MH BONIFACE JACOB AENDELEA KUCHANJA MBUGA KWA KASI ZAIDI YA ROCKETI

chuuma

JF-Expert Member
May 19, 2015
363
557
Siku ya leo april 22, Mh Boniface amefanikiwa kutembelea vikundi mbalimbali katika manispaa ya kinondoni akiwa katika zoezi la kuwagawia hundi za mikopo ili wananchi hao wawezi kujikwamua kiuchumi hii ni dhahiri kuwa mh Boniface yupo tayari na anafurahia kuona wananchi wake wanajikwamua kiuchumi.

Mojawapo ya vikundi vilivyotembelewa na mstahiki meya Boniface Jacob ni
Kikundi cha akina mama wanaojishughulisha na ushonaji wa nguo, saloon na mama lishe Kigogo-Mbuyuni ambapo aliwakabidhi hundi ya milioni 7.7

Kikundi cha akina mama kinachojishughulisha na uuzaji wa samaki na mama lishe Kimara - Kilingule B ambapo amekabidhi hundi ya tsh Milioni 3
 
Akigawa kiongozi wa ccm ungesikia nyumbu humu wakisema ni rushwa,lakini hongera Jackobo kwa jitihada hizo.
 
kama nchi hii ingekuwa na viongozi wa namna hii basi kila mtanzania angekuwa na maisha bora. Mimi mpaka leo najiuliza yale mabilioni ya Mzee jakaya yalipitia wapi!

Haya tunazingojea ml 50 kwa kila kata ambazo kwa mujibu wa serikali kupitia waziri wa fedha bw mpango wameaidi kuanzia mwakani yataanza kugawiwa. Sasa sijui na hizi zitaingia mifukoni mwawajanja kama za mzee yakaya!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom