Mahawanga Janeth akamilisha zoezi la usajili wa vikundi kwa wanawake wagonga kokoto, Kunduchi

PendoLyimo

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
879
956
Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Dar es Salaam Mahawanga Janeth amekabidhi vyeti vya usajili na uandikishwaji wa vikundi saba (07) vya wanawake kutoka mitaa tofauti wanaojishughulisha na kugonga kokoto katika Kata ya Kunduchi sambamba na kuwafungulia akaunti za Benki kwa ajili ya kukamilisha zoezi zima la kupata mkopo.

Mh Mahawanga katika ziara yake aliyoifanya tarehe 08/10/2022 kwenye mitaa mbalimbali iliyopo kwenye Kata ya Kunduchi aliguswa sana na wanawake ambao wanapasua kokoto kwa kutumia mikono na kujipatia fedha kidogo ambazo hazitoshelezi kwa matumizi binafsi hivyo akaona ni vyema kuwapa elimu ya Vikundi, usajili wa vikundi, sambamba na fursa ya mikopo.

Hivyo alihakikisha elimu hiyo inaeleweka na kuungana nao kutengeneza Vikundi, kuvisajili na kuungana na Benki ya CRDB kuhakikisha amevifungulia akaunti kupitia Benki hiyo ya CRDB vikundi vyote sita kimoja kikiwa nicha Vijana wenye Ulemavu ambao nao wanafanya shughuli za kugonga kokoto.

Mh. Mahawanga amewaahidi kuwa hatua ya mwisho ameishaitekeleza ambayo ni kuandaa maandiko ya miradi kwa ajili ya Vikundi hivyo ili kupata mikopo ya asilimia 10% inayotolewa kwenye kila Halmashauri kuhakikisha wanapata mikopo hii ili waweze kujikwamua kiuchumi kama jinsi ilivyo dhamira yake ya kumkomboa Mwanamke wa Dar kiuchumi.

Aidha amewashukuru sana Benki ya CRDB kwa kukubali kujumuika nao kutoka Ofisini na kuja kuwafata akina mama hao ili kuwafungulia akaunti lakini pia amewapongeza wanawake wote waliojitokeza kwa namna ambavyo wameendelea kushirikiana naye na kusisitiza ataendelea kuwapamoja nao mpaka kuhakikisha lengo kuu la kumkwamua mwanamke kiuchumi linafanikiwa.

Pia amempongeza sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo anaendelea kufanya kazi kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo na amesisitiza kuendelea kumuunga mkono kwa kuhakikisha anatekeleza vyema Ilani ya CCM 2020/25 hasa kwenye suala la kuwainua wanawake kiuchumi kupitia mikopo ya Halmashauri na wadau mbalimbali wa maendeleo.

#TishaMama
#ItazameDarKiutofauti


IMG-20220104-WA0269.jpg
 
Suala la microfinance Hilo eneo nilifanya Sana miaka 10 iliyopita...hao akina mama sio wageni kwenye mikopo Ni wazoefu wa zaidi ya miaka 15 wanakopa. Mwanzoni wanarudisha vizuri mbele ya Safari mziki wake si kitoto.....hizo pesa labda awape inform of grants au fund tu kuwasaidia. Au muhusika labda Ana malengo mengine ya kugombea ubunge etc .

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom