Mgomo wa madaktari ni batili: Askofu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari ni batili: Askofu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Jan 29, 2012.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Leo asubuhi nilipita karibu na kanisa lilipo karibu kabisa na bandari ya Dar.
  Askofu ambae akiongoza misa hiyo aliwashtumu sana madaktari wale wanagoma, alisema si vyema kugoma huku wananchi wakitabika. alidai Taaluma ya Utabibu ni huruma zaidi badala ya kipato na anasa. aliwalaumu zaidi hasa wale wa Hospitali za dini.
  alisema ni vigumu kuamini hawa madaktari waliozaliwa katika ukiristo,kukulia na kulelewa katika ukiristo leo wanaingia kwenye mtego huu wa hospitali za umma na alidai sijui wana ajenda gani na binaadamu wenziwao.
  alidai serekali inatoa fedha nyingi kwa taasisi hizi kupitia MOU lkn leo hii wanagoma kushindika kulipwa mishahara mikubwa.

  aliomba Serekali kuwachulia hatua kali madaktari wote waliokuwa chanzo cha mgomo
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Habari yako MS? mZIMA?...Siku hizi unajiita tena Dogodogo?
  Kanisa lililopo jirani na bandari ndiyo nini hiyo?
  Ulijuaje aliyekuwa anahubiri ana cheo cha Askofu...au unafurahisha jamvi?
  Acha umbea mkubwa mwenzangu~!
   
 3. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kanisa halina jina, hata askofu pia?
  Na umejuaje kuwa anayezungumza ni Askofu ilhali hukuingia ndani?
   
 4. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  malaria sugu at work!!
   
 5. Mr Suggestion

  Mr Suggestion JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 605
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 60
  Mameno matupu hayata saidia kitu, wapeni pesa wanayohitaji kwani maisha magumu kwa wote si wabunge peke yao

  Vipi maaskof wa kenya walisemaje kipindi cha mgomo huko kenya? Hii ndio dawa ya watawala wasiotumia akili kufikiru
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Haahaaa! Askofu asiye na jina wala kanisa must be a fictious askofu.
   
 7. vimon

  vimon Senior Member

  #7
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 3, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  malaria sugu aje tumpe quinine at pona
   
 8. F

  FJM JF-Expert Member

  #8
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Madaktari hawajaomba ushauri wa maaskofu. Sana sana huyu Askofu alitakiwa looong time ago waisharuri serikali waboreshe huduma za afya pamoja na maslahi ya madaktari. Hawajafanya hivyo sasa wanataka kumuuingiza Yesu kwenye huu uzembe wa serikali. Huduma za afya zimeanza kuzorota leo? Kinachofanya wakubwa wapelekwe India ni nini?

  Kwa nini hawa maaskofu wanachanganya watu? Wanasimamia nini? Harambee?
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Matusi ya nini na wewe ndugu yangu? kwani ulitaka aseme askofu ameunga mkono mgomo kama John Mnyika na wenzanke walivyosema huku wakijua kabisa wanatenda dhambi ya kutowapenda wanzao wanaoteseka mahospitalini. Najua wewe siyo daktari kwani usingeweza kuporomosha matusi hivyo. Bila shaka wewe ni teja fulani naamini kama ni mtu na akili zake timamu na siyo mwanasiasa huwezi kuuunga mkono mgomo ambao matokeo yake ni vifo. Teja, Mwanasiasa, kichaa anaweza na kwa vile umeanza na matusi naamini kundi la teja , mwanasisa haumo. Labda chizi.
  Mwenzako kasema alichokisikia wewe unabwatuka, kama unajua ugonjwa ni nini na wewe ni binadamu na kwamba una familia au ndugu anayeweza kuhitaji huduma ya matibabu huwezi hata sekunde moja kuunga mkono mgomo, labda kama unataka umaarufu kama ambavyo umetumwa na wanasiasa ubwatuke bila kutafakari mateso wanayopata wenzako. Nini maslahi bora bwana, huwezi kuchezea maisha ya watu kisa maslahi bora. Naiasa Serikali kuwa kali kwa hili na hata mgomo utakapomalizika iwe serious na utendaji wao kwani wanaumiza wananchi sana kwa kuwaomba rushwa, kutoka kazini kabla ya muda, kuchukua madawa na kuyapeleka katika dispensari zao na usumbufu mwingi usiyo wa lazima.
   
 10. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #10
  Jan 29, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Pengo (and his subordinate bishops) can never (and would never) kneel nor bow to make any request from the government. MARK MY WORDS!
   
 11. only83

  only83 JF-Expert Member

  #11
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Japo wakristo tunaambiwa usimnenee mabaya mpaka mafuta ya Bwana...huyu askofu anapaswa aende akapate nasaha za kuimarisha ubongo wake...Hivi kama udaktari ni huruma kwa hiyo hao madaktari wakapate wapi pesa za kulisha familia zao,wapi pesa za kulipia ada za watoto wao..kama yeye anasema hii kazi ni huruma,mbona wao wanakula zaka zetu na sadaka zetu sisi hatusemi uaskofu ni kazi ya huruma? Naanza kukosa imani na viongozi wengi wa dini,kweny vitabu vyote vya dini hakuna sehemu ambayo Mungu anakubaliana na watu kuteswa na kunyimwa haki zao za msingi..na Mungu anaita upole uliopitiliza kama upumbavu...ebu tuachwe tudai haki zetu za msingi ili mradi hatuvunji sheria wala taratibu zozote za nchi.
   
 12. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #12
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  dogodogo mpaka akili ya ki dogodogo,umejuaje kuwa alikuwa anahubiri ni askofu wala si padre,si mchungaji,si shemasi,si mgeni rasmi,kama ulipita karbu na bandari labda alikuwa kuli au ulikuwa unatoka baa?huwezi kumchonganisha askofu na daktari,afterall kuna maaskofu ambao pia ni madaktari. Tafta njia nyingne,hii ni failed mission.
   
 13. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ubovu wa huduma za afya nchini haujaletwa na madaktari wala manesi bali ni utendaji mbovu na ufisadi wa serikali yetu. Daktari na nesi ni taaluma inayofundisha sana maadili ya kazi na wanayafuata kwa kiwango kikubwa lakini inapofika wakati Nesi anaondoka nyumbani gongoramboto nakwenda kukesha muhimbili na huku amewaacha watoto na familia yake hawana hata hela ya kitafunwa kesho yake utegemee atakuwa na mudi gani ya kazi kama siyo kufukuzia virushwa vidogovidogo japo apate elfu mbili za maandazi kesho yake?

  HakuNa binadamu aliyeshiba ambaye angependa kujidharirisha kwa kupokea rushwa ya sh. 2000 au kuiba gloves akauze! Haya yote ni mfumo mbaya wa kuwaangalia zaidi wapiga domo kuliko watendaji tunapopanga hata mishahara. mbunge wa darasa la nne ambaye kazi yake nikulala tu bungeni anapata mshahara mkubwa na miposho rundo ilihali daktari au Engineer mwenye phd wanapiga miayo na mshara wa mwaka 47. Kuna ma prof muhimbili wanatibu na kufundisha lakini nenda kaangalie maisha wanayoishi unaweza kulia wamepewa vijumba vya mabachara ili hali wanafamilia kubwa. Ukiingia nyumbani kwao unasema ni bora ukafanye biashara kuliko kuwa prof nchi hii.

  Hayo yote tisa kumi ni kwamba serikali inao uwezo wa kuboresha mazingira ya hawa ndugu ispokuwa wanaona kutoa zaidi matumbo yao yatapungiwa!

  Nadni kuna haja ya kugeuza kibao ili wataalamu wanaosota katika kupata utaalamu huo wafaidi matunda ya juhudi zao na wale walizembea wakitarajia kuja kupiga porojo na kuibuka na mishahara na marupurupu basi nao wafaidi uchungu wa matunda yao.

  Kunahaja ya kujenga taifa linaloheshimu taaluma na siyo sisa kama ilivyo leo. Mtu aingie kwenye siasa akiwa ametosheka na matunda ya taaluma yake ili aingie huko kwa ajili ya utumishi na kuridhisha nafsi yake tu lakini si kuchuma kama ilivyo leo. Na hili litafanikiwa kwa kuunga mkono harakati kama hizi. Wananchi tunahitaji kuungamkono madai ya malipo ya haki kama ya madaktari na walimu na kupinga malipo ya wizi kama ya wabunge.
   
 14. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,163
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  kwanini mnashindwa kuibana selikali ili itimize wajibu wake? Wakati wewe unawalaum ma dr. Kuwa wanauza madawa na vitendea kazi vingine, wao wanaibana selikali kuleta vitendea kazi vya kutosha!
   
 15. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  only83 ,uyu dogo dogodogo mbea tu,wala asikugombanishe na charismatic leaders.
   
 16. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  "Shetani ni muuaji na baba wa uongo"
   
 17. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ni jina lake tu ndio limepigwa ban, mawazo yake bado ni yale yale
   
 18. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Acha kukurupuka na hoja nziiito ukapanda presha bure, una ugeni na Malaria Sugu? Kapigwa ban juzi hapa sasa msioweza kumtambua kwa maneno yake mtachangia mada hasaaaa. Ukitafakari utabaini kuwa mtu ukipita nje ya kanisa huwezi kujua kama anayehubiri ndani ni ASKOFU, PAROKO au PADRE. Usiwe mwepesi hivyo kukamatwa na huyu ****
   
 19. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #19
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Habari yenyewe imekaa ki MS MS. Mods pelekeni huu uchafu Chit chat!
   
 20. kanyasu

  kanyasu JF-Expert Member

  #20
  Jan 29, 2012
  Joined: Feb 9, 2009
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kauli hii inatia matumaini maana huko nyuma tumezoea kuona kila jambo baya siku hizi viongozi wa makanisa wanakaaa kimya.mimi nataka kuwaambia watanzania hasa wana JF taaluma zote tanzania zinatakiwa zipewe kipaumbel siyo madaktari tu,anayekwambia daktari ni mtu muhimu kuliko mwalimu anakudanganya,maana bila mwalimu hakuna daktarai,dereva je? uliwahi kusikia mgomo wa madereva huko ujermani? nchi nzima ilisinyaa, je wakigoma benk? je wakigoma polisi? je maduka yote yakifungwa wanyabiashara nao wakagoma mwezi?
   
Loading...