Mh. Job Ndugai, salamu kwako,
Ukiwa kama mkuu wa mojawapo ya mihimili mikuu ya mfumo wa uendeshaji nchi (Bunge, Serikali na Mahakama), ningependa kukusihi utafute muda utafakari, ungependa ukumbukweje na vizazi vijavyo kuhusu utendaji wako kama Spika wa Bunge katika kipindi chako hiki cha sasa.
Kuna njia kadhaa za kufanya hivyo, mojawapo ni kurudi nyuma kwenye historia na kuwatazama wenzako waliopita (Mzee Pius Msekwa, Marehemu Samuel Sitta na mwishoni hapa Mama Anna Makinda) kwa jinsi gani unadhani wanakumbukwa kutokana na utendaji wao.
Sitaki nitoe hukumu leo kwa utendaji wako wa sasa, ila ningependa wewe mwenyewe ujilinganishe na hao waliopita na kisha uamue ungependa legacy yako iwe ya namna gani.
Una fursa kubwa na nzuri sana ambayo wengi wangetamani kuwa hapo ulipo wewe ili wajenge legacy, ambayo hatimaye itakuja kukumbukwa na vizazi vijavyo katika siku za usoni.
Uamuzi ni wako, unataka ukumbukwe kwa lipi?