Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 2,169
- 10,464
Siasa za dijitali, siasa za mitandaoni, siasa za Instagram, siasa za uchawa.
Ukiwa na akili timamu huwezi kushabikia siasa za Makonda na umapepe wake wa kulazimisha kukubalika Kila pembe ya nchi.
Makonda ni moja ya viongozi wachapakazi sana ila tatizo lake ni moja Kila anachokifanya anataka Dunia nzima ijue. Kwangu huu nauita ni ulimbukeni na ushamba.
Humphrey Polepole miongoni mwa waliomkubali na kukubalika na hayati Magufuli naye ni wale wenye siasa za kupenda kuonekana mbele, yaani wao kwanza kuliko maslahi ya taifa.
Shaka Hamdu Shaka
Huyu Naye alikuja na Kasi fulani hivi wao hutaka waitwe wachapakazi lakini ukweli ni kujiweka front ili tu kuongeza curriculum vitae kwa masilahi yao.
Lengai Sabaya
Huyu nisiongee sana wengi wanajua, umri wake tu ulionesha namna alivyomjinga kwa kutaka engagement kubwa kwa kuumiza baadhi ya raia wake kwa kisingizio chake cha kutanguliza masilahi ya nchi.
Wengine ni Albert Chalamila homeboy, Kenan kihongosi, Ally Hapi,
Ni wachapakazi haswa ila tatizo hawana utulivu.
Wapo wengi wanaojiita machawa wenye vyeo na wasio na vyeo jambo ambalo huenda serikali ni kama imebariki.
Pamoja na yote hayo wapo vijana wengi tu Wana siasa nzuri sana miongoni mwa hao ni Dotto Biteko.
Alionekana ni sukumagang kwa mujibu wa mgawanyo kwenye chama cha mapinduzi, alitabiriwa kushindwa au kuachwa kwenye hii serikali ya mama lakini bado kijana anadunda.
Utulivu wake, kufanya kazi kwenye eneo lake bila kujipendekeza, kumefanya afike alipo, ni naibu waziri mkuu ,pia ni waziri wa nishati.
Yanazungumzwa mengi kwamba huenda nafasi alizopewa ni mtego lakini ukweli huyu ni hazina kubwa kwenye hii nchi. Nina Imani naye huyu jamaa.
NB; hakuna binadamu aliyekamilika, jamaa ana mapungufu yake kama ilivyo kwa yeyote yule.