Mh Lukuvi katazo la kujenga, kuendeleza au kuuziana maeneo yote yasiyopimwa limepuuzwa

illegal migrant

JF-Expert Member
Oct 18, 2013
1,277
1,117
Mh nivumilie kweli nimekuwa nakuandama lakini ni kwa wema tu, siku za hivi karibuni ulitoa agizo kuwa ni marufuku kujenga, kuendeleza kuuziana maeneo yote yasiyopimwa, nadhani ulikuwa na lengo zuri tu katika kuzuia migogoro ya ardhi ambayo ipo mingi na inazidi kuibuka kila kukicha.

Sina uhakika kama agizo hili ulilitoa kisiasa ama ulidhamiria kwa sababu huku pembezoni watu bado wanauziana na ujenzi unaendelea kama kawaida kwa baraka zote za serikali ya mitaa, hawa wenyeviti wa serikali za mitaa ni kero na ni chanzo kikubwa sana wa migogoro wakishirikiana na watendaji wa halmashauri wasio waaminifu.

Inasikitisha sana kuona serikali inapambana na mipango miji wakati watu wanazidi kuuziana maeneo holela na kujenga holela sijui lengo ni nini hasa.....nawasilisha
 
Na ndio haohao wanakwamisha maendeleo ya nchi, sheria ikifata mkondo wake wanalalama ooh tunaonewa
 
Yaani hutaki wenzako wajenge?
Hhutaki wenzako wauze viwanja walivyonunua kwa hela zao?
Hiyo migogoro inakuumiza vipi au inakuhusu vipi wewe?

Sijui kama una taarifa kuwa jiji la Dar linatakiwa lifumuliwe upya kama uliangalia vichwa vya habari vya magazeti ya jana zilitawala habari za bomoa bomoa.......kuna gazeti limeandika "tutawasaidia watakaobolewa" kuna lingine limeandika bomoa bomoa iko pale pale kuna lingine limeandika ukitaka usibomolewe fuata hatua hizi.
 
Sasa wao wakibomolewa kutokana na uzembe wao wa kujua au kutokujua wewe inakuuma nini?
Kwa ulivyoandika si kuwa unawaonea huruma hao watu bali naona ni kuwa unawaonea wivu wao wanauza
 
Yaani hutaki wenzako wajenge?
Hhutaki wenzako wauze viwanja walivyonunua kwa hela zao?
Hiyo migogoro inakuumiza vipi au inakuhusu vipi wewe?
We umesema wivu tu unamsumbua
 
H
Mh nivumilie kweli nimekuwa nakuandama lakini ni kwa wema tu, siku za hivi karibuni ulitoa agizo kuwa ni marufuku kujenga, kuendeleza kuuziana maeneo yote yasiyopimwa, nadhani ulikuwa na lengo zuri tu katika kuzuia migogoro ya ardhi ambayo ipo mingi na inazidi kuibuka kila kukicha.

Sina uhakika kama agizo hili ulilitoa kisiasa ama ulidhamiria kwa sababu huku pembezoni watu bado wanauziana na ujenzi unaendelea kama kawaida kwa baraka zote za serikali ya mitaa, hawa wenyeviti wa serikali za mitaa ni kero na ni chanzo kikubwa sana wa migogoro wakishirikiana na watendaji wa halmashauri wasio waaminifu.

Inasikitisha sana kuona serikali inapambana na mipango miji wakati watu wanazidi kuuziana maeneo holela na kujenga holela sijui lengo ni nini hasa.....nawasilisha

Hivi uko serious kweli?

mwenye wajibu wa kupanga mji ni nani? je ni serikali au ni wananchi? sasa kama mwenye wajibu wa kupanga mji hapangi unadhani maisha ya wananchi yanasimama.

Waziri na mtoa mada wote mna fikra sawa!

dawa ya kupanga miji ni kwa serikali kupanga na kupima viwanja vingi kuliko mahitaji ya wananchi ya wakati huo na ndio hapo serikali inakuwa na uhalali wa kupiga marufuku kujenga sehemu zisizopimwa. Mbali na kupima viwanja vingi zaidi inatakiwa viwanjo hivyo vipatikane kwa bei zinazoendana na vipato vya watu.

Tujiulize mwaka wa 2016/17 serikali katika jiji la Dar imepima viwanja vingapi? na je mahitaji ya watu yalikuwa kiasi gani? na ukiona tofauti utajua ni nani anayesababisha makazi holela.
 
Sasa wao wakibomolewa kutokana na uzembe wao wa kujua au kutokujua wewe inakuuma nini?
Kwa ulivyoandika si kuwa unawaonea huruma hao watu bali naona ni kuwa unawaonea wivu wao wanauza
Sijui unachotetea ni nini binafsi nimeshabomolewa nyumba, jaribu kuangalia post zangu za nyuma za malalamiko nimejidunduliza tena nashindwa kununua kwa hofu hii ambayo niliipata, waziri amepiga marufuku kuuza na kununuà ardhi isiyopimwa inanilazimu niendelee kukaa nyumba ya kupanga nawaonea huruma wale wanaondelea kuuziana na kujenga maeneo ya nje ya mji siku bomoa ikija......
 
Mh nivumilie kweli nimekuwa nakuandama lakini ni kwa wema tu, siku za hivi karibuni ulitoa agizo kuwa ni marufuku kujenga, kuendeleza kuuziana maeneo yote yasiyopimwa, nadhani ulikuwa na lengo zuri tu katika kuzuia migogoro ya ardhi ambayo ipo mingi na inazidi kuibuka kila kukicha.

Sina uhakika kama agizo hili ulilitoa kisiasa ama ulidhamiria kwa sababu huku pembezoni watu bado wanauziana na ujenzi unaendelea kama kawaida kwa baraka zote za serikali ya mitaa, hawa wenyeviti wa serikali za mitaa ni kero na ni chanzo kikubwa sana wa migogoro wakishirikiana na watendaji wa halmashauri wasio waaminifu.

Inasikitisha sana kuona serikali inapambana na mipango miji wakati watu wanazidi kuuziana maeneo holela na kujenga holela sijui lengo ni nini hasa.....nawasilisha

Mtoa mada nisaidie muktadha wa hili agizo kama kweli lipo. Nami nipate kumshangaa waziri Lukuvi
 
H

Hivi uko serious kweli?

mwenye wajibu wa kupanga mji ni nani? je ni serikali au ni wananchi? sasa kama mwenye wajibu wa kupanga mji hapangi unadhani maisha ya wananchi yanasimama.

Waziri na mtoa mada wote mna fikra sawa!

dawa ya kupanga miji ni kwa serikali kupanga na kupima viwanja vingi kuliko mahitaji ya wananchi ya wakati huo na ndio hapo serikali inakuwa na uhalali wa kupiga marufuku kujenga sehemu zisizopimwa. Mbali na kupima viwanja vingi zaidi inatakiwa viwanjo hivyo vipatikane kwa bei zinazoendana na vipato vya watu.

Tujiulize mwaka wa 2016/17 serikali katika jiji la Dar imepima viwanja vingapi? na je mahitaji ya watu yalikuwa kiasi gani? na ukiona tofauti utajua ni nani anayesababisha makazi holela.
Uko sahihi kabisa, NHC ambao walipewa jukumu la kujenga nyumba mijini kwa ajili ya kupangisha wafanyakazi na watu wa kipato cha chini imegeuka kuwa ya matajiri. Watu wakijihangaikia wapate walau pa kujisitiri wanakuja kubomolewa, huwa najiuliza hii nchi kama kuna watu wanatumia akili zao vizuri
 
Mh nivumilie kweli nimekuwa nakuandama lakini ni kwa wema tu, siku za hivi karibuni ulitoa agizo kuwa ni marufuku kujenga, kuendeleza kuuziana maeneo yote yasiyopimwa, nadhani ulikuwa na lengo zuri tu katika kuzuia migogoro ya ardhi ambayo ipo mingi na inazidi kuibuka kila kukicha.

Sina uhakika kama agizo hili ulilitoa kisiasa ama ulidhamiria kwa sababu huku pembezoni watu bado wanauziana na ujenzi unaendelea kama kawaida kwa baraka zote za serikali ya mitaa, hawa wenyeviti wa serikali za mitaa ni kero na ni chanzo kikubwa sana wa migogoro wakishirikiana na watendaji wa halmashauri wasio waaminifu.

Inasikitisha sana kuona serikali inapambana na mipango miji wakati watu wanazidi kuuziana maeneo holela na kujenga holela sijui lengo ni nini hasa.....nawasilisha

Matamshi ya waziri yako kinyume cha sheria
 
Lukuvi asitoe maamuzi utadhani Jamii hii ni ya Ulaya au mabara mengine yaliyoendelea!. Lazima ajue mazingira na hali ya jamii yake!
Kupima ardhi siyo chini ya Milioni Nne na nusu, wangapi wanaweza kuafford hiyo?
Mchakato wa hati bado ni mrefu wenye vizingiti vingi, anataka watu wasipojenga wataishije?
Lukuvi aache kutoa matamko, afanye kwanza reform za msingi kwenye sector ya ardhi ndo aje na amri kama hizo alizotoa!
 
Mzee Uzi umeutoa hata kabla sijaanza kuweka msingi maana ndio juzi kati tu nimenunua plot nataka nijenge fasta we unambumburua jamaaa
 
Hiyo kauli tu imeshatengeneza mazingira ya rushwa. Maana mtu ana enelo lake uswahili akianza kujenga wanakuja serikali ya mtaa simamisha ujenzi mpaka uwakatie pesa.

Wakulaumiwa ni serikali kwanini wasipime viwanja matatizo ya panya road , uhuni ,pombe chafu tutazipunguza.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom