Mh. Beatrice Shelukindo aeleza ukweli kuhusu posho

Brightman Jr

JF-Expert Member
Mar 22, 2009
1,225
232
Akihojiwa na Othman Miraji wa Deutsche Welle Mh. Shelukindo amekiri kuwa ni kweli mpango wa kuongezwa posho ya Tsh.200,000/=ulifanyika kutokana na ugumu wa maisha ya mjini Dodoma. Akiri rais kukataa kusaini ombi la posho hizo. Na kusisitiza kuwa si kweli kwamba wameanza kulipwa. Amesema tume ya kuangalia upya posho hizo itakutana jumamosi. Haya wadau nafikiri kweli posho hizo bado hazijaanza kutolewa kutokana na kauli za watu zaidi ya wawili kukataa kuwa posho bado. Mwasemaje wanaJf?
 
Kwa hiyo nani mkweli nani muongo!! Yaani hata SPIKA atakuwa haaminiki!!! Haya bana tumeyazoea haya mazingaombwe!!
 
Hivi wanao miliki hizo hoteli tunazoambiwa zinachaji Tsh 100,000 per night si hao hao waheshmiwa?
 
Sasa naanza kuwa na wasiwasi na usikivu wa masikio yangu kama si uelewa wangu, kwenye ile taarifa ya habari ya saa Mbili usiku ITV nilimwona na kumsikia huyu bibi Nanihii akitamka pamoja na mambo mengine kwamba hizi posho zilianza kulipwa kwenye mkutano ulioisha na kwamba Zitto Kabwe hakuweza kupewa kwasababu ya kanuni zinazotoa sifa ya kuzipata ni lazima Mbunge awe amesaini asubuhi na jioni wakati huo Zitto asingeweza kwani hakuwepo. Leo hii huyu Shelukundu anatwambia tofauti. Je tumwamini nani!
 
Kama posho zinaongezewa kwa sababu maisha Dodoma yamepanda, na je hao wanaoishi Dodoma miaka yote, "posho" na mishahara yao imepnda lini?
 
Watu mtaishi kwa woga hadi lini muelimike jamani, marais wenye heshima zao duniani huwa wanaitwa majina ya ajabu ajabu na kuchorwa juu sembuse huyu kiroboto, kama vipi waambie wani PM mimi.

mfano rais gani anaitwa jina la ajabu...?

"ᵀᴴᴱ'ᴼᴿᴵᴳᴵᴻᴬᴸ✯

eti shelukindo kaulizwa kasema asilimia 300 ni kidogo mpaka mtangazaji kashangaa,anataka kufananisha eti we mtangazaji unalipwa bei gani huko ujerumani? hao ndio wabunge tulio nao
 
Hawa viongozi wetu ni kama wamelogwa.Suala la mawasiliano kwao ni kidonda ndugu,KASHILILA anasema hawajalipwa, Bibi kidude anasema wamelipwa!!.Sasa tumuamini nani kati ya Brot her KASH na Bi. Kidude?
 
Akihojiwa na Othman Miraji wa Deutsche Welle Mh. Shelukindo amekiri kuwa ni kweli mpango wa kuongezwa posho ya Tsh.200,000/=ulifanyika kutokana na ugumu wa maisha ya mjini Dodoma. Akiri rais kukataa kusaini ombi la posho hizo. Na kusisitiza kuwa si kweli kwamba wameanza kulipwa. Amesema tume ya kuangalia upya posho hizo itakutana jumamosi. Haya wadau nafikiri kweli posho hizo bado hazijaanza kutolewa kutokana na kauli za watu zaidi ya wawili kukataa kuwa posho bado. Mwasemaje wanaJf?

Huyu spika ni kimeo wakuu....nadhani kuna haja ya kumfanyia uchunguzi wa kina kwenye akili zake,anaendesha bunge kama nyumba yake vile..anajiona ana mamlaka makubwa sana kuliko viongozi wengine wa bunge na wabunge shit!!
 
nashauri badala ya kuwapa posho wabunge ni bora zikajengwa hostel za bunge halafu wakawekewa mpishi.
kwa upande mwingine inabidi tuanze kukagua matumizi ya posho hizo kama zinatumika kulingana na makusudio yake.
 
Sasa naanza kuwa na wasiwasi na usikivu wa masikio yangu kama si uelewa wangu, kwenye ile taarifa ya habari ya saa Mbili usiku ITV nilimwona na kumsikia huyu bibi Nanihii akitamka pamoja na mambo mengine kwamba hizi posho zilianza kulipwa kwenye mkutano ulioisha na kwamba Zitto Kabwe hakuweza kupewa kwasababu ya kanuni zinazotoa sifa ya kuzipata ni lazima Mbunge awe amesaini asubuhi na jioni wakati huo Zitto asingeweza kwani hakuwepo. Leo hii huyu Shelukundu anatwambia tofauti. Je tumwamini nani!

Shelukindo, Mbunge wa Kilindi, mkoa wa Tanga.

eti shelukindo kaulizwa kasema asilimia 300 ni kidogo mpaka mtangazaji kashangaa,anataka kufananisha eti we mtangazaji unalipwa bei gani huko ujerumani? hao ndio wabunge tulio nao

Mkuu kumbe nawe umempata? Kwenye point hiyo Mtangazaji akampiga chenga ya mwili asitake kutaja anapokea ngapi kwa kurusha kipindi kimoja hewani! Du...!
 
Watu mtaishi kwa woga hadi lini muelimike jamani, marais wenye heshima zao duniani huwa wanaitwa majina ya ajabu ajabu na kuchorwa juu sembuse huyu kiroboto, kama vipi waambie wani PM mimi.

Mkuu, nimeipenda! Manake kulikuwa na Mtanganyika ambaye yuko Marekani, alipoulizwa kuhusu Tanganyika ndani ya muungano alikuwa Mwoga hadi akafikia kuuma maneno na kushindwa kueleweka ana msimamo gani! lakini alipoulizwa mZenj, bila kujiuma ameeleza kwamba waTg kama hawaitaki Tg wao wazenj haiwahusu maadam Zenj inatambuliwa! Leo huyo mama mbunge anatetea posho wakati anaelewa wazi matumizi ya serkali ni makubwa kuliko wanachozalisha hata huko bungeni! Hivi kweli hawaoni gharama ya kuwahudumia watawala wa jamhuri ya zenj? Vunjeni muungano muone kama hamkupata posho zaidi ya hiyo! Mmebakia kukamua Beberu mkifikiri ana maziwa!
 
Anne Kilango Malecela,Samwel Sitta,Christopher Ole Sendeka,John Pombe Magufuli,Nape Nnauye,John Shibuda na Beatrice Shelukindo...Wote hawa nawafananisha na simba jike aliyejeruhiwa....Dhamira zao za ndani zmejaa chuki,visasi,woga na unafiki....Hawafai hta kdogo
 
Sasa naanza kuwa na wasiwasi na usikivu wa masikio yangu kama si uelewa wangu, kwenye ile taarifa ya habari ya saa Mbili usiku ITV nilimwona na kumsikia huyu bibi Nanihii akitamka pamoja na mambo mengine kwamba hizi posho zilianza kulipwa kwenye mkutano ulioisha na kwamba Zitto Kabwe hakuweza kupewa kwasababu ya kanuni zinazotoa sifa ya kuzipata ni lazima Mbunge awe amesaini asubuhi na jioni wakati huo Zitto asingeweza kwani hakuwepo. Leo hii huyu Shelukundu anatwambia tofauti. Je tumwamini nani!

ha ha ha ha Lukund haswaa
 
Anne Kilango Malecela,Samwel Sitta,Christopher Ole Sendeka,John Pombe Magufuli,Nape Nnauye,John Shibuda na Beatrice Shelukindo...Wote hawa nawafananisha na simba jike aliyejeruhiwa....Dhamira zao za ndani zmejaa chuki,visasi,woga na unafiki....Hawafai hta kdogo

Mkuu tunajadili ''ukweli'' kuhusu poshooo......! tuliza jazba!
 
Back
Top Bottom