Mgomo wa Madaktari na wanaharakati wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa Madaktari na wanaharakati wetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Paul S.S, Mar 13, 2012.

 1. P

  Paul S.S Verified User

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Jana wakati Rais JK anaongea na wazee wa DSM aliligusia hili la wanaharakati wetu jinsi walivyoshiriki katika mgomo huu, ingawaje kwa walio wengi ambao walisapoti Drs hili wataliona ni moja ya porojo alizokuwa anazipiga Mzee wa Kaya.
  Wakati ule wanaharakati walipo ingilia kati kwa kusapoti DRs kwa asilimia mia moja wenye akili timamu tulihoji,
  tulihoji kuwa kweli wanaharakati hawaoni na upande wa pili kuwa wananchi wanaowasimamia katika harakati zao wanaumia kwa vita ya GVT vs DRs, kwa bahati mbaya hatukueleweka

  Nadhani hii ni changamoto kubwa kwa wanaharakati wetu kuangalia upya kile wanacho kitetea kwa maslahi ya mwanachi wa chini kabisa
  Kwenye mgomo huu Ingawaje DRs walikuwa na madai yao ya msingi ambayo GVT ilionyesha nia ya kuyatekeleza wanaharakati hawa walikuwa kimya hadi pale DRs walipotaka viongozi wa kisiasa wawajibishwe kwanza ndio maswala mengine yafuatie ama sivyo mgomo moja kwa moja
  Hapa sasa waliibuka from no where na kuanza kushinikiza mawaziri wawajibishwe na kuunga mkono mgomo uendelee hadi watolewe mawaziri.

  Binafsi nilijiuliza sana kwamba ni kweli DRs wanasuguana na GVT kuhusu madai yao na hapa wanao umia ni wananchi, je wanaharakati ni lazima walalie upande mmoja wa DRs na kuacha wananchi wakitaabika, hivi walifanya juhudi gani kuhakikisha wanatetea maslahi ya mwanachi wa kawaida anayeuza vitumbua na maji akakuta Drs wamegoma na mfukoni ana pesa ya kumudu gharama za hospitali za serikali tu.

  Kweli walimfikiria mwananchi huyu au walifikiria JK ni mgumu kuwajibisha wateule wake na sasa watumie mwanya huo kushinikiza bila kujali athari kwa wananchi wano watetea?

  Je wanaharakati wetu ni ma opportunist wanao subiri tukio ndio waonekana kwenye media "kutetea" wananchi?
  To be frank sijawahi kusikia wanaharakati wetu hawa wameibua hoja na kuivalia njuga zaidi ya kusubiri matukio pamoja na kuwa wanafanya kazi nzuri kiasi

  Je kuwa mwanaharakati ni nini? nikuwa againt GVT muda wote hata kama kufanya hivyo ni kuumiza wananchi wasio na hatia kwa mambo yasiyo na ulazima

  Mtazamo wangu nadhani ni vizuri wanaharakati hawa wakaangalia maslahi ya wananchi kwa ujumla hasa linapokuja swala la uhai wa watu, nilitarajia wanaharakati wangekuja na msimamo wa kuitaka GVT itimize matakwa ya DRs haraka huku wanaharakati hao wakiwataka DRs kurudi haraka kazini kuokoa maisha ya wananchi wano watetea wakiwa kama wanaharakati, vinginevyo uwana harakati wao itakuwa ni kupinga serikali tu na si maslahi kwa umma
   
 2. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Rated: ****:hand:
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkuu nasikia Wana- haraka-tu wamehamia Arumeru kukikabili Chama tawala, ni kweli au uvumi?
   
 4. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  So unataka WANAHARAKATI waendelee kusupport ukosefu wa vifaa vya kutendea kazi mahospitalini?

  Mbona MKWERRE hakuongelea kabisa ukosefu wa mikasi na gauze mahospitalini?..takwimu zile alizosoma zinasaidia nini kwa mgonjwa aliyewasili OPD?

  U should be joking meen!
   
 5. Nicas Mtei

  Nicas Mtei JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 21, 2010
  Messages: 11,569
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ntarudi tena kuisoma baadaye
   
 6. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 149
  Trophy Points: 160
  ...mkuu ungetumpuzisha ata kidogo basi!...eeehi! "TU ME CHO KA"...na tumeisha choshwa na porojo zenu za kipuuzi...alianza katibu mkuu wa afya,akafuata waziri wa afya,akafuatia waziri mkuu,juzi mwenyekiti wa CCM na leo tena wewe!?,kwa mambo yaleyale ya kijinga!?...hapana bhana haya maongezi peleke kule kwa wazee wa Dar es salaam ndo wana-muda wa kusikiliza hizi porojo za kijinga na kukupigia makofi...
   
 7. m

  massai JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: May 2, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  jk kilaza kama mwanae mwanaasha,sasa jana pale aliongea nini cha maana zaidi yakutuhadithia kilichojiri kwenye mgomo wa madaktari.sikusikia point hata moja ya maana zaidi ya porojo tu.hamna kitu pale,ni aibu tu afadhali angekaa kimya kuliko porojo zake
   
 8. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hili la opportunist nakubaliana na wewe, hawa jamaa siku zote huvizia matukio na kudandia hoja huku wakitafuta publicity kwenye media. Ukweli ni kwamba wako pale na vi-NGO vya advocacy kama sehemu ya ajira lakini uwezo wao kuhamasisha umma ni mdogo hivyo kuwafanya wavizie lolote litakalojitokeza.
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Tatizo CCM na serikali yake inadhani wanaharakati sio watanzania ,wanasema wanafanya mambo kwa wanaowapa pesa,NGO nyingi zinapata pesa kutoka kwa wafadhili wale wale wanaoipatia serikali pesa,wanawajibika kutoa ripoti za kazi zao kama vilevile serikali inavyowajibika.
  Wanaharakati wanasafari ndefu ya kuhamasisha jamii kujua haki zao na kudai kutoka serikalini kutokana na hali ya uelewa ya uhalisia ,mambo mangapi yanafanywa na wanaharakati kutetea wanyonge ambayo serikali imekuwa ikitumia vyombo vyake vya dola kuwakandamiza
  siku watanzania watakapo jifahamu kwa kweli serikali itajua umuhimu wa wanaharakati
   
 10. M

  Mukalabamu Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Wanaharakati mnawasingizia kwa sababu zenu mnazozijua,Ni lini wanaharakati walitamka kwamba wanaunga mkono mgomo wa madr?wenyewe waliunga mkono kuwa huduma bora ya afya ni jukumu la serkali,na serikali ilikuwa haionyeshi urgency kumaliza mgogoro,na kama wahusika kwenye wizara ndo waruhumiwa kwa nini wasijihuzuru? Kwa nini wasiwajibike kwa kushindwa kutatua Haya matatizo tangu yalipoanza?
   
 11. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  You are very wrong, unajua analysis zinazotolewa na wanaharakati kipindi cha budget?
  Ever heard of Budget analysis? Umeshawahi kumsikia Irenei Kiria akuwa na team yake wakiongelea swala la allocation ya budget ya Afya? how small it is, and what are the key i=areas ambazo haziguswi kila siku?

  Mkuu, wakati hawa wanaharakati wakiwa wanapambana na serikali katika level hiyo, wewe na wengine wetu huwa hatuoni kazi yao.
  sasa hapa unakuja kutuambia eti vi-NGO vyao?
  Wakati Wanaharakati wa haki za binadamu wakitoa taarifa za mauaji ya raia ambayo serikali haijachukua hatua yoyote, wakati wakisema this government should act firmly on the issues surrounding deaths of citizens in the gold mines, the right to live as a fundamental human right is to be protected by the regime........wewe hukuona kwamba wanafanya kazi?

  Tuacheni porojo, watazania tutatawaliwa na hawa wahuni mpaka mwisho wa dahari!!.......kwa mwendo huu!!!.duh!!

  Wanaharakati hawakwenda kuwa-support Drs, walikwenda kuiambia Serikali iwajibike kwa kushindwa kutoa huduma za afya na hatimae kusababisha vifo!!,

  Ni kazi ya serikali kuhakkisha huduma za afya zinatolewa no matter what, wanaharakati waliona mgomo, wakasema madaktari wanahoja, lakini ni kazi ya serikali kutatua swala lao. baada ya kuona huduma za afya hasa kwenye hospitali za rufaa zimedorora, wao wakaema. no, we cannot have a government that does not act!

  Paulss, jipange tena, apa umechemka mbaya!
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  JK hakujibu hoja za msingi, swala ni vifaa au salary? sifuri tu
   
 13. M

  Mukalabamu Member

  #13
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 53
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Tusiendeshwe tu na propaganda za serikali kujilinda na lukwepa wajibu kwa kushambulia watu wengine,wanaharakati hawakuunga mkono mgomo,walishinikiza serikali iwawajibishe walopalilia mgogoro na kuwahakikishia watz huduma bora za afya
   
 14. grndossy

  grndossy JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hivi unapomwita mkuu wa nchi kilaza unajisikiaje? Tena unamlinganisha na mwanae; hivi ungetendewa wewe hivyo ungejisikiaje. Usimtendee mwenzako usilopenda kutendewa wewe. Hata kama ana makosa ziko lugha za kuongea kama great thinkers sio kama kijiweni. Alichokosea ni nini? Je haki ya mwanadamu ni kifo au uhai? Ina maana ni sahihi madaktari kufanya madai yao kwa gharama za uhai wetu? Au wewe hujawahi kuuguliwa? Je unajua madaktari wanalipwa kiasi gani ukilinganisha na watumishi wengine wa umma? Je wao ndio wenye haki tu ya kulipwa fedha hata kama ni za bajeti yote na watumishi wengine waendelee kufa njaa? Let us be serious and realistic!!!!!!!!!!! Unapochangia jambo tafuta ukweli wa upande wa pili. Hebu fanya utafiti kidogo madaktari wanalipwaje ukilinganisha na watumishi wengine wa Serikali. Linganisha Scale yoyote ya madaktari uilinganishe na scale ya watumishi wengine wa serikali k.m. walimu, polisi, wahasibun.k. Uone jinsi ambavyo mishahara yao ni kama mara karibu tatu ya hao wengine. Sikatai kwamba wana haki ya kudai haki zao lakini si kwa gharama ya maisha ya watu na kwa kuzingatia kile wanacholipwa sasa na ukweli kwamba serikali ilishapokea madai yao.
  Hivi madaktari wakipewa malipo wanayotaka na wahasibu nao wakagoma nao wadai kulipwa kama madaktari, wao watalipwa na nani? Au polisi wakigoma itakuwaje? Wote hatuwezi kuwa madaktari, uhasibu au ulinzi ungefanywa na nani ili wao waweze kufanya kazi zao? Sisi tu mwili mmoja kila mmoja ni kiungo kwa mwenzake hakuna ambaye peke yake anaweza kufanya kila kitu peke yake. Tuache ubinafsi kila mmoja anahitaji maisha mazuri.:lock1::decision::attention:
   
 15. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  wanaharakati walikuwa wanatetea madaktari wapewe milioni 7 lakini walipinga posho za wabunge laki 2
   
 16. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Je, WANAHARAKATI au WANAHARA-KATI? Mwanaharakati haogopi kuitesa au kuipoteza nafsi yake kwa ajili ya wengine kwa mfano Mh. Godbless Lema (Mb). Lakini tumeshuhudia wanaojiita wanaharakati ni ngonjera pasina vitendo, hata pale wanapoitisha maandamano, wakitishwa na habari za kiintelejensia za Alshabab wanahara kati zoezi linaishia hapo hapo halifiki mwisho wa malengo.

   
 17. muhosni

  muhosni JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,114
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naona tuna safari ndefu kuliko tulivyodhania
   
 18. P

  Paul S.S Verified User

  #18
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu nahakika hujasoma vizuri bandiko langu vizuri, vinginevyo usinge niuliza hivyo
   
 19. F

  FJM JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kwa kumbukumbu zangu, wanaharakati waliingilia kati wakiwa na ujumbe mmoja tu "serikali ingilie kati mgomo wa madaktari kwa sababu watu walikuwa kwenye hatari ya kupoteza maisha". Hili ndilo walilokuwa wanasema muda wote, na walizidisha sauti pale Spika wa bunge alipokataa (mara sita) hoja za wabunge toka vyama vyote kujadili mgomo huo.

  Kauli aliyotoa rais jana inatoa picha inayosema kuwa wanaharakati walikuwa 'wanashinikiza mgomo bila kujali uhai wa watanzania'. Hii sio sahihi kabisa na sielewi kwa nini rais na team yake wameamua kugeuza mantiki nzima ya message ya wanaharakati?

  Pia kwenye ujumbe wake, rais ameonekana kuthamini (walau kwenye hotuba ya wazee wa Dar) uhai wa watanzania. Hili ni jambo zuri, lakini ningetaka kujua ni kwa nini hatumjaskia rais akiongea kuhusu mauji ya raia wasio na hatia yanayofanywa na polisi? Nyamongo, Mbeya, Arusha, Songea n.k! Ni lini rais atawaita wazee (wa mkoa wowote) ni kuwasema polisi kama alivyowasema wanaharakati? Kama kweli serikali inathamini uhai wa raia wake basi iko haja kuweka mambo yote hadharani na kwa kuanzia Polisi imulikwe.
   
 20. P

  Paul S.S Verified User

  #20
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  I better reserve my comment.............. sioni hoja zenu

  Mkuu natambua kazi nzuri wanayofanya........ lakini katika hili la mgomo wa DRs sidhani kama waliangalia pande zote mbili kwa maslahi ya wananchi wanaodai wanapigania haki zao za msingi ikiwemo kuishi
   
Loading...