Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 56
Mwafrika wa Kike,Ninataka niamini kuwa ni kweli kuwa CHADEMA kuna mgongano kuhusu uteuzi wa zitto kwenye kamati/tume/jinalolote ya JK ya madini. Kama hizi habari ni kweli, basi hii ni dalili nzuri sasa kuwa watanzania wamegundua kuwa kabla ya kukubali au kupitisha jambo lolote kubwa na lenye kugusa maslahi ya watu wengi nchini ni lazima kuwepo na mjadala na mchanganuo wa kutosha.
Ninashawishika pia kusema kuwa kama chama tawala, bunge, halmashauri zetu zingefanya maamuzi kwa msingi wa kuruhusu mawazo ya wengi yasikilizwe ikiwemo wale wanaopinga kabla ya kupitisha vitu haraka haraka Tanzania ingekuwa bila IPTL, Kiwira na maovu mengi yaliyopitishwa na watu wachache sana kwa manufaa yao binafsi.
Hii ni nafasi kwenu viongozi wa CHADEMA kuonyesha nchi hii kuwa mko tayari kutunza demokrasia na kuruhusu utofauti wa nia na mawazo ndani na nje kwa nia ya kujenga kitu kikubwa na chenye manufaa kwa watanzania wa leo na wajukuu zao.
Fanyeni mjadala wazi na kila kitu kiweke pamoja ili mwishoni ikiamuliwa nini kifanyike kunusuru taifa na mafisadi wanaouza nchi, kila mtanzania azidi kujenga imani kwenu na kwa watanzania wote ndani na nje ya serikali waliochoshwa na uozo unaondelea.
Zitto ameshafanya uamuzi wa kuingia katika kamati/? hii na mie naona kuwa ni vyema aingie huko kama hivyo ndivyo anashawishika kufanya. Zitto ameahidi kuwa ataendeleza kulinda maslahi ta Tz kwa hiyo ni vyema apewe nafasi kufanya na kuthibitisha hilo. OK Zitto, kafanye mambo huko ila ukisalimu amri afadhali uombe kazi huko ikulu or something. Kwa sasa GOOD LUCK - NENDA KAFANYE KAZI
Mwafrika wa Kike,
Flip flopping, when did you change your mind on this? I thought you were against the idea of Zitto joining the committee.
mwafika wa kike,sasa kama Zitto akiteuliwa kuwa Waziri mtakakataa wanachama wa Chadema? Mie naona mnacheza cheusi chekundu i mean karata 3 Zitto kuwa pale ni kwa maslahi ya taifa au Chadema?? na Chadema ni kwa ajili yenu akina Mtei na Mbowe au ya Taifa?
Hebu acheni siasa za ajabu muacheni afanye kazi kama kweli alikuwa against na mikataba mibovu ya madini atasema nakama akikubaliana na hali ile nae atakuwa wale wale tu
Mkuu Heshima mbele, the ishu ni Chadema na Zitto na kamati ya rais, sasa CCm inatokea na kuingilia wapi? Siasa sio lazima iwe kila ishu, kuna sometimes inabidi ifike mwisho na this is one of those ishus.
Maana kama ni kukomaaa kwa chama wananchi ndio wanaojua zaidi na walishaamua kwenye kura zao, hata kura za uongozi mdogo tu wa madiwani, wao wanajua ni nani aliyekomaa kidemokrasia, lets talk Zitto na kamati, the real ishu hapa!
Mkishachanganya, na sisi wananchi mnatuchanganya! Mkuu Kitila you are too big for this!