Mh. Kikwete, Tundu hatafuti umaarufu wa kisiasa!

Unaona nyie wawili mnavyopingana. Wewe unasema wana digrii na huyu anasema ana diploma.
Wewe hujanielewa na huyo jamaa hajaelewa nini tunakisema hapa.

Huhitaji kuwa na degree ili kuwa hakimu unless kama utaratibu umebadilishwa kipindi hichi, kwani mpaka sasa kuna chuo cha mahakimu Lushoto na watu wako darasani wanasoma hata sasa hivi.

Sasa kama ni hivyo kwa nini jaji kiongozi Mbarook(Siyo jaji mkuu) anasoma Degree ya kwanza hapa OUT na anakiri kuwa anasoma na utawala wa OUT wanakiri ni mwanafunzi wao?
 
Kwa maoni yangu binafsi, hakimu wa wilaya ni jaji. Na kama sio jaji basi hafai kuwa hata hakimu wa wilaya. Kama huyo jamaa alikuwa ni hakimu wa wilaya na amependelewa kuwa jaji basi alipendelewa kuwa hakimu wa wilaya.

maoni yako ni muhimu sana hasa hasa katika kuendeleza na kukuza soko la "wanasheria vichaka" aka bush lawyers. Mungu akuzidishie ufahamu maoni yako yabaki kua mchango kwa familia yako tu, lakini sio taifa hasa lile linalokua.
 
Diploma sio Degree, na sheria inaposema 'degree' haimaanishi 'Diploma'. Na kuna umuhimu gani wa kuwa sheria ambayo haifuatwi? Hao majaji waliokuwa wanaambiwa jinsi majaji wanavyopatikana nao wamechoka kuona taaluma yao inavurugwa. Mahakama ni mhimili muhimu sana kwa ustawi wa jamii, maana inasimamia utoaji HAKI. Kulikuwa na ulazima gani wa kurukia mtu mwenye Diploma na sio Degree kama sheria inavyosema?

Na sasa imeshabainika kuna majaji wasio na sifa, nini kifanyike? Tulaumu walioteuwa, au wenye mamlaka (kwa mujibu wa katiba yetu) wachukue hatua stahiki? Nisingependa mimi binafsi au ndugu yangu siku moja nikiwa na kesi, isikilizwe na jaji asiye na sifa - huko ni kunivunjia haki zangu za msingi za kupata huduma bora kama katiba inavyosema.

Kwani maana ya diploma nini? Mimi ninayo Dip. Judr. Je ni lazima nipate digrii?
 
Ni vitu gani vinakufanya utambue kuwa chuo husika kinatambulika kutoa digrii ya kumfanya mtu awe jaji. Kuna rafiki yangu kasoma Urusi na ni hakimu Tanzania. Je unataka kuniambia kuwa uzoefu wake na digrii yake havitoshi kumfanya awe jaji?

Soma tena hapa na kazia zaidi hapo kwenye bold.

2/Uwe na Degree ya kwanza ya Sheria kutoka katika chuo kikuu chochote duniani inayotambulika na kukubalika na Common Wealth Judiciary System.

Judiciary system ya Urusi ni tofaufi na 'Commonwealth'. Nchi zinafuata Commonwealth judiciary system kwa lugha nyepesi na kwamba sheria zao zina-base kwenye sheria za Uingereza.
 
Kwani maana ya diploma nini? Mimi ninayo Dip. Judr. Je ni lazima nipate digrii?

If you don't maana ya Diploma and/or the difference between a Diploma & Degree then I am afraid I can not help you.
 
Wewe hujanielewa na huyo jamaa hajaelewa nini tunakisema hapa.

Huhitaji kuwa na degree ili kuwa hakimu unless kama utaratibu umebadilishwa kipindi hichi, kwani mpaka sasa kuna chuo cha mahakimu Lushoto na watu wako darasani wanasoma hata sasa hivi.

Sasa kama ni hivyo kwa nini jaji kiongozi Mbarook(Siyo jaji mkuu) anasoma Degree ya kwanza hapa OUT na anakiri kuwa anasoma na utawala wa OUT wanakiri ni mwanafunzi wao?

Nadhani mahakimu wa mahakama ya mwanzo huhitaji degree, lakini district and resident magistrates unahitaji degree ya sheria.
 
Kwanini hatuwezi ku-focus katika issue moja. Issue ni uteuzi wa majaji na mahakama. Ghafla bin vuu tunaanza kutoa mifano ya rushwa.

nataka kuonesha mbinu za JK kujibu hoja. katika Rushwa anakemea. kamaliza. katika hili la majaji, anakejeli, kamaliza
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Zakumi naona waitumia jmosi yako kikatiba kabisa..

ninavyoelewa watoa hoja wanazungumzia kutotimia kwa mojawapo ya vigezo vya mtu kuteuliwa kuwa jaji.

Jaji ni mtu muhimu sana ktk jamii uteuzi wake haupaswi kutiliwa mashaka...majaribio ya kuteua yafanywe kwa wakuu wa mikoa au wilaya sio majaji..
 
Last edited by a moderator:
Ni vitu gani vinakufanya utambue kuwa chuo husika kinatambulika kutoa digrii ya kumfanya mtu awe jaji. Kuna rafiki yangu kasoma Urusi na ni hakimu Tanzania. Je unataka kuniambia kuwa uzoefu wake na digrii yake havitoshi kumfanya awe jaji?
Hata kama ni mme wako kwenye ukweli acha usemwe wakati anachanguliwa kuwa jaji alikuwa na digrii hata kama ni out....
 
Wewe hujanielewa na huyo jamaa hajaelewa nini tunakisema hapa.

Huhitaji kuwa na degree ili kuwa hakimu unless kama utaratibu umebadilishwa kipindi hichi, kwani mpaka sasa kuna chuo cha mahakimu Lushoto na watu wako darasani wanasoma hata sasa hivi.

Sasa kama ni hivyo kwa nini jaji kiongozi Mbarook(Siyo jaji mkuu) anasoma Degree ya kwanza hapa OUT na anakiri kuwa anasoma na utawala wa OUT wanakiri ni mwanafunzi wao?

Kama huhitaji kuwa na digrii kuwa hakimu kwanini jaji atakiwe kuwa nayo?
 
Ivi ni kweli TL hajui kuwa Rais anasoma majina ya maJaji wateule aliyopelekewa na Tume ya Mahakama, majina yanapitiwa na mkuu wao mahakama ndo yanamfikia Mkulu
 
Zakumi naona waitumia jmosi yako kikatiba kabisa..

ninavyoelewa watoa hoja wanazungumzia kutotimia kwa mojawapo ya vigezo vya mtu kuteuliwa kuwa jaji.

Jaji ni mtu muhimu sana ktk jamii uteuzi wake haupaswi kutiliwa mashaka...majaribio ya kuteua yafanywe kwa wakuu wa mikoa au wilaya sio majaji..

Realman:

Natumia haki yangu. Watu wote ni muhimu katika jamii ndio maana katika nchi za wenzetu wamehamua kuwa vigezo vya shule kwa majaji wa ngazi zote ni sawa. Ukiashaanza kufanya kazi kitakachokupandisha juu ni performance yako ya kazi na sio shule tena.
 
Kupitia uzi huu nimejifunza mambo nisiyoyajua,kumbe kikwete ni bomu hivyo?najuta na nitajuta kumpa kura yangu 2005!
 
Hivi jana majaji walichukuliaje kauli ya Kikwete? Nani msemakweli JK au TL?

Majaji wanajua Tundu Lissu anasema kweli maana Kikwete alimteua Jaji Mbaruk wa Zanzibar kuwa Jaji wa mahakama ya rufaa Tanzania wakati hana degree ya kwanza ya sheria kwa mujibu wa katiba inayomtaka jaji kuwa na sifa hiyo kwasabbau Mbaruk degree yake ya kwanza sio sheria ila ana post graduate ya sheria ambayo sio sifa ya mtu kuwa jaji na kwasasa anasoma Open University degree ya kwanza ya sheria kukidhi matakwa ya katiba maana kaumbuliwa tayari. Kuna jaji nafahamiana na mtoto wake kayika maongezi ya kifamilia alisema anamshukuru sana Lissu maa Kikwete alishaanza kuiharibu kada ya sheria kwa kuteua maswaiba na vimada kama ambayo hufanya katika uteuzi wa wakuu wa wilaya na wabunge viti maalumu
 
Kwani digrii ya sheria ya OUT ina tofauti gani na ya UDSM?

we mkuu yaaani huwezi kuwa hata state attoney kama huna first degree ya sheria,yaani huo ujaji aliopewa ni jambo la kushangaza sana,only in Tanzania.
 
mbona wakenya wamewamwaga majaji wote walio patikana kinyume na talatibu? kenya wawepo majaji vilaza tz ndo ishindikane? Itakuwa ajabu sana.
 
Kwani digrii ya sheria ya OUT ina tofauti gani na ya UDSM?

Wewe zakumi nawasiwasi sana na uwezo wako wa kufikiri,kinachozungumziwa hapa c degree ya udsm au out,kinachozungumziwa ni 1st degree inayomfanya mtu aqualify kuwa jaji.sasa kuna jaji ameteuliwa hata 1st degree hana ndio kwanza anasoma out.acha kudandia gari kwa mbele.
 
Majaji wanajua Tundu Lissu anasema kweli maana Kikwete alimteua Jaji Mbaruk wa Zanzibar kuwa Jaji wa mahakama ya rufaa Tanzania wakati hana degree ya kwanza ya sheria kwa mujibu wa katiba inayomtaka jaji kuwa na sifa hiyo kwasabbau Mbaruk degree yake ya kwanza sio sheria ila ana post graduate ya sheria ambayo sio sifa ya mtu kuwa jaji na kwasasa anasoma Open University degree ya kwanza ya sheria kukidhi matakwa ya katiba maana kaumbuliwa tayari. Kuna jaji nafahamiana na mtoto wake kayika maongezi ya kifamilia alisema anamshukuru sana Lissu maa Kikwete alishaanza kuiharibu kada ya sheria kwa kuteua maswaiba na vimada kama ambayo hufanya katika uteuzi wa wakuu wa wilaya na wabunge viti maalumu

Nchi nyingi siku hizi hazitoi digrii ya kwanza ya sheria. Kwa hiyo hata hao majaji watanzania itabidi waangalie upya.
 
Back
Top Bottom