'''Mwisho ni malizie kwa kuwataka wanaharakati na wale vyama vya siasa akiwemo Kada ya Chadema, Godbles Lema ambao wametoa matamko ya kulaani kitendo alichofanyiwa Ulimboka na Lema akasema akifa Ulimboka atalala barabarani, nawataka wageuze upande wa pili wa shilingi na waone kuwa kuna mamia ya wagonjwa wanakosa huduma na kupoteza maisha yao kwaajili ya mgomo huo haramu,mbona makundi hayo hatusikii yakitoa tamko ya kuwasema wananchi hao na kulaani mgomo huo haramu wa kisheria ambao mahakama ilisema mgomo huo ni batili?.
Wewe Lema unayesema utalala barabarani Ulimboka akifa, tumuulize huyu Lema ni kwanini alishindwa kulala barabarani siku ile Jaji Gabriel Rwakibalila wa Mahakama Kuu Kanda ua Arusha alipotoa hukumu dhidi yake ambapo alimvua ubunge na kumfungia kugombea ubunge baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kutoa lugha chafu?
Maana hukumu hiyo ndiyo imemfanya Lema hivi sasa awe kaka sisi tusiowabunge kwani analifuatilia bunge kupitia redio na televisheni, hapati tena posho na mshahara na hapewi heshima na stahili za kibunge tena,sasa tumuulize sasa alishindwa kulala barabarani kwa hukumu hiyo iliyokuwa ikumuhusu na imemwathiri yeye binafsi ndiyo leo hii atakuwa na ujasiri wa kufanya hivyo kwa Ulimboka ambaye hawana hata undugu?'''-Happiness Katabanzi.
Huyu dada ndio kanisikitisha kabisa.Hapa Lema kaingiaje?Hata kama mwandishi ameamua kumuhusisha kamnda wetu katika uchambuzi wake uliojaa jazba na kebehi dhidi ya madaktari ,bado haewezi kuwa na mamlaka na uwezo wa kuwachagulia wananchi wenzake,nikiwemo mimi ama Lema ama Molemo masuala ya kusimamamia na kujadili.Ajue hivyo na aache mara moja.Inafaa afahamu kuwa Lema si mbinafsi ,anapigania maslahi mapana ya jamii na amekwisha tamka muda mrefu kuwa kutokuwa mbunge hakumzuii kuwapigania wananchi wenzake.....Eti analeta hoja dhaifu kuwa Lema hana undugu na Ulimboka!!!Nimuulize dada mwandishi swali:hivi madaktari waliopambana hadi Ulimboka anapelekwa South Africa wote ni ndugu zake Ulimboka ?Naomba nitajiwe mwanaharakati anayeyatazama masuala kwa misingi ya undugu,ukabila na bado akabaki kuwa mwanaharakati?Eti anadai Lema sasa hana tena 'heshima ya kibunge' na 'mishahara ya ubunge'!!Hoja dhaifu!!
Yeye,dada mwandishi, anayejifanya anayewatetea wananchi ina maana wananchi wote wa Tanzania ni ndugu zake?
Huyu dada anaandika kihisia zaidi...anatumia lugha ya kuudhi na isiyo ya kindugu kabisa dhidi ya ndugu na rafiki zetu madaktari.Ameuanika udhaifu wa fikra zake.Sidhani kama kuna haja ya kusoma maandiko yake tena.
Kuhusu RAIA MWEMA:Mimi si mwanahabari ingawa,ili kuweza kuzifuatilia vema siasa za Tanzania nalazimika kuwategemea wanahabari ..Habari husika ilinishtua sana hasa baada ya kuona mwandishi ameihusisha CHADEMA.Baada ya kutafakari niliamua kuichukulia kama mawazo na maoni ya mwandishi na si maoni ama msimamo wa gazeti zima. WAKATI WA KAMPENI ZA ARUMERU WALIDAI KUWA NASSARI ANASAFIRIA NYOTA YA DKT.SLAA NA MBOWE NA KUWA VIJANA WENGI HAWAKUWA WAMEJIANDIKISHA KUPIGA KURA NA KUWA WALITAKA TUAMINI KUWA CDM ingeshindwa.Yaliyotokea sote tunajua.
Ujumbe wangu kwa Raia Mwema ni kuwa mjitathmini mjihadhari na uwezekano ama tishio la kuwa co-opted na serikali ama CCM.Pamoja na kosa hili la kiufundi walilotenda ,bado ninawamini kama chanzo cha uchambuzi maridhawa.