Mgomo watatiza shughuli SA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo watatiza shughuli SA

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by OSOKONI, Aug 18, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Aug 18, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  Mgomo wa wafanyikazi wa umma nchini Afrika Kusini umeingia siku yake ya pili, huku wafanyikazi zaidi wakitarajiwa kujiunga na mgomo huo, ambao umekatiza hudumu za umma kote nchini humo.

  Imetangazwa kwamba wanachama laki moja wa muungano wa wafanya kazi wa umma ambao hawakugoma jana watajumuika na wenzao hii leo kudai nyongeza ya mishahara.

  Vyama vya wafanya kazi nchini humo vimetishia kufunga mojawapo wa barabara kuu na yenye shughuli nyingi sana katika mji mkuu wa Johannesburg kuishinikiza serikali kuwaongezea mishahara.

  Zaidi ya wafanyikazi millioni moja wakijumuisha madaktari, wauguzi, maafisa wa polisi na walimu wamegoma wakitaka nyongeza ya mishahara ya asilimia nane nukta sita badala ya asilimia saba iliyopendekezwa na serikali
  bbc
  hii ndio migomo sio utani tunaofanya sisi wafanyakazi wa TZ!!
   
 2. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #2
  Aug 18, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aiseee baba yangu kama ni elimu hao watumishi wana masters huku tanzania ndio kwanza tunafanya mtiani wa taifa darasa la 4 kuingia la 5,,hao jamaa wanajuwa kupigania haki zao za msingi
  nawaunga mkono
   
Loading...