illegal migrant
JF-Expert Member
- Oct 18, 2013
- 1,277
- 1,121
Mh nivumilie kweli nimekuwa nakuandama lakini ni kwa wema tu, siku za hivi karibuni ulitoa agizo kuwa ni marufuku kujenga, kuendeleza kuuziana maeneo yote yasiyopimwa, nadhani ulikuwa na lengo zuri tu katika kuzuia migogoro ya ardhi ambayo ipo mingi na inazidi kuibuka kila kukicha.
Sina uhakika kama agizo hili ulilitoa kisiasa ama ulidhamiria kwa sababu huku pembezoni watu bado wanauziana na ujenzi unaendelea kama kawaida kwa baraka zote za serikali ya mitaa, hawa wenyeviti wa serikali za mitaa ni kero na ni chanzo kikubwa sana wa migogoro wakishirikiana na watendaji wa halmashauri wasio waaminifu.
Inasikitisha sana kuona serikali inapambana na mipango miji wakati watu wanazidi kuuziana maeneo holela na kujenga holela sijui lengo ni nini hasa.....nawasilisha