Mh. Kikwete bora ulishindwa 1995

Mh. Kikwete bora ulishindwa 1995

Status
Not open for further replies.
Huyu jamaa alichaguliwa ili akale bata na maswahiba wake pale magogoni na si kuiongoza nchi,PONDA RAHA KUFA KWAJA wananchi watajijua wenyewe na njaa zao.
lazima tumshukuru Julius Nyerere kwa kumkataa mtu huyu, bado ukimfikiria anavyoshiriki kuturudisha nyuma hadi roho inauma
 
Alichosema Nyerere ni kwamba mtu anataka urais wa nchi yetu tukimwangalia usoni tuamini kuwa ni kweli anakerwa na matatizo yetu. Je tulizingatia hilo? Nyerere aliendelea kusema kuwa tusichague Rais kwa kuangalia uzuri wa sura, ' kama mkimpenda mtu kwa sura yake mchukueni mkanywe nae chai lakini si Urais' Nyerere bana!
 
Ni zama tu watanzania tunakwenda kwa matukio sana. Si Mhe. Mwinyi tulimkubali alipokuwa madarakani, wala Mwl Nyerere wala Mkapa (hakupenda sana uheshimiwa na utukufu). Sasa anayebisha na aseme sasa. Kikwete akiondoka itakuwa kila siku aheri ya jana. Tufikirie kwa tathmini na siyo kama watoto wadogo wakipewa peremende wanasahau yoote wanaanza upya. Nawakilisha.
 
Ni zama tu watanzania tunakwenda kwa matukio sana. Si Mhe. Mwinyi tulimkubali alipokuwa madarakani, wala Mwl Nyerere wala Mkapa (hakupenda sana uheshimiwa na utukufu). Sasa anayebisha na aseme sasa. Kikwete akiondoka itakuwa kila siku aheri ya jana. Tufikirie kwa tathmini na siyo kama watoto wadogo wakipewa peremende wanasahau yoote wanaanza upya. Nawakilisha.
Duh avator yako kali!
 
kumbuka mwl nnyerere alimkataa si udogo wake bali alimjua mcheka hovyo vyema na madhara yake kwa taifa changa kama Tanzania.lakini baada ya kifo chake, kawekwa magogoni kaonesha alivyo hodari wa kuchekacheka hadi kwenye misiba na kwenda kuuza sura na G-UNIT
 
Mi bado naitafakari hii ardhi yetu alivyokomalia kuiuza na bado amekuwa dalali huko ulaya, katikati ya hali hii ya uchumi wa dunia!... Afadhali angeingia mwaka 95, maana tungeshirikiana na Baba wa Taifa Mzee Nyerere kumtoa hata baada ya miaka 2 tu ya kukaa magogoni, ila kwasasa hamna wa kumzuia anaiweka nchi rehani anapiga misele dunia nzima, familia yake ndio usiseme. Wananchi watz kama tumekula tambuu, tunamchekea tu!
Mara kumi Lowassa kuliko huyu m.k.w.e.r.e. hivi nyie mnaona tuna mtu/kitu pale?
 
Kwa taarifa yako Uchumi wa zimbabwe na fujo zote zile kwa sasa uko juu zaidi ya nchi yoyote unayoifahamu East Africa.Ukiwa unatoa hoja ujitahidi kuwa na Takwimu sahihi.Nadhani wewe ni mshabiki na mfuatiliaji wa propaganda za BBC kwa hilo sikulaumu sana.
Hoja yako inamashiko ila umekosa mifano hai kuweka mkazo/nguvu hoja ya msingi.
Namfikiria Mh. Kikwete , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mzaliwa wa Msoga , hivi angeshinda uchaguzi wa mwaka 1995 na kuwa Rais wa Tanzania katika hali ya uchumi legelege kama alivyoiacha Mzee Mwinyi , Je angeweza kutuvusha salama kwa miaka kumi kama ambavyo Mkapa aliweza ? Kikwete asingeweza kuwa na Mbinu za kutuendeleza ma kuinua uchumi wetu.

Huyu ndie Rais ambaye kashindwa kuwa na mtizamo chanya juu ya kuiendeleza Tanzania kutoka pale ambapo Mzee Mkapa aliishia .

Alikabidhiwa nchi iliyokuwa na Macro Economy Imara sana, leo tumeanza kurejea kulekule tulikotoka, ambapo inahisiwa kuwa kufikia mwishoni mwa Utawala wake Uchumi wetu utakua Kaputi kukaribiana na uchumi wa Zimbambwe .
 
Mwacheni kijana wa watu!! Kutwa kawajaa midomoni jakaya jakaya lol!!

Duh! Hivi kijana ni mtu mwenye umri gani au kati ya miaka mingapi? Kama jk kijana basi mie mtoto! Kama unmhurumia kanywe nae chai! Baba wa Taifa alisema kama unaona mzuri ...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom