anasima na kudai CDM imemteka na kumpiga Steven Ulimboka Mtu anayeongoza mgomo Unaoungwa mkono na CDM Hiyo hiyo?

  Hizi ndizo propaganda zilizo gada Kabisa haziisaidii CCM zaidi ya Kuizika katika kaburi la wenzao KANU na UNIP!
   
 17. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,960
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  wapuuzi hawa!
   
 18. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,150
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Anachonikera Mwigulu, ni uongeaji wake wa kupayuka, kuongea kwa jazba, kuongea kwa dharau akioneha kuwa yeye ni bora kuliko watu wengine. Kweli kuiba wake za watu nayo ni laana ambayo huweza mgahrimu mttu maisha yake yote, hana pa kuomba suluhu
   
 19. Christine1

  Christine1 JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2012
  Messages: 12,291
  Likes Received: 1,214
  Trophy Points: 280
  wamejisahau kabisa,hawajui km bado miaka 2 na nusu hivi warudi majimboni!na hapo ndo watajua nguvu ya m4c
   
 20. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Well said mkuu, jitahidi hii analysis ichapishwe kwenye magazeti wananchi wengi waone uozo wa hawa jamaa hasa kwenye gazeti la UHURU
   
Loading...