Mgomo wa Mabasi, case study Japan!

Kijakazi

Platinum Member
Joined
Jun 26, 2007
Posts
10,638
Reaction score
18,315
Japani wanavyofanya wakileta tanzagiza madereva sijui watasemaje kwa mfano, ni hivi japani kituo cha mabasi kama kile cha mbezi kuna kituo cha polisi ambacho kina dirisha la kioo kama vile dirisha la bank teller, asubuhi madereva wakifika kitu cha kwanza wanakabidhi leseni kwa trafiki polisi dirishani kama vile benki unavyompa kadi yako ya benki dirishani halafu askari anampa dereva kipima kilevi na dereva anaweka mdomoni kupima kama amekunywa (kunywa pombe maana yake kama pombe hata ya jana bado iko) pombe/drugs au la.
halafu baada ya kutoa mdomoni anarudisha kwa polisi, kama majibu ni negative unarudishiwa leseni (yako) na kuendelea na kazi kama ni positve leseni hairudi ni kama vile tu benki ambapo kuna mazingira pia wanaweza wasikurudishie kadi yako na wakaifungia, dereva anarudi nyumbani na ndiyo imeisha hiyo.

kulingana na kiwango cha kilevi/drugs alichokutwa nacho, anaweza kurudishiwa (leseni) baada ya kutozwa faini, kurudishwa shuleni kwa gharama yake ofcourse na kujifunza upya udereva, akapelekwa kwa psychologist na kupimwa kama ni mzima kichwani na hana ugonjwa wa akili ambao unaathiri concentration yake na psychologist ataamua kama yuko sawa au la, au hata kushitakiwa na kufungiwa kuendesha gari tena nchini japani na ni maisha yake yote.

Huo ni mfano mdogo tu watu walivyo kuwa makini, dereva mmoja mzembe anaweza kuuwa hata watu 30, tuache mchezo na haya mambo, hapa ndipo nilitegemea serikali ya tanzagiza ionyeshe kama ipo kazini na siyo kukimbizana na hawa watu, serikali nzima inakwenda kusikiliza maoni ya dereva? wtf ...
 
Yaani hawa haters (chadema, yaani nyumbu) wa Samia kusema ukweli ni wapumbavu sana, wao ni kuunga mkono tu chaos yoyote wanayoamini itaitikisa serikali.....labda wataingia wao madarakani na chiba wao😅
Mbona unaandika upumbavu? Walio goma si ndo hao matajiri walio ichangia CCM wakati wa kampeni?
 
Lete na mlinganisho wa RUSHWA hapa pia tuone?!
 
YAani serikali wa ignore madai ya madereva? Wale ni watoto kwamba allegations zao ni za kutungwa?

Pale watu wazima wanaendesha haya mabasi, behind them wanafamilia . Hakuna dereva anaamka kwenda kuua watu, anaamka kwenda kuangusha basi la tajiri ambayo ndio ofisi yake

Am nor saying wako right kuna baadhi but wana deserve kusikilizwa si kutumia nguvu

Culture ya japan ni very very different, huwe apply sheria zao bongo is why hata wao hawawezi copy sheria zetu
 
Acha kufananisha kulipia na ustaarabu na kulipo na uharamia.
 
K
Yaani hawa haters (chadema, yaani nyumbu) wa Samia kusema ukweli ni wapumbavu sana, wao ni kuunga mkono tu chaos yoyote wanayoamini itaitikisa serikali.....labda wataingia wao madarakani na chiba wao😅
Kwani Japan askari wanapokea rushwa barabarani hadi wanapigwa picha kama inavyotokea hapa ?

Chadema imeingia vipi kwenye biashara ya mabasi na rushwa barabarani.
 
Tukiishi kwa kuruhusu wataalamu wafanye kazi zao kwa weledi na wanasiasa wakajitenga na kuingilia masuala ya kitaaluma hakika hili Taifa litafika mbali.
Haiwezekani mtu aliyechaguliwa kwa sifa ya kujua kusoma na kuandika tu, eti anaenda kumvimbia mbobevu wa kukusanya kodi ili kupata political millage.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…