Mgomo wa wahadhiri UDOM wanukia

vipi udsm?

 
UDOM kuna hata kundi la Muslim Brother hood mwislam akitaka hata million moja kama kipindi hiki ambapo hakuna mshahara anapiga sm kwa mhasibu( mwislam mwenzake) anaomba kisha anaambiwa pitia saa 4 asb. Wewe wasema nini? Kama huna data tulia sikiliza. Wakati wahadhiri wanazuiliwa kwenda kusoma nje ya chuo mawadern waislam wamepelekwa Kusoma nje kwa gharama za chuo. Ila mhadhiri anatakiwa asomee hapahapa UDOM na tena akatwe 10 % ya mshahara wake kla mwezi. PIMBI WEWE HUNA DATA KAA KIMYA. NYANG'AU MKUBWA.
 
Duh!Tanzania tumefikia pabaya sana kama tumefikia hatua ya kuangalia ratio ya wafanyakazi kwa kuangalia dini zao! Bahati nzuri hili ni la JF tu lakini nje tunaishi kama ndugu japo kwa kinafiki lakini inasaidia tuishi kwa amani! Haya sasa mkimaliza UDOM tuanze ofisi kwa ofisi tuangalie ratio zao kwa imani zao za kidini,tena tuangalie top management tu halafu tuone sasa tutaipeleka wapi nchi yetu! Watu tunajidai wadini kweli wakati hata dini zenyewe hatuzijui. wengi humu ni wakristo-jina na waislamu-jina tu lakini mapovu sasa duh!
 

Mkuu umechambua vizuri. ni kweli ni wakristo- jina na waislamu -jina tu. MUNGU hapendi chuki, hasira, visasi na kutanguliza tamaa ya mambo ya dunia (kimwili) mbele na ya kiroho kama upendo njuma.

Naomba kuuliza, hawa waliopanga kugoma UDOM kutokana na mada hii humu, ni kama uamsho wa zanzibar au boko haram wa Nigeria? na utofauti wao ni hawa wanaegemea upande wa kujiita wakristo au sio?.

Kama ni kweli wana elements za boko haram basi ni hatari. Tena wapo kwenye taasisi kubwa ya elimu ya juu, tusipoangalia hata watoto wetu na wa kizazi kijacho kinaweza kuathirika.

Naomba tuingie kwenye maombi na kufunga ili MUNGU aingilie kati hili jambo. Nawatahadharisha shetani yupo kazini kutufarakanisha na kuchochea chuki hii. Chuki ni ugonjwa mkubwa sana ambao shetani hutumia.
 

Haya tenaaa! Kuna tatizo la msingi ktk uteuzi wa viongozi. Juma Mwapachu si mtu anayestahili kuonyesha mafanikio. Huyu ni mtu aliyefika hapo kwa sababu za kihistoria tu. Brain iko nusu na mbaya zaidi anahangaika sana kila wakati kuonyesha kwamba ni mwenye mafanikio.

Hapo kwenye RED mimi nashauri kesi hiyo ya matusi ipelekwe mahakamani. Yeye kuwa mwenyekiti wa Baraza isiwe sababu ya kutukana watu.

Kutukana ni kosa linalostahili kufikishwa mahakamani. Apelekwe hata kama mashahidi watagoma kusema walilosikia lakini itampa ufahamu kwamba hayuko juu ya sheria.
 

Naomba nitumie Prospectus ya UDOM ya 2011-12 kuna safu kama ifuatavyo:
  1. Chancellor - Mkristo
  2. Chairman of Council - Msilamu
  3. VC - Msilamu
  4. DVC ARC - Mkiristo
  5. DVC PFA - Msilamu
  6. College Principals
    1. Education- Mkristo
    2. Humanities and Social Sciences - Mkristo
    3. Informatics and Virtual Education - Mkristo
    4. Natural Sciences and Mathematics - Mkristo
    5. Health Sciences - Mkristo (msabato)
    6. Earth Sciences - Mkristo
  7. Deans wapo kwenye schools 13 kati ya hao ni wawili tu ni waislamu nao ni Dr. S. Vuai ambaye ni Mzanzibar wa pili kati ya wawili tu walio kwenye madaraka UDOM (kwa ufafanuzi Mzanzibari mwingine ni DR. Ame ambaye ni Mkurugenzi wa Graduate Studies)
  8. Dean of Students wote ni wakristo
  9. Directors wapo 6 wakristo ni 4 na waisilamu ni 2
  10. Secretary to Council ni Mkristo
  11. Chief Internal Auditor ni Mkristo
  12. Estate Manager ni Mkristo
Nimechunguza pia ofisi ya Bursar wakristo ni wengi tu.

Kwa kuhitimisha nashauri TUSIANGALIE IDADI YA UKRISTO NA USLAMU BALI TUPENDANE NA TUUNGANE KUJENGA NCHI YETU KWA KUTOA ELIMU BORA NA SIO MALUMBANO YASIYO NA MSINGI.

Kwa kufuata list hapo juu inaonyesha mada hii haina ukweli ya kuwa kuna udini.
 

Kwanza kumuita Mugabe sio tusi. Na pili kuamriwa kuitisha uchaguzi kama katiba yao ndio inavyoonyesha, hakuna ubaya hapo. Ni vema kufuata taratibu zilizowekwa tena na wadau. Mfano kama muda wa uongozi wa UDOMASA ukipita sasa ataruhusiwa vipi kuingia kwenye baraza la chuo?. Akiwa kama nani na muda wake ulishapita?. Balozi yupo sahihi, hana kosa na hakutukana.
 
kwa kweli udini upo UDOM, alafu walioajiriwa kwa mgongo wa dini au u-mjomba wana lugha chafu haoooo....kuna dada mmoja anaitwa Cheusi ni secretary wa dean wa social science, duh huyu dada usiombe ni mvivu alafu lugha atumiayo kwa anaowahudumia sio nzuri hata kidogo.
 
Kuwa na Chancellor, VC, DVC ARC, Director HR, Bursar, Internal Auditor, Director Undergraduate Studies, Director Finance na kadha wa kadha Wakristo in maanisha UDSM ina udini?


"Kunya anye kuku akinya bata kaharisha"
wengine wapagani bwana hawana dini
 

chancelor siyo mtendaji, na dvc academic hausiki hata kidogo na ajira kazi yake kubwa ni taaluma ambayo ni engine ya taasisi yoyote ya elimu ya juu ! ajira ambalo ndio bomu kubwa udom anahusika dvc wa utawala na fedha naomba pitia tena vizuri kwenye RED haupo sawa hata kidogo!
 
Ni mimi Niambieni. Samahani naomba msinitafisiri vibaya. Mimi sipendi udini bali napenda yote yampendezayo MUNGU. Naomba soma kwa makini na tafakari, ila nakuomba usikasirike wala usidhani nina chuki bali nina upendo


SOMO MUHIMU KWA WOTE PAMOJA NA
WAISLAM NA WAKRISTO WOTE
​

ACHA MAUAJI, ACHA CHUKI, ACHA MAOVU, ACHA DHAMBI. OKOKA! YESU NI MWOKOZI -" Naye atazaa mwana,nawe utamwita jina lake Yesu,maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao" (MT 1: 21).

UKIBISHA FAHAMU YA KUWA "… mshahara wa dhambi ni mauti. Bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" (Warumi 6: 23).
OKOKA "Kwasababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako yakuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka" (Warumi 10:9). Wapo wakristo wengi tu wanasema eti hakuna wokovu wakati Biblia zao zina warumi 10:9.


HAKUNA NJIA INGINE YA WOKOVU BALI NI KUPITIA KWA YESU TU!
TUSIPENDE UDINI TUPENDE YOTE YAMPENDEZAYO MUNGU
​
 

Bado sijaona udini wowote hapo! lugha chafu na uvivu si uisilamu hata kidogo! Tutatue matatizo yaliyopo, tuepukane na udini!
 


Kuna maswali mengi kuliko majibu kwenye tuhuma zenu.

Mosi; Kama katika madai yenu ya umoja wa wanataaluma unamadai, je, umoja huo ni wa wakristo pekee?

Pili; Iwapo hamfungamani na upande wowote, je, si matumizi mabaya ya madaraka yenye ubaguzi wa kidini kama hao mnaowatuhumu?

Tatu; Umesema maamuzi ya baraza la chuo ni kuondoa baadhi ya "priviledge" kama usafiri na matibabu, je uamuzi huo hauwaathiri waislamu?

Nne; Je, nini uwiano wa wakristo na waislamu?

Tano; Je, wakuu wa 'schools' wana nguvu gani katika mfumo wa maamuzi wa chuo?

Sita; Je, madai yenu ni dhulma dhidi ya dini ya moja au haki zenu?
 

anayeajiri ni DCV Academic au DVC Administration ? siku zote inajulikana kuwa Utawala (Administration) ndio wanaoajiri.
 
Tupeni Updates za mgomo sasa. Mbona kimya? Mgomo umeshaanza au bado? n00b tafadhari mkuu!
 
Ninachoona hapa ni kuwa kuna waliotumwa kuvuruga madai halisi ya wahadhiri kwa kuongeza hoja ya udini isiyokuwa na msingi wala ukweli. Na wenye madai yenu msiposimama kuipinga hii, hamtafanikiwa kamwe. Hoja ya udini itawagawanya mtashindwa kupigania haki yenu.
 

You are not serious! Unamaanisha hata nafasi ya ukatibu mkuu wa EAC Juma Mwapachu alipewa 'kihistoria' na kwa 'akili nusu'? Naomba tu uache haya matusi! Au nawe ni mmojawapo katika waliotumwa kuwavuruga wahadhiri kwenye umoja wao?
 
Chimwanga simu hazikamati nini? Tupeni updates tafadhari hata kama ni kwa mchina.
 
Chimwanga simu hazikamati nini? Tupeni updates tafadhari hata kama ni kwa mchina.

Tumshukuru MUNGU naona wahadhiri UDOM "wamegoma kugoma" na hali ni nzuri na tazama MUNGU amesikia maombi yetu.

TUMWOMBE MUNGU adumishe upendo, amani na furaha kwenye jamii yetu na hata zituzungukazo na duniani kote.

Ukweli ni furaha kuu kama wooooteeee siku moja tukikutana mbinguni na kufurahia na wote walio huko. Ningependa hata shetani atubu na abadilike na kuwa pendezo kwa MUNGU MUUMBA WETU.

UPENDO NI TUNDA TAMU SANA. JARIBU KUMPENDA JIRANI YAKO, UONE TABASAMU NA HISIA ZAKE, NI KUWA UPENDO UZAA UPENDO. WAHADHIRI UDOM, MUNGU ANAWAPENDA SANA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…