lazima tumshukuru Julius Nyerere kwa kumkataa mtu huyu, bado ukimfikiria anavyoshiriki kuturudisha nyuma hadi roho inaumaHuyu jamaa alichaguliwa ili akale bata na maswahiba wake pale magogoni na si kuiongoza nchi,PONDA RAHA KUFA KWAJA wananchi watajijua wenyewe na njaa zao.
Kama Jakaya ni kijana na vijana utawaitaje?Mwacheni kijana wa watu!! Kutwa kawajaa midomoni jakaya jakaya lol!!
Duh avator yako kali!Ni zama tu watanzania tunakwenda kwa matukio sana. Si Mhe. Mwinyi tulimkubali alipokuwa madarakani, wala Mwl Nyerere wala Mkapa (hakupenda sana uheshimiwa na utukufu). Sasa anayebisha na aseme sasa. Kikwete akiondoka itakuwa kila siku aheri ya jana. Tufikirie kwa tathmini na siyo kama watoto wadogo wakipewa peremende wanasahau yoote wanaanza upya. Nawakilisha.
Mara kumi Lowassa kuliko huyu m.k.w.e.r.e. hivi nyie mnaona tuna mtu/kitu pale?Mi bado naitafakari hii ardhi yetu alivyokomalia kuiuza na bado amekuwa dalali huko ulaya, katikati ya hali hii ya uchumi wa dunia!... Afadhali angeingia mwaka 95, maana tungeshirikiana na Baba wa Taifa Mzee Nyerere kumtoa hata baada ya miaka 2 tu ya kukaa magogoni, ila kwasasa hamna wa kumzuia anaiweka nchi rehani anapiga misele dunia nzima, familia yake ndio usiseme. Wananchi watz kama tumekula tambuu, tunamchekea tu!
Namfikiria Mh. Kikwete , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mzaliwa wa Msoga , hivi angeshinda uchaguzi wa mwaka 1995 na kuwa Rais wa Tanzania katika hali ya uchumi legelege kama alivyoiacha Mzee Mwinyi , Je angeweza kutuvusha salama kwa miaka kumi kama ambavyo Mkapa aliweza ? Kikwete asingeweza kuwa na Mbinu za kutuendeleza ma kuinua uchumi wetu.
Huyu ndie Rais ambaye kashindwa kuwa na mtizamo chanya juu ya kuiendeleza Tanzania kutoka pale ambapo Mzee Mkapa aliishia .
Alikabidhiwa nchi iliyokuwa na Macro Economy Imara sana, leo tumeanza kurejea kulekule tulikotoka, ambapo inahisiwa kuwa kufikia mwishoni mwa Utawala wake Uchumi wetu utakua Kaputi kukaribiana na uchumi wa Zimbambwe .
hivi amerudi nasikia ameenda kujinunulia suti mpya ?
Mwacheni kijana wa watu!! Kutwa kawajaa midomoni jakaya jakaya lol!!