Mh. Job Ndugai, ungependa ukumbukwe kwa lipi utakapomaliza kipindi chako?

Mchanya

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
788
1,000
Mh. Job Ndugai, salamu kwako,

Ukiwa kama mkuu wa mojawapo ya mihimili mikuu ya mfumo wa uendeshaji nchi (Bunge, Serikali na Mahakama), ningependa kukusihi utafute muda utafakari, ungependa ukumbukweje na vizazi vijavyo kuhusu utendaji wako kama Spika wa Bunge katika kipindi chako hiki cha sasa.

Kuna njia kadhaa za kufanya hivyo, mojawapo ni kurudi nyuma kwenye historia na kuwatazama wenzako waliopita (Mzee Pius Msekwa, Marehemu Samuel Sitta na mwishoni hapa Mama Anna Makinda) kwa jinsi gani unadhani wanakumbukwa kutokana na utendaji wao.

Sitaki nitoe hukumu leo kwa utendaji wako wa sasa, ila ningependa wewe mwenyewe ujilinganishe na hao waliopita na kisha uamue ungependa legacy yako iwe ya namna gani.

Una fursa kubwa na nzuri sana ambayo wengi wangetamani kuwa hapo ulipo wewe ili wajenge legacy, ambayo hatimaye itakuja kukumbukwa na vizazi vijavyo katika siku za usoni.

Uamuzi ni wako, unataka ukumbukwe kwa lipi?
 

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,743
2,000
Labda anataka kukumbukwa kwa ubabe wa kutumia askari bungeni kuwanyanyasa wabunge wa upinzani
 

Man Thom

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
716
1,000
Hivi katiba yetu inasemaje kuhusu kuwa na spika asiyefungamana na chama chochote, Jaji Joseph Sinde Warioba sio mnafiki, ni mpenda haki, na siku akiondoka atakumbukwa kwa mengi sana! Ni wakati wetu sasa kudai mabadiliko ya katiba ili tuepukane na huu ubabe unaofanywa na hawa wanaojiona kama hii nchi ni ya kwao peke yao!
 

jaji mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
9,835
2,000
JUZI; ACACIA hawa ni wezi, hawana leseni ya kuchimba madini nchini, hawana usajili, hatuwezi kuwalinda kwa askari wetu wezi wanaotuibia hawa.., hakuna mchanga kutoka nje.., ni wezi.

JANA; mimi kama mbunge wa eneo hilo, sasa natoa Rai kwa wananchi wangu, kuhakikisha tunazuia hawa wezi wa ACACIA wasituibie tena, tunakwenda kuzuia madini uetu yasisafirishwe.

LEO; HAPANA.., huyu mbunge ni mchochezi.., akamatwe na aunganishwe kwenye watu wenye vurugu, anahatarisha usalama wa nchi, anawasumbua wawekezaji.., akamatwe!!

#My_Take; Muombe Mungu kila siku.., usipewe ubongo na akili kama za ndugu zetu wa CCM.., ni laana, sasa ndugu zetu ndio wamebeba tafsiri sahihi ya neno "matumizi mabaya ya akili za binadamu", hawajui hata wanataka nini, kama bendera kavu tu, wanapepea!
 

Mkumbwa Jr

JF-Expert Member
Mar 23, 2016
1,465
2,000
Atakumbukwa kama msomi mfukua kaburi na anaeringa kumiliki kikosi cha askari wasiozidi kumi
 

Planett

JF-Expert Member
Mar 20, 2014
8,706
2,000
angependa akumbukwe kwa kujeruhi na kuzimisha mtu wakati wa campaign
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom