amba.nkya
JF-Expert Member
- Jan 7, 2010
- 446
- 131
Kuna mgomo baridi umeanza kwa wauza mafuta ya petroli, dizeli na taa kwenye vituo kadhaa jijini Dar es Salaam.
Mgomo huo umeanza kufuatia EWURA kutangaza jana bei mpya elekezi (cap price) ambapo jijini Dar kwa mfano bei ya petroli inatakiwa kuuzwa sh 1955 kwa lita.
Miongoni mwa vituo ambavyo vimeanza huo mgomo ni PUMA Mwanamboka, Kinondoni, PUMA Sea view road karibu na Bank M, n.k.
Maswali ya kujiuliza:
Kwanini makampuni hayo inapotokea bei ya mafuta kupanda kwenye soko la dunia nao hupandisha bei muda huo huo lakini inapotokea bei imeshuka hawataki kushusha bei?
Je, serikali haina mamlaka ya kudhibiti hali hii?