Mh. Kikwete bora ulishindwa 1995

Status
Not open for further replies.

nguvumali

JF-Expert Member
Sep 3, 2009
4,923
1,325
Namfikiria Mh. Kikwete , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mzaliwa wa Msoga , hivi angeshinda uchaguzi wa mwaka 1995 na kuwa Rais wa Tanzania katika hali ya uchumi legelege kama alivyoiacha Mzee Mwinyi , Je angeweza kutuvusha salama kwa miaka kumi kama ambavyo Mkapa aliweza ? Kikwete asingeweza kuwa na Mbinu za kutuendeleza ma kuinua uchumi wetu.

Huyu ndie Rais ambaye kashindwa kuwa na mtizamo chanya juu ya kuiendeleza Tanzania kutoka pale ambapo Mzee Mkapa aliishia .

Alikabidhiwa nchi iliyokuwa na Macro Economy Imara sana, leo tumeanza kurejea kulekule tulikotoka, ambapo inahisiwa kuwa kufikia mwishoni mwa Utawala wake Uchumi wetu utakua Kaputi kukaribiana na uchumi wa Zimbambwe .
 
Angetufanya tutumie nguvu nyingi ili kuleta mali kidogo. Asingefaa kamwe.
 
Kama kakuta hali ya uchumi ya namna ile na yeye kashindwa kupiga hata hatua 2 mbele, kwakweli naamini kweli Nyerere alikua kiona mbali kumkataa na kuwashawishi wale NEC ya ccm kumkataa huyu jamaa, angetuingiza shimoni huyu jamaa wa Msogo, asingeweza kujenga uchumi mpana wala Micro economy.
 
Nyerere aliposema hajakomaa alimaanisha kuwa hakuwa na uweazo wa kuongoza taifa................................aliwakataa akina lowasa wao waliingia kwa mbinu na jeuri ya fedha mara mzimu wa mwalimu ukawakumba................uliza leo lowasa yuko wapi?

Mbwembwe tu mitaani na kutoa matamko km vile watz wote ni mauzuz kwamba wako tayari kumsikiliza upuuzi wake.......................kikwete alikataliwa kwani kiongozi bora huonekana tangu mwanzo.

Kama ni watoto basi kikwete na lowasa sio riziki na sasa tunategemea miujiza ili tusiendelee kuzama zaidi kwenye tope lililokorogwa na kikwete na lowasa na Rostamu
 
Mi bado naitafakari hii ardhi yetu alivyokomalia kuiuza na bado amekuwa dalali huko ulaya, katikati ya hali hii ya uchumi wa dunia!... Afadhali angeingia mwaka 95, maana tungeshirikiana na Baba wa Taifa Mzee Nyerere kumtoa hata baada ya miaka 2 tu ya kukaa magogoni, ila kwasasa hamna wa kumzuia anaiweka nchi rehani anapiga misele dunia nzima, familia yake ndio usiseme. Wananchi watz kama tumekula tambuu, tunamchekea tu!
 
Ndugu yangu hii ndo nchi pekee ya raia mabwege..........................tunakodoa tu mimacho na kulalamnika.....na jamaa anatucheka kishenzi yani
mi bado naitafakari hii ardhi yetu alivyokomalia kuiuza na bado amekuwa dalali huko ulaya, katikati ya hali hii ya uchumi wa dunia!... Afadhali angeingia mwaka 95, maana tungeshirikiana na baba wa taifa mzee nyerere kumtoa hata baada ya miaka 2 tu ya kukaa magogoni, ila kwasasa hamna wa kumzuia anaiweka nchi rehani anapiga misele dunia nzima, familia yake ndio usiseme. Wananchi watz kama tumekula tambuu, tunamchekea tu!
 
Namfikiria Mh. Kikwete , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mzaliwa wa Msoga , hivi angeshinda uchaguzi wa mwaka 1995 na kuwa Rais wa Tanzania katika hali ya uchumi legelege kama alivyoiacha Mzee Mwinyi , Je angeweza kutuvusha salama kwa miaka kumi kama ambavyo Mkapa aliweza ? Kikwete asingeweza kuwa na Mbinu za kutuendeleza ma kuinua uchumi wetu.

Huyu ndie Rais ambaye kashindwa kuwa na mtizamo chanya juu ya kuiendeleza Tanzania kutoka pale ambapo Mzee Mkapa aliishia .

Alikabidhiwa nchi iliyokuwa na Macro Economy Imara sana, leo tumeanza kurejea kulekule tulikotoka, ambapo
inahisiwa kuwa kufikia mwishoni mwa Utawala wake Uchumi wetu utakua Kaputi kukaribiana na uchumi wa Zimbambwe .

Inahisiwa?
 
hana la kusema kuhusu uchumi, shilingi imeshuka thamani hata wanyama ambao sura zao ziko kwenye noti wana mpango wa kuandamana sura zao ziondolewe kwani wanazalilishwa. Wanasema ni bora zingewekwa kwenye toilet paper kuliko kwenye noti ya Tz
 
Mwalimu Nyerere alisema ili nchi iweze kuendelea ni lazima kuwepo vitu vinne,ARDHI,WATU,SIASA SAFI na UONGOZI BORA.Sasa hapa tuna watu wa kutosha na ardhi iliobarikiwa na Mungu kwani ina utajiri wa kupindukia tatizo ni SIASA ZA MAJI TAKA NA UONGOZI MBOVU.Nawasihi watanzania wenzangu tumuenzi BABA WA TAIFA kwa kuchagua Viongozi BORA na sio SURA NZURI,DINI,PESA,UKANDA na pia tuwe wazalendo.Yote haya yanayotupata yanatokana na kuyapuuza yale ya HAYATI MWL JK.NYERERE.
 
Huyu jamaa alichaguliwa ili akale bata na maswahiba wake pale magogoni na si kuiongoza nchi,PONDA RAHA KUFA KWAJA wananchi watajijua wenyewe na njaa zao.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom