Mgomo wa Madaktari na wanaharakati wetu

Mkuu.. Hivi unadhani Madaktari walikuwa wanafurahia huo mgomo..? Au unafikiria Madaktari ni wakatili na hawana huruma hata kidogo..? Hii ndo dhana ambayo inalazimishwa kwa jamii kwamba Madaktari ni katili..! Unfortunately na ww kwa makusudi au bahati mbaya unasaidia kuisambaza hii dhana.. Ningependa Paulss uombe kwamba Serikali i-meet Doctors' demand halfway.. Badala ya kuendelea kujaribu kuwa-portray vbaya Doctors..
Sisi tutajuaje mkuu wangu kama walikuwa na uchungu?.. Hivi kweli unaweza kuletewa mgonjwa mahututi ukamfungia mlango usoni ukisema:- Tumefunga hakuna huduma tupo ktk mgomo...Halafu unasema walikuwa na uchungu sana kumwona mtu akifa na sio kwamba kifaa hakikuwepo au dawa ila kumtolea yeye mfano jinsi serikali ilivyokuwa haisikii madai yao na madai yenyewe mawaziri wajiuzuru kwanza na sio waletewe dawa au vifaa vya kazi kwanza!..Dah! ama kweli kazi ipo!
 
Mkandara, hapo kwenye Red nilikuwa namjibu Paulss. Ili kujua kwa nini niliandika, fuatilia majibizano yalikoanzia na ndiyo utaelewa kwa nini. Na sikuandika hivyo ili kujisifu, la hasha. Ilikuwa kama "unanitishia hivi, na mie ntakutishia hivi."
Ndiyo maana Paulss akaja na majibu "Ataniwekea picha za waliopona kwa babu na kuweka alama..... lol

Mkuu, Traffic Polisi wakikukamata kwa kwenda high speed kwenye highway, huwa wanakiri kabisa kuwa wengi wanakwenda highspeed. Ukikamatwa basi una mkosi. Kuna miaka ya 90 nilikuwa kwenye sehemu ya mazoezi na tukiwa barabarani, pembeni wamesimama traffic, ghafla wakalisimamisha gari kwa mwendo kasi. Ila wakiwa wanaongea na driver, likapita gari kwa speed kubwa zaidi ya jamaa na wakamwacha jamaa na kuingia kwenye gari lao na kuanza kumfukuza huyo mvunja sheria zaidi. Hii haina maana huyu wa mwanzo hakuwa na makosa.

Pia, sheria nyingi duniani zilikuwa zinavunjwa kwanza na walipoona kuwa ni imekuwa too much, wakaona iwekwe sheria kuzuia uharibifu huo. Akifufuka leo Nyerere na umwambie kukopi CD ya mwanamuziki au film na kuiweka kwenye Internet ni dhambi atashangaa sana maana wakati anakufa, akina Kazaa walikuwa wanapendwa sana duniani. Ila ilivyoanza kuwa too much, ikawekwa sheria kuzuia hii kitu.

Aliyekufa enzi wameanza kupiga marufuku kudownload miziki online na akafufuka na kukuta wewe unadownload kwenye Itunes, atashangaa sana na kukuambia "Watakufunga wewe." Na wewe unamwambia sasa ni ruhusa ila UNALIPIA.

Hawa Mawaziri na viongozi wa Wizara ya Afya, ni kweli kabisa kuwa si wao pekee wazembe kwenye Serikali ya Kikwete au CCM. Karibu wote wameoza na hawafai kabisa. Inawezekana angelikuwa Rais mwingine, pamoja na Uozo wao, nina uhakika wangelikuwa na nafuu nafuu sana. Bob Marley aliimba "Ukimpa centimeter atachukua meter."
Ila cha muhimu ni kuwa sasa Watanzania tumeona imekuwa too much. Sasa Madokta wameona kuwa imekuwa too much. Sheria inabidi ipitishwe ili hili jambo libadilike. Lazima awepo mtu kumfunga paka kengele na wakaona waanze wao wakitegemea Watanzania wataingia barabarani kudai UOZO huu uondolewe. Tungelianza na hawa akina Mponda na tukahamia kwa Ngereja au Kawambwa, wengine wangelianza kubadilika.

Sasa unategemea mtu kama Malima anajali sana matatizo ya binadamu? Mtu anajua tu kula goodtime na Machangudoa wa Kitusi na hajali hata usalama wake kwani na mdudu anavyotesa Tanzania, bado mtu anajiokotea kwenye mabaa.
Watanzania wanalala giza, yeye na Boss wake Ngereja wanatesa na Machangudoa ovyo ovyo.

Malima: ALIYEMUIBIA WAZIRI MALIMA NI CHANGUDOA - Global Publishers

Ngereja: https://www.jamiiforums.com/celebri...club-na-aunt-ezekiel-usiku-wa-manane-dom.html

Magufuli, baada ya kuuza nyumba za Serikali, anawaambia watu wa Kigamboni kama hamna hela, OGELEENI. Halafu unataka nikae meza moja na huyu mtu aliyelewa madaraka. Yeye pia kauzia hadi nyumba ndogo mali ya serikali.

Watanzania ACHA TUFE ndiyo tutatia akili zetu uelewa. Mkandara na Paulss mnahuruma sana ila kumbuka kitabu cha Ezekiel Kezilahabi cha GAMBA LA NYOKA anaposema kuwa, hili ni JIPU SASA. Ni lazima kulipasua ingawa kupasua, kuna husisha maumivu makali sana. Msiwe na huruma kwa Watanzania maana hizo HURUMA ndiyo zilizotufikisha hapa. Watu wakifa saana kwa kukosa huduma, watakumbuka na kuelewa mbaya wao ni nani. Wasipoelewa, basi taifa zima halifai, acha wafe wote na Wahindi/Wachina watakuja kuishi Tanzania. Hata Palestine wana shida sana ya ardhi wanaweza kuja kuishi kama siyo Wakenya wanaouwana kwa kukosa ardhi. LET US DIE.

Sikonge,
Mkapa kasema hivi huko Arumeru - "Wapinzani ni wajinga na hawana Adabu". Sasa mtamfanya nini huyu mzee, mtagoma uchaguzi hadi avuliwe uanachama wa CCM?.

- *Unajitolea mfano wa kupona bila kwenda Hospital kama kigezo mkuu wangu?... Dah! haya sasa madaktari wa nini? basi tusiwalipe kabisaa hawana maana.
 
Jana wakati Rais JK anaongea na wazee wa DSM aliligusia hili la wanaharakati wetu jinsi walivyoshiriki katika mgomo huu, ingawaje kwa walio wengi ambao walisapoti Drs hili wataliona ni moja ya porojo alizokuwa anazipiga Mzee wa Kaya.
Wakati ule wanaharakati walipo ingilia kati kwa kusapoti DRs kwa asilimia mia moja wenye akili timamu tulihoji,
tulihoji kuwa kweli wanaharakati hawaoni na upande wa pili kuwa wananchi wanaowasimamia katika harakati zao wanaumia kwa vita ya GVT vs DRs, kwa bahati mbaya hatukueleweka

Nadhani hii ni changamoto kubwa kwa wanaharakati wetu kuangalia upya kile wanacho kitetea kwa maslahi ya mwanachi wa chini kabisa
Kwenye mgomo huu Ingawaje DRs walikuwa na madai yao ya msingi ambayo GVT ilionyesha nia ya kuyatekeleza wanaharakati hawa walikuwa kimya hadi pale DRs walipotaka viongozi wa kisiasa wawajibishwe kwanza ndio maswala mengine yafuatie ama sivyo mgomo moja kwa moja
Hapa sasa waliibuka from no where na kuanza kushinikiza mawaziri wawajibishwe na kuunga mkono mgomo uendelee hadi watolewe mawaziri.

Binafsi nilijiuliza sana kwamba ni kweli DRs wanasuguana na GVT kuhusu madai yao na hapa wanao umia ni wananchi, je wanaharakati ni lazima walalie upande mmoja wa DRs na kuacha wananchi wakitaabika, hivi walifanya juhudi gani kuhakikisha wanatetea maslahi ya mwanachi wa kawaida anayeuza vitumbua na maji akakuta Drs wamegoma na mfukoni ana pesa ya kumudu gharama za hospitali za serikali tu.

Kweli walimfikiria mwananchi huyu au walifikiria JK ni mgumu kuwajibisha wateule wake na sasa watumie mwanya huo kushinikiza bila kujali athari kwa wananchi wano watetea?

Je wanaharakati wetu ni ma opportunist wanao subiri tukio ndio waonekana kwenye media "kutetea" wananchi?
To be frank sijawahi kusikia wanaharakati wetu hawa wameibua hoja na kuivalia njuga zaidi ya kusubiri matukio pamoja na kuwa wanafanya kazi nzuri kiasi

Je kuwa mwanaharakati ni nini? nikuwa againt GVT muda wote hata kama kufanya hivyo ni kuumiza wananchi wasio na hatia kwa mambo yasiyo na ulazima

Mtazamo wangu nadhani ni vizuri wanaharakati hawa wakaangalia maslahi ya wananchi kwa ujumla hasa linapokuja swala la uhai wa watu, nilitarajia wanaharakati wangekuja na msimamo wa kuitaka GVT itimize matakwa ya DRs haraka huku wanaharakati hao wakiwataka DRs kurudi haraka kazini kuokoa maisha ya wananchi wano watetea wakiwa kama wanaharakati, vinginevyo uwana harakati wao itakuwa ni kupinga serikali tu na si maslahi kwa umma

Mkuu Drs na wanaharakati hawakukosea kama vile unavyotaka kutuaminisha hapa jf. Drs na Wanaharakati wanauzoefu na utendaji kazi wa jk kwamba ni mtu mwenye kichwa kigumu (kichwa cha nazi). Hawezi kufanya jambo lolote bila mashinikizo ya nguvu. Chukulia mfano mgomo huu wa drs mkuu jk alipata tetesi mapema sana kuhusu mgomo na madai ya drs lakini hakuchua hatua zozote za kuongea nao kabla ya madhara hayajatokea, badala yake alichofanya ni kwenda zake kuinjoy hali ya hewa ya mlima kimanjaro wakati watu wanaendelea kufa bila matibabu. Kwa hiyo wakulaumiwa siyo drs wala wanaharakati bali ni jk asiye na mbinu ya kukabiliana na majanga kabla hayajasababisha madhara makubwa. Paulss tafadhali acha umbaiwayu onaga mambo katika mwanga angavu achana na mambo ya ukungu mzito.
 
Mkandara,

To be, or not to be, that is the question.

Ni maneno yaliyopo kwenye mchezo wa Hamlet kutoka kwa Shakespeare. Sijui kama umeshawahi kuyafuatilia zaidi au lah. Kama bado basi samahani maana nimekupa neno ambalo umelitafasiri vibaya.

Ukiweza basi lifanyie Homework na kujua kwa nini kwenye vita vya pili vya dunia, Waingereza (PM Churchill) alilitumia hili neno na nini kilikuwa matokeo yake. Kwa hint tu: Rubani saba wa kiingereza, waliotumwa kwenda USA, walitunguliwa na Wamarekani ndani ya jet-fighter zao kama ndege na wote kufa.

To be, or not to be, is more than PLAY SCENE.

We ain't making a play scene!
Mkapa hakutuambia sisi tuna wivu wa kike na hatuna elimu na bado leo ndio mnasema Kiongozi bora kuliko wote? mbona dharau hizi za viongozi zipo miaka yote na mnaendelea kuwachagua kama wabunge wetu..Unajua fika kabisa kwamba viongozi wetu wapo juu ya sheria halafu mnataka hao hao watoe hukumu. Kesi ya Ngedele kumpelekea Nyani, tofauti mnachagua nyani gani anayefaa. Yet bado mnashindwa kuelewa sisi tumesimama wapi? Ama kweli usistaajabu ya Mussa...
 
Wanaharakati wa Tanzania wengi wamejikita kwenye NG0 kwa ajili ya maslahi yao binafsi ni watu hatari sana kwa mustakabali wa taifa letu.
 
Sikonge,
Ulichoandikahapo juu sipingani nacho hata kidogo wala sisemi hawa madaktari walikuwa na makosa kuweka madai yao na hata mgomo ila kama uliwahi kunisoma nilizungumzia kiwango cha mgomo na kisha kubadilika kwa sababu ktk majadiliano. Kwa kila hatua ya mgomo ule nilieleza kuitoridhika kwangu kwa hatua zilizochukuliwa na madaktari hawa.

Sasa ikiwa tumechoka na huduma mbaya za serikali na hasa mawaziri kwa nini tunarudia yale yale ya kumwondoa Waziri kama ndio dawa ya ukosefu wa huduma nzuri nchini?. JK kabadilisha baraza la mawaziri zima, wala sii mara moja kutokana na kutoridhika kwetu, na akawaachisha baadhi karibu kila mwaka kuna mabadiliko lakini wapi!...Mchezo ni ule ule kila anayeingia madarakani anafanya hivyo hivyo ina maana makosa sio mawaziri bali MFUMO mzima wa Utawala. Na nikasema katika AFYA ni wapi makosa yalipo na tuyazungumzie. hakuna Mtanzania hata mmoja anataka kuyazungumzia kwa sababu yanawagusa kiimani na pengine kimaslahi.. Sasa, utamfukuza Mponda na Nkya ili iweje?. Nini sababu haswa? tunaambiwa hawa wana jeuri, jamani kuna kiongozi asiyekuwa na jeuri?..

Jamani hata Hospital sisi wananchi hukutana na jeuri za madaktari hadi unaomba mbingu ipasuke.. Mwanamke anazaa kwa matusi tena ya nguoni lakini ndivyo tulivyojenga Taifa la watu jeuri na washenzi na ili kuondoa Ujeuri na ushenzi kama huu inabidi kufumua mfumo mzima wa Utawala. Kwa nini walibadilisha toka madai makubwa na muhimu kwenda ktk kujiuzuru kwa mawaziri -nilihoji! na kusema hapo ndipo walipoacha silaha kubwa wakachukua bastola wakati Machine gun bado imejaa risasi.. Ni makosa ambayo nili yazungumzia pia sikukubaliana kuwaacha wagonjwa wahtuti bila kuhudumiwa ..Vita hii ni yetu sote including huyo mgonjwa.

Silaha yetu kubwa sisi wote ni KATIBA mpya na hapo tuhakikishe mabadiliko makubwa sana na sii kurekebisha iliyopo. Uchaguzi wa mwaka 2015 uwe fundisho kwa viongozi na watawala wote ya kwamba mabadiliko ni lazima na katika harakati hizi tunatakiwa kuunda UMOJA na sio madaktari kivyao, vyama vya Upinzani kivyao tukiogopa utawala unaotutenga makusudi ili tutawalike..
 
ni lini na wapi wanaharakati walisema wanasupport madr wapewe kiasi hicho cha hela?acheni upotoshaji na kutumiwa na wanasiasa kisha mnatupwa kama condom
 
YouTube - Last Poets, the - Niggers Are Scared Of Revolution Kuna poem hii inayosema "Niggers are scared of revolution"...ukisikiliza kwa makini ni kama vile anazungumza na sisi waswahili pia! Tunappenda sana mabadiliko lakini hatutaki kupita njia ya kuelekea huko...Afande Sele aliwahi kuimba kama unapenda pepo kwa nini uogope kifo? Tunaweza kuwalaumu madaktari na wanaharakati tutakavyo na tukachagua kuiamini serikali hii itashughulikia matatizo ya sekta ya afya...lakini tusisahau mwezi wa sita hauko mbali, bunge la bajeti litakaa na hapo tutaona hizo ahadi tamu zimetekelezwa kwa kiasi gani!!
 
YouTube - Last Poets, the - Niggers Are Scared Of Revolution Kuna poem hii inayosema "Niggers are scared of revolution"...ukisikiliza kwa makini ni kama vile anazungumza na sisi waswahili pia! Tunappenda sana mabadiliko lakini hatutaki kupita njia ya kuelekea huko...Afande Sele aliwahi kuimba kama unapenda pepo kwa nini uogope kifo? Tunaweza kuwalaumu madaktari na wanaharakati tutakavyo na tukachagua kuiamini serikali hii itashughulikia matatizo ya sekta ya afya...lakini tusisahau mwezi wa sita hauko mbali, bunge la bajeti litakaa na hapo tutaona hizo ahadi tamu zimetekelezwa kwa kiasi gani!!
Sasa huyo mgonjwa anayekufa hospital kwa kukosa kutibiwa anapigana vipi na serikali akisha kufa ama kufa kwake?..
 
Sasa huyo mgonjwa anayekufa hospital kwa kukosa kutibiwa anapigana vipi na serikali akisha kufa ama kufa kwake?..

Mkuu moyo huu wa huruma tulioonyesha kwa wagonjwa walioathirika na mgomo natumaini tutaendelea kuuonyesha kwa wananchi pale watakapoendelea kuathirika na hata kupoteza maisha kutokana na ukosefu wa madawa na vifaa vingine, vitanda na n.k. Tuendelee kuwa wakali hivi hivi! Ndio maana nikasema ngoja tusubiri bajeti isomwe sio mbali sana tutaona kweli nia ya serikali ni ya dhati au ni gumashi...
 
Hapana, ni sisi ndiyo tulitakiwa kupigana na Serikali ili mgonjwa apone.

Serikali ya CCM inatawala kwa raha sana kwa sababu, In Every action they take, there is no equal and opposite reaction.

Kwa sisi watanzania kuvunja Newton's law, hii imesababisha vifo hivyo. Waliosababisha siyo Madokta wala Serikali/Kikwete ila ni sisi Watanzania ambao tumekaa kimya kama mikondoo. Damu zao zipo mikononi mwetu maana hao jamaa wamekufa na wataendelea kufa wengine/tutaendelea kufa kama hatutabadilika.

Nakubaliana na wewe Mkandara, KATIBA MPYA ndiyo itakuwa dawa. Ila bado pamoja na kuwa na katiba mpya, kama Mitanzania itaendelea kuwa Mikondoo, tutatukanwa sana na akina Mkapa kuanzia "hatuna akili, tuna wivu wa kijinga, mbayuwayu, ukitaka kula kubali uliwe kidogo ....... na mengine mengi."
Sasa huyo mgonjwa anayekufa hospital kwa kukosa kutibiwa anapigana vipi na serikali akisha kufa ama kufa kwake?..
 
Hapana, ni sisi ndiyo tulitakiwa kupigana na Serikali ili mgonjwa apone.

Serikali ya CCM inatawala kwa raha sana kwa sababu, In Every action they take, there is no equal and opposite reaction.

Kwa sisi watanzania kuvunja Newton's law, hii imesababisha vifo hivyo. Waliosababisha siyo Madokta wala Serikali/Kikwete ila ni sisi Watanzania ambao tumekaa kimya kama mikondoo. Damu zao zipo mikononi mwetu maana hao jamaa wamekufa na wataendelea kufa wengine/tutaendelea kufa kama hatutabadilika.

Nakubaliana na wewe Mkandara, KATIBA MPYA ndiyo itakuwa dawa. Ila bado pamoja na kuwa na katiba mpya, kama Mitanzania itaendelea kuwa Mikondoo, tutatukanwa sana na akina Mkapa kuanzia "hatuna akili, tuna wivu wa kijinga, mbayuwayu, ukitaka kula kubali uliwe kidogo ....... na mengine mengi."
Nakubali kabisa kwamba sisi ndio tulitakiwa kupigana ili mgonjwa apone, tatizo nalolisema ni pale mgonjwa anapotumiwa kama human shield kaa wanavyofanya wale wapiganaji wa Syria. Madai yao kuondolewa kwa Assad ni ya haki kabisa na yanaunga mkono lakini wanapojificha ndani ya majumba ya watu na kuwazuia kutoka wakijua kuna watoto, wanawake na vizee ndipo napopinga mimi.

Madaktari wanataka kupambana na serikali zipo njia nyingi sana tena rahisi kabisa ambazo zote zimekiukwa. Nimejieleza sana tu huko nyuma na hata kusema madai yao yalikuwa ya msingi lakini ile kuahirisha mazungumzo kwa sababu sijui wanasubiri watu kutoka bara, mara hawamtaki Mponda na Nkya jambo ambalo lingeweza kabisa kuepukwa ndio kero yangu. Na umwondoe Mponda na Nkya ili iweje ikiwa hii ni vita na hao ndio majemedari wa serikali?. Wameweza vipi kufika Ikulu safari hii na walishindwa zamani? Na wamekubali kwa ahadi gani ambazo zina thamani ya maisha ya watu waliopotea.

Hii haikuwa vita dhidi ya serikali bali ilibadilishwa na kuwa vita baina ya WATU wakitaka mtawala yule yule Kaizali atoe maamuzi ya kuondoa majemedari wake. Ilikuwa vita yao wenyewe na mifano kibao walituonyesha kutopenda mtu yeyote aingilie as if ni hostage taking! watu wanakufa mikononi mwao na sii kwamba hawawezi kuwaponyesha ila kuwaonyesha serikali mwanaume nani? Narudia kusema Udaktari sio Silaha bali ni nyenzo ya kuponya watu na unapoitumia kama silaha hapo ndipo makosa yanapojitokeza.
 
Nakubali kabisa kwamba sisi ndio tulitakiwa kupigana ili mgonjwa apone, tatizo nalolisema ni pale mgonjwa anapotumiwa kama human shield kaa wanavyofanya wale wapiganaji wa Syria. Madai yao kuondolewa kwa Assad ni ya haki kabisa na yanaunga mkono lakini wanapojificha ndani ya majumba ya watu na kuwazuia kutoka wakijua kuna watoto, wanawake na vizee ndipo napopinga mimi.

Madaktari wanataka kupambana na serikali zipo njia nyingi sana tena rahisi kabisa ambazo zote zimekiukwa. Nimejieleza sana tu huko nyuma na hata kusema madai yao yalikuwa ya msingi lakini ile kuahirisha mazungumzo kwa sababu sijui wanasubiri watu kutoka bara, mara hawamtaki Mponda na Nkya jambo ambalo lingeweza kabisa kuepukwa ndio kero yangu. Na umwondoe Mponda na Nkya ili iweje ikiwa hii ni vita na hao ndio majemedari wa serikali?. Wameweza vipi kufika Ikulu safari hii na walishindwa zamani? Na wamekubali kwa ahadi gani ambazo zina thamani ya maisha ya watu waliopotea.

Hii haikuwa vita dhidi ya serikali bali ilibadilishwa na kuwa vita baina ya WATU wakitaka mtawala yule yule Kaizali atoe maamuzi. Ilikuwa vita yao wenyewe na mifano kibao walituonyesha kutopenda mtu yeyote aingilie as if ni hostage taking! watu wanakufa mikononi mwao na sii kwamba hawawezi kuwaponyesha ila kuwaonyesha serikali mwanaume nani? Narudia kusema Udaktari sio Silaha bali ni nyenzo ya kuponya watu na unapoitumia kama silaha hapo ndipo makosa yanapojitokeza.

Mkandara,

..wakati kuna mgomo JK aliondoka nchi akenda zake Davos.

..alipotoka Davos akaenda Botswana kwenye sherehe za chama tawala cha huko.

..wakati wote huo wananchi wanateseka, wagonjwa wanakufa.

..kitendo hiki wewe unakichukuliaje?

..hivi Maraisi wengine wakikabiliwa na mgomo wa madaktari nchi nzima wanaweza kweli kusafiri nje ya nchi???

NB:

..ilifika mpaka mahali bunge lililosheheni wabunge wa CCM likaamua kuingilia kati.
 
Mkandara,

..wakati kuna mgomo JK aliondoka nchi akenda zake Davos.

..alipotoka Davos akaenda Botswana kwenye sherehe za chama tawala cha huko.

..wakati wote huo wananchi wanateseka, wagonjwa wanakufa.

..kitendo hiki wewe unakichukuliaje?

..hivi Maraisi wengine wakikabiliwa na mgomo wa madaktari nchi nzima wanaweza kweli kusafiri nje ya nchi???

NB:

..ilifika mpaka mahali bunge lililosheheni wabunge wa CCM likaamua kuingilia kati.
Hapana mkuu wangu waligoma baada ya JK kuondoka na nilisema wazi kwa nini haikuwa kabla maana safari yenyewe tuliijua week nzima kabla (tafuta safari za JK) hajaondoka.. WHY haikuwa before hajaondoka!..
 
Mkandara, uko sawa kabisa.

Ila sasa hebu niambie, hao wanne waliotakiwa kufukuzwa kazi kwa Ubabe wao na uzembe kama wewe ni Daktari, utaongea nao? Watu tunakosea sehemu ndogo sana kwa kuacha kujiuliza, kwa nini hawawataki hao wanne?

Je hawa Madaktari wamepata ugonjwa gani hadi ghafla bin vuu waanze kutamka "hawa wanne hatuwataki?"

Tatizo ni LUGHA na DHARAU wanazofanya hawa viongozi. Wangeliondolewa hawa, walau wengine wangelianza kuongea na Watanzania kama binadamu.
Unakumbuka kesi ya Ngereja na yule Mlinzi wa Bank? Ngereja kukumbushwa tu kuwa asiongee kwenye kibanda cha kuchukulia pesa kwa sababu watu wanasubiri, Mlinzi wa watu akafukuzwa kazi na matusi tu....."Unanijua mimi ni nani wewe?" Huu ubabe wa "Nitakuonyesha" ndiyo ambao umewaudhi zaidi Madokta na si hayo mengine. Ni heshima kidogo tu kama msomi, binadamu, mtu mzima ambaye kila siku anacheza na magonjwa hatari ili kuokowa maisha ya Mtanzania. Leo anatukanwa na kuchekwa kama ni Msukuma mkokoteni au Mgogo Mchoma mkaa.

Hapa zaidi ilikuwa inategemewa kuwa wakigoma kumtibu mgonjwa yeyote, Watanzania wataingia barabarani siku hiyohiyo kuandamana. Matokeo, Watanzania wakaanza kuwacheka Wana harakati kwa kuandamana kwao na Polisi tayari wakaanza kushika virungu kuanza kazi.

Ukitaka kujua wenzetu, Mjinga mmoja hapo Canada kwenu, aje na kupitisha kisheria cha ajabu au kauzembe ka ajabuajabu na PM amtetee huyo mtu. Utaona watu hawatampa hata muda anywe chai. Wataacha kila kitu na kula naye sahani moja. Sisi Mawaziri ufuska tu na kutukana Watanzania na Mitanzania inakubali. Sasa wewe Mkandara UNAITETEA YA NINI?

Narudia tena, maadam akili zetu hazina akili, ACHA TUFE TU. Hizo huruma zenu wapelekeeni wanazozihitaji. Sisi Watanzania tutaenda kutibiwa kwa kutumia Kikombe Kimoja huko Loliondo kama siyo Tabora na wapi sijui?

Mchungaji%2BMstaafu%2BAmbilikile%2BMasapile%2B(kushoto)%2Bakimpa%2Bdawa%2BWaziri%2Bwa%2BNchi%2BOfisi%2Bya%2BWaziri%2BMkuu%2B(Sera%2Bna%2BUratibu)%2C%2BWilliam%2BLukuvi%2Bna%2BRosemary%2BNyerere%2Bmwishoni%2Bmwa%2Bwiki%2Biliyopita..jpg
Lukuvi na Binti Rose-Mary Nyerere.

And the winer is ............................
babu2.jpg
 
Kuna msemo unasema vita vya panzi furaha kwa kunguru.. na hapa kunguru ni wanaharakati
Pia upo unao sema vita ya mafahari wawili aumiae ni nyasi................hapa nyasi ni sisi akina kajamba nani
 
Mkuu wangu sijui kaa unalitazama swala hili kwa uwazi na open minded. hao kina mama wanaokwenda tibiwa na matusi hukataa tiba kwa sababu daktari kamtukana? Na unaweza kweli kumchagua daktari mwingine badala ya huyo ili utibiwe! Mkuu wangu tunazungumzia Tanzania hii ama nchi nyingine!

Madai ya madaktari yalikuwa Posho kwanza, wakaongeza mishahara kisha na mazingira ya kutendea kazi yakaongezwa juu. Pamoja na kuwepo makosa bado madai haya tunayakubali lakini wapoweka vikwazo jambo ambalo tulitegemea kutoka serikalini ndipo waliondoka ktk hoja ya msingi na kuanza kuonekana kwamba mgomo ule ulihusu kumwondoa Nyoni, Mponda na Nkya madarakani. Kulenga kufanya hivyo inawaweka madaktari ktk mchezo wa kisiasa unaoitwa kuunda FITNA kumwondoa mtu madarakani. Na hakuna kitu kibaya kama utaambiwa wewe mwache mkeo kwanza ili upate kuzungumza na hata mzazi wako, hapo mkuu wangu anayekwambia hivyo atakuwa kapoteza hoja yake ya kwanza.

Hii ya kujiuzuru hao watu, mimi Mtanzania maskini haitoweza kunisaidia kitu ikiwa viongozi wote wana tabia hiyo. Kaondoka Chenge akisema vijisenti, kaondoka mshikaji wa karibu wa JK marehemu Dito na bado viongozi wanatukana na wanabeba bastola. Unataka mifano gani zaidi ili mkubali kwamba tatizo sio watu bali mfumo uliopo ndio MBOVU.. Jamani mara ngapi nirudie maneno haya haya..

Nyerere alifanya nini kuondoa Unyapala wa mawaziri?.. jambo dogo sana tu - Hakuna UHESHIMIWA - kila mtu ni NDUGU yako..tukaitana sana ndugu, kaka na mshikaji na kadhalika lakini uheshimiwa ukafa.. Neno moja tu la mheshimiwa linampa mtu yeyote kiburi maana huu sio utamaduni wetu ila kukuzwa kuwa nyapala kama Jela ama Jeshini. Na wala usifikirie kwamba hapa Canada ndio hawafanyi hivyo, wanafanya sana tu isipokuwa kwa kufuata sheria na wajibu. Huwezi kumlazimisha Waziri mkuu amwondoe waziri wake kwa sababu ana dharau, zitatazamwa dharau zenyewe kama anaweza funguliwa mashtaka na hapo ndipo anaweza kuondolewa kupisha uchunguzi kama walivyofanya kwa Nyoni lakini sio kiongozi aondolewe tu madarakani kama kukomoana wakati vyombo vya sheria, bunge na hata washauri wapo.

Ni makosa madogo madogo kama haya ndio yanatuponza. Tupige vita Posho za wabunge na viongozi wote watumishi wa serikali ili tupange mishahara bora ngazi zote na posho ziwe tu kwa kutumikia kazi ulopewa ambayo utarudisha stakabadhi za kuonyesha umezitumia vipi, hizi hazitakuwa pato la mtumishi bali matumizi ya serikali. Tuvunje muundo wa AFYA uliopo maana umeshindwa kuboresha huduma hii nchini. Na tuvunje mfumo wa ELIMU, MADINI, TAX EXEMPTION, IMPORTS na kuziba miaya yote ya Ufisadi inayotokana na nguvu kubwa tulowapa mawaziri na viongozi wa sekta tofauti. Tanesco na mashirika mengine yawe responsible moja kwa moja na maendeleo ya mashjirika hayo, serikali itaingilia tu ikiwa Tanesco wanaomba fund zaidi au kuonekana kuzembea tena basi ushauri wangu labda libinafishwe na kuingia DSE tuchague viongozi wetu.

Kuwafukuza mawaziri was a low blow!.. mbona walikubali kukaa tena wakati mishahara haijabadilishwa isipokuwa ahadi hewa?, leo kweli walitegemea Pinda angeweza kuwafukuza mawaziri within 72 hours wakati sii jukumu lake bali la rais?. Acha hivyo mbonna wamekubali kuacha mgomo leo kwa kupewa nini kama sio ahadi zile zile. What have they gained so far? maana mawaziri hawajafukuzwa bado tunasubiri ahadi zile zile kama walivyopewa mara ya kwanza. I doesn't make sense! Mkuu sikusoma kama wao lakini nadhani Umri wangu umekuja na busara na hekima ambayo wao hawana..
 
Mkuu hata mimi naweza kukuweka picha za watu kibao waliopona kutokana na hospitali hizi hizi kabla ya mgomo, mmoja wapo nikiwa mimi mwenyewe nilipelekwa hoi bin taabani:focus:

Mkuu kwanza naomba unielewe sipo hapa kuitetea GVT hapana, nipo hapa kuangalia pia nini wajibu wa hawa DRs juu ya dhamana ya afya zetu, Mkuu Mkandara amelijengea hoja vizuri sana hili.
Iweje uhai wetu uwe ndio dhamana ya madai yao, na kibaya zaidi wamekubaliana mambo ya msingi yatafanyiwa kazi lakini wao wanasema hayo ya vifaa vya hospitali na huduma bora weka kando kwanza, ili turudi kazini toa kwanza waziri na naibu vinginevyo acha watu ajifie...... hili sita kaa nilielewe kamwe
Kama serikali ilikuwa imeisha fanya upumbavu wa kupuuzia madai ya msingi na baadae ikajirudi kulikuwa na sababu ya ndugu yangu kufa kwasababu mponda bado ni waziri? hapa ndipo tunalazimika kuangalia na upande wa shilingi je role yao katika hili ilikuwa vipi?



Naamini hata huduma za afya zikiwa mbaya sana bado kuna watu watakwenda hospitalini na kupona. Nikiwa na maana ulipona kwa bahati nzuri yako - yawezekana ulipokewa na Dr mwenye roho pana. Pia yawezekana mwili wako wenyewe ulipougua ulipata nafasi ya kujijengea nguvu ya kutosha kupigana na vidudu vya magonjwa.

Angalia mambo kwa upana wake, drs wana madai ya msingi na raia pia ni kweli wanahitaji huduma zuri ya afya - kubalance hapo inabidi kuchambua tatizo na kulitatua - mchawi wetu si ma drs. Mgomo wao ulitokana na chenga ama ahadi hewa za serikali za muda mrefu.

Sote tunajua kua waajibu wa Drs juu ya afya zetu ni vile ambavyo wote hapa tungependa iwe - yaani kwamba Drs wahakikishe wanawahudumia raia. Lkn hapo hapo tukumbuke hao Drs nao ni watanzania na wanaishi nasi na wanajua vipato vya TRA, Wabunge, nk nafasi wanazopewa viongozi kutibiwa nje ya nchi kwa gharamba kubwa - Sasa kwa nini tunataka Drs waonyeshe uzalendo zaidi ya Raisi wa nchi ama Mawaziri ama na Wabunge? Ukiangalia zaidi hutakosa kuona madai ya drs yana UZALENDO, hasa kwa dai la kutaka mazingira ya kazi kuboreshwa kama ilivyo TRA, nk.
 
Sikonge,
Mkapa kasema hivi huko Arumeru - "Wapinzani ni wajinga na hawana Adabu". Sasa mtamfanya nini huyu mzee, mtagoma uchaguzi hadi avuliwe uanachama wa CCM?.
Irrelevant and out of context!!:A S 13:
 
Hapana mkuu wangu waligoma baada ya JK kuondoka na nilisema wazi kwa nini haikuwa kabla maana safari yenyewe tuliijua week nzima kabla (tafuta safari za JK) hajaondoka.. WHY haikuwa before hajaondoka!..
Mkandara acha fix,
Kikwete aliondoka jioni ya tarehe 24 Jan,
Mgomo wa madaktari ulianza tar 23 Jan,
Kumbuka ulishakuwa umetangazwa lon time before that!!
 
Back
Top Bottom