Mgongano wa Utawala Wilaya Ileje, Mkurungenzi aliyehamishwa Bi Grady Ndyamvunye ameitwa kujieleza!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgongano wa Utawala Wilaya Ileje, Mkurungenzi aliyehamishwa Bi Grady Ndyamvunye ameitwa kujieleza!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KING COBRA, Jul 17, 2012.

 1. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Mapema Mwezi wa tano Mwaka huu Mweyekiti wa baraza la Madiwani Ileje Mh Mohamed Mwala aliitisha kikao Cha madiwani kilichopelekea Kumukataa Mkurungenzi mpya wa Wilaya na kumupendekeza Afisa mfugo wa Wilaya aitwaye Dk Kasanga kushika nafasi ya Mkurungenzi mtendaji.

  Tuhuma za Mkurungenzi mpya Bi Sylivia Siriwa zilikuwa ni :
  1.Kuiletea Halimashauli Madeni hewa zaidi ya 1.2bils
  2.Kushindwa kudhibiti Jaribio la wizi wa 86,000,000/= kupitia NMB
  3.Kumudharau Mwenyekiti.


  Hata hivyo imebainika kuwa madeni hewa yalisababishwa na utawala uliopita na mkurungenzi mpya ameyakuta na kukabidhiwa na kamati ya fedha ya Wilaya.

  Suala la Jaribio la Wizi lilizuiwa na Bi Syliwa Siriwa kwa kupiga simu kwa meneja Benki NMB na kuamuru wahusika wakamatwe. Hata hivyo wizi huo ulipangwa na Wazawa na kumuzunguka Mkurungenzi wakati yeye akiwa safari.

  Watendaji katika vitengo Wilaya ya Ileje wana lalamika kuwa kuna ubaguzi wa Ukabila na Uzawa ambapo watendaji kutoka katika maeneo mengine nje ya Ileje wanashambuliwa vibaya na kwamba wapo watu wano tuma majungu serikali kuu juu ya Watendaji wasio wazawa wa Ileje ili waondolewe na nafasi hizo kuchukuliwa na Wazawa.

  Pia imebainika kuwa Migogoro ya Ileje imetokana na baadhi ya watendaji ambao walishindwa katika kura za maoni CCM 2010 na baadaye wakateuliwa na Serikali kuongoza .

  Wanatolea mfano Dkt Kassanga alishindwa na Mhe Job Ndugai kura za maoni CCM na sasa anafanya siasa kumutoa Mkurungenzi wakatin yeye mwenyewe anatuhuma za kuiba pesa za kuchimba mabwawa Ileje.  Kufuatia Mgogoro huu , Mkurungenzi Ileje Bi Syliwa Siriwa ameachwa aendelee na Kazi na badala yake Mkurungenzi wa Zamani Bi Grady aliyehamishiwa Lindi ameitwa kujibu tuhuma na ameingia Ileje jumapili!!!!.

  Inavyo onyesha Wanasiasa wanahaha utawala 2015
   
 2. L

  Lindongo Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Rekodi ya Ileje inaonyesha kuwa wakurugenzi ambao sio wazawahawatakiwi, kwa muda mrefu Wazawa ndio waliongoza halmashauri hiyo eg. Shimwela aliyeyopo Sumbawanga MC na Shimwela aliyepo Mufindi DC. Suala la ukabila limekithiri kwenye LGA, na lugha za huyu ni mwenzetu na huyu sio mwenzetu na kitu cha kawaida kwenye council nyingi. watu wasio na makosa ndio wantolewa kafala na wenye makosa wanalindwa. hii ndio Local Government.
   
 3. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Huyo Simwela Wa Mufindi naye ameanza kufukuzwa huko Mufindi inaonyesha Uzawa unatawala
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  kwa nini kila mgogoro, ndani ya chama-ccm, au serikalini lazima unakuta ni uhasama baada ya kura za maoni? hiki ccm kina uongozi kweli?
   
 5. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnamo tarehe 28/5/2012 , Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mhe. Diwani Mohamed Nwala( 0759 275310, 0784 688270) aliongoza kikao cha Baraza la Madiwani ambacho pamoja na Mambo mengine kilikuwa kinalenga kupindua Serikali ya Wilaya kwa kwenda kinyume na Kanuni za Utumishi wa Umma na Utawala Bora kwa kuzingatia utaratibu wa Utoaji haki. Hata hivyo Uchunguzi wa kina umeonyesha kuwa Kikao hicho kiliratibiwa na Wanasiasa waliopo madarakani na wale walioenguliwa wakati wa kura za maoni katika nafasi za Ubunge kupitia CCM mwaka 2010. Hapa ndipo tulipobaini na kuthibitisha kuwa Afisa Kilimo wa Wilaya Dkt Kasanga (0784 603371) ambaye aligombania Ubunge na Kuenguliwa baada ya Mhe. Job Ndugai Kushinda jimboni Dodoma na kuukwa ubunge huo 2010. Mhe. Aliko Kibona(Mbunge wa Jimbo la ILEJE) anayetoka ukoo wa Machifu Bundari na Mwenyekiti wa Wilaya waliongoza mapinduzi hayo ya kumuondoa Mkurungenzi wa Wilaya ambaye ni Mteule wa Rais huku wakimwandaa Dkt Kasanga ambaye ni mtu wao Kukaimu nafasi hiyo huku wakijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume na waraka wa TEMISEMI wenye kichwa cha habari “MABARAZA YA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI KUAZIMIA KUWAKATAA WATUMISHI NA KUTOA ADHABU KWA WAKURUNGENZI “uliosambazwa ,tarehe 4/03/2011 nchi nzima na kupokelewa na mabaraza ya Madiwani wakiwemo wa Wilaya ya Ileje. Pamoja na suala la Kisiasa kutawala katika mfumo wa Kumupindua Mkurungenzi lakini imebainika kuwa , Hisia za Mfumo dume na uzawa zinatumika zaidi ambapo watendaji wa zamani katika Halmashauri hiyo hawataki kuongozwa na wageni (Watendaji kutoka Wilaya Nyingine) hasa wanapokuwa Wanawake. Mfumo dume ndio unatumika kuwakataa ama kuwaletea misukosuko Watendaji wanawake ambao ni wageni kutoka Wilaya Nyingine Jambo ambalo linaleta Ukabila na Ukanda. Aidha uchunguzi wetu umebaini kuwepo kwa Mtumishi wa Halimashauri ya Jiji la Mbeya , mzaliwa wa Ileje ambaye amekuwa anatuma Majungu Dar –es salam kumushutumu Mkurungenzi wa Wilaya kwa malengo ya kumuondoa ili ageuke kujipigia debe nafasi hiyo.
   
 6. A

  ASKOFU MSAIDIZI JF-Expert Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 209
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tarehe 17/2/2012 taarifa iliyowasilishwa kwenye kamati ya Fedha ,Uongozi na Mipango ilibaini kuwa madeni ya kiasi cha Tshs 1,096,944,323.56 yaliyo wasilishwa lakini yalikataliwa kuwa ni makubwa mno na hawana imani nayo na Kamati hiyo iliamua kuteua Wajumbe Watano kuhakiki madeni hayo na kuchukua hatua. Tarehe 16/3/2012 Taarifa ya madeni yaliyo hakikiwa iliwasilishwa kwenye kamati ya fedha ikiwa na kiasi cha Tshs 1,121,690,714/= ikiwa ni zaidi ya Tshs 24,746,391 ya madeni yaliyowasilishwa na mkurungenzi hapo awali. Taarifa hiyo ndiyo iliyopelekwa kwenye baraza la madiwani tarehe 30/4/2012 ambayo ndiyo iliyotumika kumuhumu Mkurungenzi kuwa amewasilisha madeni hewa Hata hivyo kwa mujibu wa kanuni za fedha na utawala, baaada ya taarifa ya kamati ya fedha kuihakiki na kuiwasilisha kwenye baraza la madiwani inakuwa ni ya Halmashauri na sio ya Mkurungenzi kama wanavyodai Madiwani ambao wana malengo ya kisiasa. Aidha inaonyesha wazi kuwa madeni hewa hayo hakuyaleta Bi Syliwa Siriwa kutoka Sumbuwanga kwani nyaraka za madai hayo zilipatikana katika ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Ileje na yalikuwepo kabla haja hamia . Hapa ndipo madiwani walipaswa kumupongenza Mkurungenzi mpya kwa Kufichua madeni hewa badala ya kumutuhumu na kumudhalilisha. Tarehe 31/3/2012 Bi Sylivia Siriwa alizuia kwa njia ya simu Jaribio la wizi wa Tshs 86,210,000 baada ya kupata taarifa kutoka kwa meneja wa tawi la NMB –ILEJE akiomba idhini /uthibitisho wa kufanya malipo kutoka katika akaunti za Halmashauri. Jaribio hilo linahusisha kurasa ya mwisho ya kitabu cha hundi iliyonyofolea na kibutu chake yenye namba 000100 ya akaunti namba 6081200002 (Development A/C) ya tarehe 16/3/2012. Kwa muujibu wa nyaraka hizo fedha hizo zilikuwa zinalipwa kwa taasisi ijulikanayo kwa jina la “COMMANDANT SCHOOL OF INFANTRY) ya S.L.P 16105 ARUSHA kwa akaunti yake yenye namba 2071000009. Malipo haya yalikuwa yafanyike katika Tawi la NMB Temeke lililopo Dar –es-Salaam kama yasingezuiliwa na Mkurungenzi . Hata hivyo imebainika kuwa mtumishi aliyesaini hati ya malipo (PV) kama mwanzilishi wa malipo hayo ni Mr HENRY KAGOGORO (AG.DHRO) amaye ni mweka saini mmojawapo wa akaunti za Halmashauri lakini sio kwa akaunti ya Development ambayo ingetoa fedha hizo kwa kusaini tarehe 27/4/2012. Mtumishi aliyeidhinisha hati ya malipo (PV) kama mwidhinishaji ni Mr MCHUUZI LIMBANGA (DPLO) ambaye ni mweka saini katika akaunti hiyo ambayo fedha hizo zingetolewa kwa kusaini tarehe 28/02/2012 na ndiye aliyekuwa kaimu mkurungunzi wa Halmashauri kwa kipindi mkurungenzi mwenyewe (Bi Sylivia Siriwa) kuwa safarini Dodoma Kikazi kwenye mafunzo ya Maboresho ya Serikali za Mitaa ( POST-OSAKA TRAINING ALUMINI). Mtumishi aliyefanya ukaguzi wa awali (Pre-Audit) wa hati hiyo ya malipo ni Mr ANYITIKE CHISUNGA ambaye pia kwa sasa ni Cashier na anayetunza kitabu cha hundi kilichotumika kufanya malipo hayo kwa kusaini tarehe 28/02/2012 na pia kuhusika na ukurasa wa hundi namba 00030 ulio nyofolewa katika kitabu hicho cha hundi. Hundi hiyo imesainiwa na miongoni mwa waweka saini wa akaunti za Halmashauri na kwa makundi yao kwenye mabano ;Akaunti ya Development ni DPLO Mr Mchuuzi Limbanga( kundi B) na Kaimu mweka hazina wa Wilaya (Ag DT) Ms Subilaga Kapange (Kundi A). Malipo hayo yalikuwa yanafanyika kulipa gaharama za ujenzi wa Zahanati ya Luswisi na Ibaba ambazo hakuna shughuli kama hizo zinazoendelea kufanyika na taasisi iliyokuwa inalipwa fedha hizo eneo hilo. Baada ya kubaini na kuzuia wizi huu Wahusika wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi na suala hilo lilipelekwa kwenye Kamati ya Fedha , Uongozi na Mipango tarehe 16/4/2012 kama taarifa na kupelekwa kwenye Baraza tarehe 28/4/2012 kama chombo cha kushughurikia masuala ya Nidhamu kwa watumishi.Tarehe 30/04/2012 Baraza la Madiwani liligeuka kuwa kamati ya maadili na kumumutumu Mkurungenzi mtendaji Bi Sylivia kuwa ameshindwa kuwadhibiti watumishi waliofanya jaribio la kuiba fedha.Siku hiyo Madiwani 22 kati ya 25 wakiongozwa na Mbunge wa jimbo la Ileje Mhe Aliko Kibona ,walisaini waraka wa kutaka kikao cha baraza la dharura la lenye agenda ya kumutuhumu Mkurungenzi mtendaji wa Wilaya Ileje kama ifutavyo: 1).Kuiletea madeni hewa Halmashauri ya Wilaya ya Ileje kiasi cha Tshs 1,121,690,714.56 ,ambapo deni la Halmashauri halisi ni Tshs 251,732,782. 2). Kushindwa Kuthibiti Watumishi Waliofanya Jaribio la wizi wa Fedha Za Halmashauri Kiasi cha Tshs 86,210,000 na kushindwa Kuchukua hatua zinazo stahi juu yao. 3). Kushindwa kutoa Ushirikiano kwa mwenyekiti wa Halmashauri na madiwani wake Tarehe 28/05/2012 Madiwani waliazimiwa kumukataa Mkurungenzi wa Wilaya kama walivyopanga awali na kupendekeza aondolewe mara moja huku wakipendekeza nafasi hiyo akaimishwe Dkt Kasanga ambaye ni Afisa kilimo wa Wilaya ambaye kwa sasa ana makovu ya kuenguliwa kwenye kura za maoni jimboni kwa Mhe job Ndugai. Hata hivyo watafiti wetu wamebainisha kuwa , Bi Sylivia Siriwa ameingia mgogoro mkubwa na Dkt Kasanga baada ya kufuatilia fedha za miradi ya kuchimba mabwawa ambapo inatajwa kuwa kuna Ufisadi ulifanyika na fedha hizo Dkt Kasanga alizitumia Wakati wa harakati za kisisa Tarehe 29/05/2012 Mwenyekiti wa Halmashauri (Mhe diwani Mohammed Mwala) Kwa niaba ya Madiwani hao waliandika barua yenye kumb. Na Hwl/L.40/40/VoL.IV?31 kwenda kwa mkuu wa Mkoa Mhe Abbas Kandoro ikionyesha msimamo wao wa kumukataa Mkurungenzi wa Wilaya. Tarehe 03/06/2012 Mkuu wa Mkoa Mhe Abbas Kandoro alimujibu Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kwa kumurejesha katika vipengere vya haki kama ifuatavyo: (a)Mamlaka ya Nidhamu imeainishwa katika Sheria ya Utumishi wa Umma Na 8 ya mwaka 2002 kifungu Na 5(ii) na kanuni za Utumishi wa umma za Mwaka 2003 Kifungu cha 6(i) (b).Masula yote ya Kinidhamu yanapaswa kujadiliwa na kutolewa na mapendekezo kwenye kamati ya fedha , mipango na uongozi .Rejea Kifungu Na42(3) ivii cha majukumu ya kamati za kudumu za uendeshaji wa halmashauri .Hili halikufanyika. (c).Mtumishi wa umma anapaswa kuelezwa makosa yake na kupewa nafasi ya kujitetea. Utetezi huu ulipaswa kufika na kuwasilishwa kwenye kamati ya Fedha na Uongozi . Hili halikufanyika. (d). Masuala ya nidhamu hufanyika kwa siri na sio katika mkutano wa wazi.Rejea Kanuni za utumishi wa Umma za mwaka 2003 kifungu 47(7) na kanuni Namba 35 ya kanuni za kudumu za Halmashauri. Aidha Maelekezo ya jinsi ya kushughulikia masuala ya nidhamu kwa Wakurungenzi wa Halmashauri yamefafanuliwa zaidi katika barua kumbu Na. CAB.228/430/01/20 ya tarehe 04/03/2011 ihusuyo mabaraza ya madiwani katika halmashauri kuanzimia .kuwakataa watumishi na kutoa adhabu kwa Wakurungenzi kipengere cha 6(ii) “Halmashauri kuelewa kuwa haina mamlaka ya kuchukua hatua za kiidhamu dhidi ya Wakurungenzi wala kumkataa . Badala yake zinaweza kujadili utendaji na mwenendo wa Mkurungenzi na kushauri Mamlaka yake ya Nidhamu na ajira ambayo ni Mhe Waziri mwenye dhamana na Serikali za mitaa au katibu mkuu Kiongozi kupitia ofisi ya mkuu wa Mkoa kwa hatua zake. Aidha zinaweza kuomba Ushauri ofisi ya Mkuu wa mkoa wakati wowote unapohitajika ushauri wa Kitaalamu” Mkuu wa Mkoa alimshauri mwenyekiti wa Halmashauri kulifkisha suala hilo kwenye Kamati ya Fedha, Uongozi na Mipango ili kujadiliwa kwa kina kiataaluma na kupatiwa ufumbuzi. Hata hivyo Mhe Kandoro alitoa msimamo kwa mambo makuu mawili yafuatayo: Mosi Mkurungenzi ataendelea kuitumikia nafasi yake mpaka Ushauri mwingine kutoka mamlaka ya nidhamu na yenye kuridhia.Pili Mategemeo ya kuleta Externala Auditor ilikufanya Special Audit ili kupata picha halisi ya mwenendo wa fedha , matumizi na usimamizi wa miradi
   
 7. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,225
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Ileje si mahali pa kufanyia kazi, watu wa ileje ni hopeless na watumishi wote hawana ethics. Tazama wanavyomwaga docs za serikali hapa. Inaonesha wamejaa majungu. Pole zao. Ni vema serikali ikawachukulia hatua.
   
 8. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Bw Gama Doc za Ikulu na za Katibu Mkuu Nishati na madini zimevuja sembuse doc za Ileje?? Kuvujisha doc ni uzalendo sio kuvunja ethic hasa pale ambapo doc hizo zinahusu hujuma!!!

  Unakumbuka doc za list of Sham alizotoa SLAA???
  Kama wewe ni mmjawapo kaa pembeni JF ni kimbilio la Wanyonge!!!
   
 9. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #9
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Taarifa kutoka Ileje Zinaonyesha kuwa Mkurungenzi wa Sasa Bi Sylivia Siriwa amekataa ripoti ya makabidhiano ya fedha kutokana na kukosekana kwa maelezo ya deni la zaidi ya 1.2bils.

  Inaonyesha kuwa Mkurungenzi wa zamani Ileje Bi Gradys ni hawara yake na Mweyekiti wa Madiwani Ileje Mh Mohammed Mwala ambaye aliongoza kikao cha kumukataa Mkurungenzi mpya kwa kumutuhumu kuwa ameiletea Halmashauri deni hewa huku akijua kwamba deni hilo limesababishwa na utawala wa hawara yake.
  Hadi sasa Bi Gradys yupo anarekebisha ripoti hiyo ili kupata ushahi ya chanzo cha deni hilo.!!!!
   
 10. duocore

  duocore Member

  #10
  Jan 12, 2013
  Joined: Aug 27, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Inawezekana kweli kuwa alikuwa hawara yake, na madiwani wenzake wanamtazama tu. Mapenzi na kazi wapi na wapi? Madiwani kuweni macho mtakosa wataalamu, labda mpate wazawa "MBOMBO JILIPO"
   
Loading...